Wito kwa wana CHADEMA wote!

Wito kwa wana CHADEMA wote!


Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa.
ZeMarcopolo, tunalazimika and jerrytz like this.
 
Erythrocyte
===>Mimi naamini hapa kuna hoja,na inawezekana viongozi wa CDM hawajalitolea ufanunuzi hili suala,
===>Lakini viongozi wa CDM lazima wajue kuwa wao ni viongozi tu na pia wapo wanachama ambao wanahitaji kujua nini kinachoendelea kwenye chama chao.

Wanachama wenyewe ndo sisi, at the Moment tuko Happy na Uongozi wa Chama Chini ya Mbowe.
Asilani, CCM hawawezi kutuchagulia Viongozi, naona ma CCM mnataka kutumia hii techinique, kaeni na CCM yenu, tuachieni CHADEMA yetu chini ya Mbowe, kama kuna mtu ndani ya CHADEMA mnahisi anafaa kuwa Mwenyekiti,awe Shibuda ama hata Zitto, Mchukueni mumfanye mwenyekiti wenu, sisi hatutaki
 
Mwita Maranya Tumaini Makene, Curriculum Specialist
===>Mimi bado nasisitiza kuwa ni vizuri tuhuma hizi zikajibiwa kwa ushahidi na sio kwa maneno na chuki kama ambavyo hali hii inaendelea
===>Pili inaonekana ndani ya CDM kuna makundi ambayo bado yanakinzana katika kutafuta nafasi ya kuongoza chama hiki,nafikiri ni vizuri mkatafuta muafaka wa pande zote hizi kwa manufaa ya chama.
===>Sitaki kuamini kuwa aliyooandika Mkulima Maskini yote ni ya uongo la hasha kuna mengine inawezekana yakawa na ukweli wa aina fulani,CDM inaongozwa na binadamu,na binadamu sio mkamilifu wa kila kitu,yale ambayo yanaonekana yana ukweli yafanyiwe kazi na kupatiwa ufumbuzi
===>Suala la uchaguzi inaonekana pia ni nyeti sana,fanyeni uchaguzi kwa kutumia vigezo ambavyo mnahisi havitadhoofisha chama,magamba wamejipanga na naamini wanafuatilia kila hatua mnayopiga na mkikosea tu,kweli 2015 mtaisikia kwenye bomba
 
Last edited by a moderator:
Lakini anayoyazungumza jamaa kama yana ukweli flani hivi ndani yake.

Unajua hapa Morogoro mjini maeneo ya Bigwa ninakoishi kuna Ofisi ya CHADEMA kata ya Bigwa ilifunguliwa na Dr Slaa miezi kama mitano hivi iliyopita cha ajabu ni kwamba sijawahi kuiona hiyo Ofisi ikifanya kazi yaani wakati wote imepigwa kufuri sasa ukiangalia na hizi tuhuma za kwamba kuna pesa zinatolewa kwa Vyama vya Siasa kwaajili ya kuendesha shughuli za Siasa Mikoani kwamba hazifiki na hazieleweki zinakwenda wapi zinanifanya niamini hizi tuhuma na kwa utaratibu huu sidhani kama CHADEMA tutaitoa CCM madarakani kama Viongozi hawa hawatakuwa tayari kuziwezesha Ofisi za Mikoani kifedha ili ziweze kuendesha harakati za kisiasa za Chama.

Viongozi wa Kitaifa wanapaswa ku-concentrate katika katika mambo ya Chama yaliyo na sura ya Kitaifa zaidi kama vile Viongozi wa Taifa wa Chama kujitokeza zaidi katika Media na kunadi mawazo na sera mbalimbali za Chama wakati Viongozi wa Mikoani wakiandaa mikutano,Semina & Makongamano mbalimbali ya kukieneza Chama

Acha kuhara usichokijua!ofisi ya Bigwa ni ya CHADEMA JORDAN.ilivyofunguliwa wanafunzi ambao ndio waendeshaji wakaenda likizo.Ulitaka uachiwe wewe ukakenue magego yako pale?Akili finyu kama zako ndizo zinachelewesha ukombozi wa nchi hii!kila upepo mnaudaka hamna pa kusimamia
 
Baada ya Video feki sasa mmekuja na la matumizi ya vyama. Nilikuwa naangalia walengwa ni kina nani katika hili, sasa nimetambua kumbe hapa yawezekana wanaolengwa haswa ni CHADEMA kupitia mamluki wao ambao pia wapo kwenye safu ya uongozi wa juu lkn pia wanakula sahani moja na CCM, wakuu wa kaya na wakuu wa intelijensia. Ngoja tuone safari hii mambo yatakuwaje. Hii ya sasa itakuwa kali zaidi. Lkn bado ninawasiwasi kama upande wa mamluki utashinda.

....Mkuu tayari tumeshamtupa nje.....
 
Huyu Mburula eti anasema hajui fedha inatumikaje wakati chama kimeenea nchi zima na tutalaunch chadema digital muda si mrefu.. Mwigamba ni mtu mpuuzi sana..

Jamaa ana kesi ya 'WARAKA KWA ASKARI WOTE', Ccm na serikali watakuwa wamemhonga na kumuahidi kufuta kesi ili asaidie kuvuruga chama. Ndiyo majuzi walianza kutoa taarifa kuwa Chadema itasambaratika soon!!! Oh... Mwigamba!! L.u.k.u.v.i kakudanganyiani?
 
Bwana Maskini mkulima ulikua unatania CDM haya sasa kiatu hicho kimesepa umekiri mwenyewe.
 
Unajidanganya mtoa mada, chadema haitadhoofishwa kwa kuandika porojo kama hivi.

Unakiri kuwa Mbowe na Slaa wameipa mafanikio makubwa chadema wakati huo huo unataka viongozi hao wa punzishwe.

Wewe sio mwanachama wa chadema wala sio mamluki, wewe ni gamba tena gumu lililoshindikana. Umeipekua katiba ya chadema ukaona hiko ulichokiandika ndio ukitumie kukamilisha azma yako. Umegundua kuwa katiba imara ya chadema imekifanya chama kusonga, unatamani hayo unayoyapenda yangekuwepo katika katiba ya chadema!! USHINDWE!! mwizi mkubwa we.

Tena huyu sio TEAM BUKU SABA, huyu ndiyo yule mgawaji buku saba pale lumumba naona ameona vijana wanachukua hela bure bila kuleta mafanikio wanayoyakusudia hivyo ameamua aje mwenyeye!!
 
Baada ya kusimamishwa katibu msemakweli w chadema mh mwigamba kwa kuhoji ukweli juu ya viongoz masultan ndani ya Chadem (mbowe na slaa) kuwa wamachomoa kipengele cha katiba kinachosema kila kiongoz awe na ukomo wa miaka mitano kwa awamu mbili.

Kijana huyu ameshindw kueleza kwa uwaz kwani akizungumza angefukuzwa! Alafu ndio wanasema hiki ni chama cha Demokrasia.

Naanza kuamini kuwa ZITTO sio mbaya kwa chadema. napia naanza kuamin kwa halii bora LOWASA 2015 kuliko SLAA NA MBOWE kuwa viongoz wa nchi yetu. ukweli ndio huo hata ukibisha we zombi. ngoja nitafute softcopy ya katba niwaekee muone.
 
Hoja siyo tu kwa nini wabadilishe kipengele cha katiba kinyemela, bali why are they ruling with an iron hand and kangaroo committee.

Chama kilichoanzishwa kwa misingi ya kilaghai hata utendaji utakuwa niwa kilaghai.
 
Hoja siyo tu kwa nini wabadilishe kipengele cha katiba kinyemela, bali why are they ruling with an iron hand and kangaroo committee.

Chama kilichoanzishwa kwa misingi ya kilaghai hata utendaji utakuwa niwa kilaghai.

Mkuu nina imani huyu mwigamba leo atafnya press ....ili nayeye tumsikie atakachokizungumza kwa upande wake!!manake hapa jamvini machadema wanakuja na majungu tu!!mwigamba kama unanisoma tunaomba leo uitishe press conference tujue mbivu na mbichi!!ila ningeomba uwataje wale viongoz waliokuwa wanalipuwa mabomu kwenye mikutano na kusingizia jeshi la polisi
 
MTOTO KITAA
===>Mimi hapa ndio panaponishangaza,tangu jana suala hili la Mwigamba lilipoibuka watu wengi waliomba kuwa hata kama atafukuzwa je hoja alizotoa pia ni za uongo?
===>Suala la kutofanyika kwa uchaguzi pia ni la uongo?kwa kweli hata sisi mashabiki wa CDM tunaanza kushikwa na ka uoga kuhusiana na hali ya mambo ndani ya CDM,
===>Pamoja na yote haya naanza kuhisi kuwa CDM hasa viongozi hawasikilizi maoni ya wanachama wenzao,na pia inawezekana kabisa ukiongea kitu ambacho hakimfurahishi Mbowe au Dk Slaa basi wewe ni adui na ni muasi wa chama,kwa sababu kwa maelezo aliyotoa Tumaini Makene jana kuwa Mwigamba alikisifia chama kwa kutekeleza ahadi za chama vizuri,na muda huo huo akaposti tamko lililosababisha akaondolewa hii inaonekana kuwa ukisema kitu tofauti na kile ambacho viongozi hawakifurahii basi unaondolewa madarakani
===>Taratiibu naanza kumuna Zitto kama kiongozi makini na mvumilivu sana ndani ya CDM,
===>Mbowe na Dk Slaa tunaamini mnahusika kwa namna moja ama nyingine kwenye mgogoro hasa kwa nyie kuendelea kukaa madarakani bila kufuata taratibu na sheria za chama,mkijifanya mnajua na kuanza kufukuza watu ambao wanahoji yale ambayo mmekuwa mnayakosea basi mkae mkijua CDM itawafia mikononi mwenu,si lazima kwa Mbowe au Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015,au kuendelea kukaa madarakani maisha,waacheni wana CDM waamue wenyewe,kama wana CDM wanataka nyie muwe wagombea hilo halina ubishi mtakuwa tu,lakini taratibu zifuatwe ili kukinusuru chama.
===> Kitila Mkumbo,Prof Safari na wengineo wasaidieni hawa viongozi wa CDM na huu ndio wakati wa kuwa pamoja kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014,kama msiporekebisha haya itakula kwenu mapema sana.
 
Last edited by a moderator:
Erythrocyte
===>Haya ni ya kufanyia kazi,mna ushahidi gani kuwa yametoka lumumba?
===>Mnafikiri wanachama wenu hawana malalamiko?misuguano na mijadala tofauti katika taasisi kama CDM ni ya kawaida,kikubwa hapa ni kufanyia kazi suala hili,na kama limeanza kuongelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha mji ambao ni ngome ya CDM basi ujue suala hili sio dogo kama ambavyo wanafikiria
===>Na ni vizuri busara ikatumika kulitafutia ufumbuzi badala ya kuanza kufukuzana.

Jiaminishe kuwa hili bandiko ni la Lumumba katika mkakati wao wa kuisambaratisha CDM
 
Tulingo'a madiwani,Tukang'oa bi shonza na sasa ni Mwigamba.
" @Our way or highway''
 
Baada ya kusimamishwa katibu msemakweli w chadema mh mwigamba kwa kuhoji ukweli juu ya viongoz masultan ndani ya Chadem (mbowe na slaa) kuwa wamachomoa kipengele cha katiba kinachosema kila kiongoz awe na ukomo wa miaka mitano kwa awamu mbili.

Kijana huyu ameshindw kueleza kwa uwaz kwani akizungumza angefukuzwa! Alafu ndio wanasema hiki ni chama cha Demokrasia.

Naanza kuamini kuwa ZITTO sio mbaya kwa chadema. napia naanza kuamin kwa halii bora LOWASA 2015 kuliko SLAA NA MBOWE kuwa viongoz wa nchi yetu. ukweli ndio huo hata ukibisha we zombi. ngoja nitafute softcopy ya katba niwaekee muone.

Chd sio chama kinachokumbatia mafisadi au uovu ukikosa utaadhibiwa bila kujali ww ni Chenge, Lowassa, Ngeleja au Rostam ndio tofauti na chama cha majambazi. Mtasema sana lakini Mbowe na Slaa ni kiboko yenu. Ilo mnalijua kwani ndio mana maneno mengi na mmejaribu sana kuwahonga lakini hakuna kitu. Mbona hamzungumzii cuf, nccr, tlp tatizo lenu mkikamatwa mnataka kuwachagulia watu viongozi katika vyama vyao. Kwani wanachama wa cdm wamelalamika. Mnapandikiza mamluki mkitegemea kuivuruga cdm, ndio mana mlisema cdm haifiki 2014 mkiwategemea watu kama hao. Yeye ni mwenyekiti tena wa kanda alishindwa nn kuwakilisha mawazo yake kwenye vikao vya chama. Hapa ndio mjue cdm wako juu hakuna alie juu ya sheria. Mtabaki kusema oh Mbowe na Sla ni viongozi wa kudumu na ss wanacdm tunasema watakuwa wa kudumu mpaka Tanganyika ipate uhuru. Hata marehemu baba wa taifa alikaa miaka kibao kabla hajamwachia Mwinyi. Mbona hamsemi unajianya kumbukumbu huna.
 
Unaanzisha wewe uzi, unajijibu mwenyewe zaidi ya post nne kisha unaendeleaaaa,

Haya, Mwigamba hajafukuzwa bali kasimamishwa tu kwaajili ya hatua za kinidhamu
 
DOes the ID of this member change anything to his content? Kwangu mimi ni eye opener maana huyu mtu anajua anacho kiongelea, tokana na nafasi yake ndani ya Chadema. angekkua kaongea mtu mngine ningebisha. Na kuonesha kua aliyo sema yanaweza kua kweli amesimamishwa kazi baada ya kupigwa mangumi!

Mwali tulia, habari kama hizi zinatafuta waparamiaji.

1. Ni kweli kuna hiyo komputa iliyotumika pamoja na kueditiwa. Lakini hata hiyo ni homework ndogo ambayo itafanyika kuthibitisha kuwa ni mwigamba

2. Mtuhumiwa mwaigamba si mhalifu mpaka tuhuma zithibitishe

3. Ukishaona mtu analeta mambo ya ndani ya nyumbani kwake, basi ujue huyo si riziki

4. Bado naamini mbinu iliyotumika na lengo la hili bandiko linaamsha hamasa ya wanao tapatapa kujaribu mbinu mbali mbali

Nakukumbusha wiki

CHADEMA ITASAMBARATIKA

WITO WA WANACHADEMA WOTE

MWIGAMBA AKAMATWA NA POLISI

Hizi ni mbinu mufilisi za mfa maji

Mwisho huu mwito hauwezi kutoka Lumumba

Haya soma hapa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...hwa-uongozi-baada-ya-kukiri-kusema-uongo.html
 
Back
Top Bottom