Wito kwa wana CHADEMA wote!

Haya yote nataka kuyasikia baada tu ya CDM kuwa Ikulu late 2015. Tutaongea vizuri kuhusu katiba ya chama na wapinzani wetu ccm watatusaidia kujilekebisha vizuri wakati huo.
 
Mwenyekiti wa NGO na katibu wake huwa hawabadiliki, wanaobadilika ni wanachama tu. stukaaa!!!
 
 
Umerudishiwa kompyuta yako...au umeazima/nunuliwa/nunua nyingine...maana taarifa zilizopo PC yako ilikuwa chini ya uchungunzi wa ITs wa CDM. Ila una hoja ambazo zinahitaji majibu makini....viginevyo msemo wa Wassira kuwa CHADEMA maji ya shingo unaweza uwe na mashiko, nisingependa hilo litokee.
 
kama angekuwa ni jk ana nyumba marekani, uingereza, afrika kusini, na dubai, cjui mngesemaje!! maana chadema kwa kujadili watu wengine ndo sera zao. na sasa mnamjadili zito, badala ya kujadili mapato na matumizi ya chama chenu. mkija kushtuka mmetafunwaaaa
 

JK maisha yake yote amekuwa ni mwanasiasa. Mbowe anafanya biashara maisha yake yote. Kama huna akili inayosukumwa kwa 7000 utaelewa tofauti zao. JK hajakatazwa kujenga hata Makka akitaka. Tatizo ni uhalali wa fedha za kujengea huko nje.
Ukikutana na ushahidi wa fedha haramu za Mbowe leta hapa jukwaani tumdadavue
 

Usiseme ana hoja. Sema ana propaganda zinazohitaji majibu
 
 
hizo ni hadithi za bunuasi or fisi na sungura, Chadema ata wabunge 25 hawatafika na amini majimbo yote ya mjini yanaludi Ccm. kufanyika kwa uchaguzi chadema ni lazima kumbukeni Chadema ni Taasisi, lazima uchaguzi uweopo.

Ccm wanahangaika sana lakini mbowe na dr slaa sisi kama Chadema tunawakubari nyinyi mbulula semeni lakini wataongoza mpaka ushindi 2015
 
Chadema lazima wakubali kukosolewa, kuna jambo la chadema kuwezesha ofisi zake za wilayani na majimboni muhimu sana! Kuna mikoa kama lindi, mtwara, ruvuma, iringa, rukwa na tabora, ni vizuri wakaiangalia kwa upana zaidi.
Mimi nadhani fedha wanazopata CDM ni chache sana kulinganisha na mahitahitaji ya kuhudumia ofisi za wilayani. Sisemi hawatakiwi lakini nadhani hata hizo ruzuku hazitoshi. Kama tunataka wilaya na mikoa ihudumie ofisi zake vizuri lazima wanachama wilayani na mikoani wajitolee. Nadhani fedha nyingi zinazotumiwa na chama zitakuwa zinatoka kwa viongozi wakuu hasa Mbowe na wachache wao, hili si jambo jema kwa chama kama kinataka kujijjenga kama chama imara cha siasa.
 

chadema si waaminifu hakuna hata sura ya kiongozi wa chadema inayofaa kuwa rais 2015,wote wamekaa kwa kuiba iba tuu,kuna watu wao wakisikia jambo flani wao ni kupinga tuu wakizingizia ni mamluki,ngoja watu wajitafunie mihela mnayochanga,we pinga kila jambo na wakati hata fom ya uongizi wa chadema hujui ipoje,katibu msaidizi wa chama anakuambua kuwa hakuna ripot ya fedha wewe unasema hawakupewa nafasi wazungumze ,wazungumze nini? kila kitu kuzungumza tunataka vitendo,mamilion ya sabodo na yako yamejenga majumba south,kenya hahahaa
 
Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnalewa viroba hadi uwezo wenu wa kufikiri unapotea. Hoja iliyotolewa ni nzuri sana. Mnapaswa kuitafakari kwa kina

na tatizo lenu wafuasi wa ccm mna ugonjwa wa kupakatwa.
 

Rejea dhana ya ukuaji wa shughuli za chama DUNIA nzima siyo Tanzania peke yake, Ruzuku haijawahi kujenga ofisi au kukiinua chama chochote Tanzania, baada ya awamu ya kwanza na kidogo ya pili ambapo ofisi za CCM mikoani na kwingineko serikali ilihusika kutoa fedha au kutaifisha majengo hayo.....Ruzuku ni kiini macho kinacho pewa uwezo usilo kuwa nao eti iendeshe shughuli zote za Chama mpaka mikoani?

Ikumbukwe Ruzuku hutolewa na serikali kuu ambayo kwa zaidi ya miaka 50 inajiita "sekretarieti ya CCM"
inawezekana vipi tuamini CCM inatoa fedha kukijenga CHADEMA?

Huko Morogoro kufungwa makufuli ofisi za CDMM ndiyo picha halisi ya Uanachama wa watu wa eneo husika, uhai wa Chama unatokana na Ushiriki wa watu na kujitoa kwao, unapoanza kutumia fedha ili ionekane ofisi ipo mahali hapo hiyo siyo uvuguvugu wa siasa bali ni ubaridi kwani itakua unaajiri watendaji ambao kimsingi hawana mamlaka ya kiutendaji zaidi ya shughuli za ukuaji wa chama jambo ambalo linahitaji zaidi ushiriki wa kila mwanachama na siyo ruzuku.

Hebu sote tuwe wanahisabati.....ruzuku hutolewa kwa kuzingatia idadi ya wabunge Bungeni (Bunge la Muungano) ... CHADEMA Ina wabunge pungufu kidogo ya asilimia 20% ya wabunge wote Tanzania. Km tunajua nini maana ya hesabu hii ya ruzuku ..... hata kwa mtoto hata wa darasani la Saba atajua haitoshi kwa Tanzania nzima km uwiano ndio huo.... km asilimia 20% ya wabunge wanaweza kuzalisha ruzuku ya kukiendeaha Chama Tanzania nzima basi itakapo fikia asilimia 60% basi chama kitakua na majengo mpaka india...!
 

Wewe ndio umeongea vizuri.... ili uwaone viongozi wa CDM hawafai lazima uwe na ufikiri huu "hakuna sura ya kiongozi wa CHADEMA inayofaa kuwa raisi"..... inaelekea mwenzitu unapenda sana sura ...!

Wana CCM wote wa leo wako km wewe ... ufahamu wa kisiasa kwao ni mwiko ..... wao wamezoea vijembe ka vya taarabu hivi eti ndio uwezo wa utawala ka nape alivyo....au mwigulu...au kinana ..... au hata kikwete (anayeshangiliwa kwa vigelegele mikutanoni).

Yaani sina hakika hata km utanielewa... ila dawa ya kuhangaika na mjinga nikuwa mwerevu tu...! hata km utaona (mwerevu) haueleweki kauli za mwerevu zinaishi hata baada ya uhai wake. Kwa hiyo hata wapuuzi wakionekana kuishinda ...... sauti ya mwerevu asiye hai huzishinda hila na fikiri za wajinga..... Mfano kuna watu walio hai ambao wanahangaika na sauti ya Nyerere mpaka leo na ngoma nzito kuishinda sauti ya aliyesimamia utu na haki.
 
Hapa ndipo palipo na ajenda ya SIRI.... KWA NINI MACCM wote tena wale ambao hamkufuata sera bali ajenda ya siri mtu mzuri ndani ya CDM ni ZITTO?... WHY??!!!!!!!!...... KWA NINI?!!!!...
 
Hapa ndipo palipo na ajenda ya SIRI.... KWA NINI MACCM wote tena wale ambao hamkufuata sera bali ajenda ya siri mtu mzuri ndani ya CDM ni ZITTO?... WHY??!!!!!!!!...... KWA NINI?!!!!...
 

Capt Tamar,
umekuwa very bias sana na bila shaka ni kwa kuamua kuw mvivu kuisoma vyema taarifa hii. Pamoja na kuwa pro Chadema sana tu, lakini hoja yake huyu bwana ni ya msingi sana, Kiongozi hata kama angekuwa ametuvusha na kutufikisha tunapopataka napaswa kuwa mwadirifu tu, na ni kwa mantiki hiyo basi, hawa watu kama wamekosa uadirifu wakati muhimu kama huu ambapo tunapaswa kupiga kelele za ufisadi, wivi wa rasilimali zetu, rushwa nk, vile vile walipaswa kuongoza kwa mifano/vitendo.
Huyu bwana si mamruki kama wengi wanavyotaka kuaminishwa, the problem ninayoiona kwake ni namna ambavyo amewasilisha, platform haikuwa sahihi, hata kama kuna uhuru wa kutoa maoni, lakini lazima kupima nafasi yako kama kiongozi na madhara yapi yanaweza kusababishwa na namna ya utoaji habari. Lakini bottom line, ukweli unapswa kubaki kama ulivyo na kufanyiwa kazi.
 
Pale Bukoba mwaka wa uchaguzi uliopita kuna mgombea wa chadema misenyi alijitoa kugombea baada ya kunyimwa msaada katika harakati za kugombea ubunge, baada ya nguvu kupewa Rwakatale tu. I wish huo ni udhaifu, jamaa aliacha, akaendelea na mambo yake. Nafikili wanachama wa chadema mnaugua ugonjwa wa wanachama wa CCM wa kutokubali ukweli. Vyama vimewaharibu vijana, hawawezi ku argue tena, wanataka kufikili kama wanasiasa. Nafikiri kuna haja ya kutafakali kauli hii, na mkumbuke kilichoiua CCM ni makundi siyo umaarufu wa chadema. Umaarufu wa chadema umetokana na ubovu wa CCM, ndo kusema CCM akitokea mtu akachange mwelekeo wa chama, watu wake watarudi. Huwezi kuamini, ila mpasuko kwenye vyama ni hatari. Sipendekezi afukuzwe, ila kama katiba inasema ni miaka 10, lazima kuheshimu hata kama bado umri unaruhusu, na kama kweli katiba imebadilishwa kinyemela, ni hatari, ni kma yale wanayolalamikia ya serikali kubadili vifungu kinyemela. Someni katiba zote muangalie vifungu hivyo vipo na kama ni kweli vimeondolewa, mtaelewa kama jamaa ni pandikizi. Kauli za chadema kumshambulia zito hata mie nimezisikia laivu kwenye vyombo vya habari, mengine yana ukweli hata kama si sehemu sahii ya kuyawasilisha.

Jmaa mwingine nilisoma thread yake akilalamika kuwa si vema kuwachangisha watu kwenye mikutano eti wasaidie kuendesha chama, wakati watu wanapanda chopa, wakati magari yanatumia gharama nafuu kuliko chopa. Think
 

kama kuna ukweli hapo basi CCM kutoka madarakani itakuwa ni kama ni ndoto za alinacha duuuuuuuuuuuuh pia naomba hao makatibu wa wilaya na mikoa wadhibitishe kweli kama hawajapokea hizo fedha au na huyu naye anahasira zake na kiongozi fulani ndio akaona bora aje amalizie hapa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…