Wito kwa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari (tafadhali someni)

inasikitisha sana. madaktari na polisi wanashudia maajabu. wangekuwa wanapiga picha na kuziweka hadharani sijui ingekuwaje.
 
Jamani mi napenda kujua ivi inakuwa mtu anakufa kwa ajali mbaya kama ile alafu wewe unachukua ile picha yake ya ajali unaiweka kwenye mtandao huu wa JamiiForum na wana jamii wanao monitor ii forum hawachukulii hatua yoyote. Mi nilitegemea kuwa wangeweka picha yake kabla ya kifo chake wakati anafanya kazi zake. Ivi watanzania tunajua kweli maadili ya izi forum????, huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana, na napenda kuwauliza nyie wamiliki wa wana jamii ivi kama mama yako amesikika kuwa amebakwa na ikatokea tukaweka picha yake humu wakati akibakwa utaiwacha kweli watu waanze cocomments!!!! Mi nafikiri ifikie muda hao wamiliki wawape elimu wanao monitor huu mtandao wajue wanalolifanya. Mi nawasilisha hoja tu na kama mkiamua mnifute kwenye hii forum poa ila swala kama lile la kuruhusu picha ya mtu aliyeumia kama vile halikubaliki kabisa na mnaitaji kujifunza na matukio yanayotekea kama haya uko nje huwezi kukuta upuuzi kama huu !!!!!!!!
 
Kusema kweli mie sijaona tatizo la kuweka picha..Habari katika picha huwa zina ujumbe mkubwa sana na zinajaribu kutupa uhalisia wa hali halisi sisi ambao hatukuwa kwenye tukio..Na Isitoshe kuna matukio mengi tu ya jali na mambo mengine huwa picha zinawekwa hapa..
 
Naomba nitajie mtu maarufu yoyote duniani aliyekufa kwenye matukio kama yale na kuwekwa mitandaoni picha kama ii, We Zio unasema hivyo ila fikiria kama ndugu yangu ndo anadhalilishwa hivi mitandaoni ungejisikiaje?
 
kwani tatizo liko wapi hakuna uzalilishaji wowote inamaana hiyo picha ilikua inatisha sana kuliko zile zinazo wekwa wa2 wakiwa uchi hao nao utaseje kama unadai hii amedhalilishwa
 
Naomba nitajie mtu maarufu yoyote duniani aliyekufa kwenye matukio kama yale na kuwekwa mitandaoni picha kama ii, We Zio unasema hivyo ila fikiria kama ndugu yangu ndo anadhalilishwa hivi mitandaoni ungejisikiaje?

Kumbe wewe usichotaka ni picha za watu maarufu ndo sisiwekwe? Ila za waendesha bodaboda na watu wengine wa kawaida zikiwekwa hakuna neno!!
 
Naomba nitajie mtu maarufu yoyote duniani aliyekufa kwenye matukio kama yale na kuwekwa mitandaoni picha kama ii, We Zio unasema hivyo ila fikiria kama ndugu yangu ndo anadhalilishwa hivi mitandaoni ungejisikiaje?
Sasa huo udhalilishaji upo wapi hapo?? Mbona husomeki..Muwacheni marehemu apumue huko peponi/motoni sijui
 
Naomba nitajie mtu maarufu yoyote duniani aliyekufa kwenye matukio kama yale na kuwekwa mitandaoni picha kama ii, We Zio unasema hivyo ila fikiria kama ndugu yangu ndo anadhalilishwa hivi mitandaoni ungejisikiaje?

We umekaririshwa na Dina Marious huu upuuzi.
Kuna tatizo gani wakati watu wanajifunza kutokana na makosa? Watu tushajua madhara ya kutokufunga mkanda kutokana na picha zile.
Acha kushikiwa akili. Marehem angekua mkristu, angetolewa mochwari na kuwekwa hadharani apigwe chabo, je huo ni udhalilishaji?
Kamuulize Gadafi au Sadam Husein kama unastaka mpaka wengine wafanye ndo wewe uone halali.
 
Jamani mi napenda kujua ivi inakuwa mtu anakufa kwa ajali mbaya kama ile alafu wewe unachukua ile picha yake ya ajali unaiweka kwenye mtandao huu wa JamiiForum na wana jamii wanao monitor ii forum hawachukulii hatua yoyote. Mi nilitegemea kuwa wangeweka picha yake kabla ya kifo chake wakati anafanya kazi zake. Ivi watanzania tunajua kweli maadili ya izi forum????, huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana, na napenda kuwauliza nyie wamiliki wa wana jamii ivi kama mama yako amesikika kuwa amebakwa na ikatokea tukaweka picha yake humu wakati akibakwa utaiwacha kweli watu waanze cocomments!!!! Mi nafikiri ifikie muda hao wamiliki wawape elimu wanao monitor huu mtandao wajue wanalolifanya. Mi nawasilisha hoja tu na kama mkiamua mnifute kwenye hii forum poa ila swala kama lile la kuruhusu picha ya mtu aliyeumia kama vile halikubaliki kabisa na mnaitaji kujifunza na matukio yanayotekea kama haya uko nje huwezi kukuta upuuzi kama huu !!!!!!!!

Sa ishu ya kubakwa na maiti mochwari wapi na wapi?
 
Huo ni upuuzi,unaweza kutoa habari ila si kwa kuweka picha, kama ni ndugu yako angefanywa vile ungekubali, uu ni ulimbukeni wa media, Tanzania need IT policy ya haya mambo
 
kwa kawaida mtu akishafariki, sisi tuliobaki hatuna budi kuongelea mambo/matendo yake mazuri aliyokuwa akitenda, kwa mtazamo wangu mdogo nilionao, sio sahihi kuweka picha ya mtu iliyochukuliwa akiwa ameshafariki kwani zipo picha ambazo zilichukuliwa akifanya mambo mazuri kabla ya kufariki.
Ni vizuri mtu akifariki kuweka picha ambayo haiwezi kumkwaza mtu mwingine, watanzania tuelimike jamani, hebu jaribuni kufungua blog yoyote uangalie habari yoyote kuhusu hayati mwalimu julius kambarage nyerere kama utaona picha iliyochukuliwa akiwa amefariki. ''TUELIMIKE WABONGO''.
 
umbeya tu. Hakuna blog yoyote walioweka picha

Picha ipo kwenye TEENTZ, lakini pia mchango wangu kwa hili nalipinga kwa asilimia zaidi ya 100 kwani hata dini inayomuhusu marehemu Sharo(R.I.P) hairuhusu mwili wa marehemu kuangaliwa hadharani na ndo maana huwa hakuna kuuaga mwili kama wenzetu wakristo kwa hiyo kufanya hivi ni kukiuka pia misingi ya dini ya Kiislam.
 
Hahahah!ndo yule mtangazaj flan akasema"gari imepinduka watu 9 wamekufa hapohapo na masai 1"kuweka picha hakuna tatizo mbona za Muamar Ghadaf na Sadam Hussein hadi leo zpo,,,anawekwa2 hakuna maarufu wala muendesha bodaboda mbele ya M/Mungu!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tutaamini vipi kama amekufa?huoni kama huo ni uthibitisho?,halafu ulikuwa wapi wakati ule CNN wan expose miili ya watoto wa Saddam Hussein, nadhani nao wanaitaji kupashwa pia.
 
Back
Top Bottom