Uchaguzi 2020 Kuona ni Kuamini: Je, Oktoba 28, utachagua nini kati ya unachoona kwa macho kitu cha ukweli kilichopo vs ahadi tupu? Msikilize Masanja Mkandamizaji...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,790
117,278
Wanabodi,

Sisi wana tasnia ya habari, kwenye uchaguzi huu, zaidi ya kuwahimiza watu na kuwahamasisha, hiyo tarehe 28 October, wajitokeze kwa wingi, kwenda kupiga kura, na kuitumia haki yao ya kidemokrasia, kuwachagua viongozi wanao wataka, media pia tuna wajibu wa ziada wa kuwaelimisha Watanzania, to make an informed decisions, wachague viongozi bora, watakao waletea maendeleo, na kuchagua vyama vyenye uwezo wa kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

Sasa kwa vile uchaguzi wa mwaka huu una ushindani mkubwa kati ya kuna chama chenye uwezo, the ability, the capacity and the capability ya kuwaletea Watanzania, maendeleo ya kweli, ambacho kiliahidi, na kimetekeleza, halafu kuna msururu vya vyama vya ahadi tuu, ili Watanzania waweze kufanya an informed decisions, tuwasaidie kuona vitu visivyo onekanika, kuona ni kuamini, tuwasaidie Watanzania waone, kisha tuwape uhuru wa kuchagua, ama wachague kitu cha ukweli, kinachoonekanika, au wachague ahadi tupu kama tulivyo ahidiwa mbingu na peponi.

Last week, nimekutana mahali na Msaanii Masanja, Mkandamizaji, msikilize kwa makini, anasema nini na anawashauri nini Watanzania.

Kwa faida ya wale wenzangu na mimi, ambao bundles na ku play video clips ni issue, naomba kuwasaidia, kwa kifupi Masanja anasema, ukimsikia mgombea anasema ataleta maendeleo, usiishie kusikiliza tuu ahadi za kuleta maendeleo, pali mfanyie huyo mgombea the simple assessment test ya his/her ability, capacity and the capability ya kuwaletea maendeleo, kwa kuangalia personal development yake, amewahi kufanya nini, kujenga nini au kuleta maendeleo gani, ukiona ana kitu cha kuonyesha, then mchague, atawaletea maendeleo ya kweli kwa sababu ameonyesha uwezo. Lakini kama hana chochote cha kuonyesha, ambacho alikwisha fanya, then ujue mgombea huyo ana piga tuu blah blaha lakini hawezi kuleta maendeleo yoyote.
Hivyo kwanza ona,


Kisha Amini na tarehe 28 October, ufanye uamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi wa ukweli, wa kuleta maendeleo ya kweli, kutoka vyama vya ukweli vya maendeleo.

Paskali
 
Nimesoma heading tu, nikaamua kukoment bila kusoma kontenti maana najua umeandika ugoro.

Kwani 2015 alipochaguliwa Magufuli, ahadi zake zilikiwa zimeshaanza kutimizwa?

Kama tulivyomchagua Magufuli huku akiwa hajawahi kuahidi na kutimiza hapo kabla(maana hakuwahi kuwa Rais kabla ya 2015), ndivyo nitakavyomchagua Lisu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais lakini ambaye naona hatakuwa na serikali iliyojaa USHAMBA NA ULIMBUKENI WA MADARAKA.
 
Oct 28 Kura zote kwa JPM!
1603376744221.png
 
Hii ni clip mbaya sana kutoka kwa kada Pascal Mayalla

Kama unataka watu waamini kwamba kuna kitu kimefanyika, basi umasikini unaonekana baada ya miaka 60 ya uhuru nao ni kitu kimefanywa na watu wale wale wanaokuonyesha jengo.

Pili, kuna wapinzani walioahidi tu wakiwa hawana kitu. Mfano mzuri ni Dr Slaa pale Karatu. Huyu ndiye aliyefungua macho watu kwamba, unaweza kuahidi ukiwa huna kitu na kisha ukatengeneza kitu.

Ndivyo ilivyo katika sehemu nyingi tu ambako hakuna tofauti ya maendeleo ya chama tawala na wapinzani.

Kenya waliipiga chini KANU. Hawakuwa na kitu lakini Kenya ipo inaendelea. Zambia waliipiga chini ya Kaunda, hawakuwa na kitu lakini Zambia ipo na inaendelea.

Hivyo basi ukijivunia jengo, jivunie umasikini wa nchi. Yaani nchi masikini sana duniani

JokaKuu tindo Mag3
 
Back
Top Bottom