Wito kwa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari (tafadhali someni)

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
15,385
Points
2,000

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
15,385 2,000
Ndugu zangu,

Kumekuwa na tabia ya kuweka picha za marehemu tena zingine zilizoharibika kutokana na ajali kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari.Binafsi nitoe wito wa kuacha tabia hii ambayo pengine hata sisi tulio hai tusingependa kufanyiwa.

Nimeona nitoe wito huu baada ya kuona picha za Marehemu Sharo milionea kwenye blog moja.Sio kitu kizuri kufanya vile tena bila ridhaa hata ya ndugu.

Tuungane kupinga hili maana pengine sheria zetu zina mapungufu juu ya swala hili.Mwisho naomba wamiliki wa hizo blog watoe picha hizo mara moja kwa heshima ya Marehemu.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
15,385
Points
2,000

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
15,385 2,000
Nafikiri wanaharakati wa haki za binadamu wanaweza kusaidia kushawishi kuwepo na sheria maalum za kudhibiti matumizi ya picha hizi kwenye vyombo vya habari.
 
mtzd

Member
Joined
Jan 29, 2010
Messages
81
Points
95

mtzd

Member
Joined Jan 29, 2010
81 95
Ndugu zangu,habari za wakati huu na poleni kwa msiba wa ndugu yetu Hussein Ramadhan Mkieti lakini alikuwa maarufu kwa Sharo Milionea,kwa majonzi na masikitiko napenda kuweka ujumbe huu kwa wale wote ambao wameweka picha ya Marehemu akiwa tayari ameshafariki tena ikiwa kwnye hali mbaya,kwenye mitandao ya kijamii,twitter,facebook,blogs na kwingeneko.Kwa kweli inaleta majonzi na uchungu sana kwetu tena sana kwa ndugu zake wa karibu,Hebu fikiria ni picha gani wanayoipata ndani ya mioyo yao,na wewe ambaye umeweka picha hiyo kwenye account yako au mtandao wako hebu fikiria angekua ni ndugu yako,ungejisikiaje? Na kingine wengine wameiweka picha hiyo ikawa na maelezo ambayo nadhani sio ya kibinadam,Tafadhali tuwe waungwana kwa familia na ndugu waliopoteza ndugu zao kwa kuwasitiri na picha kama hizo,Wapo waliotoa samahani kwa kuonyesha picha kama hizo lakini pia sio kigezo cha wao kuziacha picha hizo kwenye mitandao yao.Nimesoma kwenye twitter ya mtu anasema eti hata kama asingeiweka yeye eti kwenye magazeti wataiweka kesho,Nimeshikwa na uchungu kweli kwa maelezo yake,wapo waliojaribu kumwomba aitoe lakini hakufanya hivyo.Ndugu zangu linapotokea jambo kama hili ni wajibu wetu ndio kuwapa watu taarifa lakini tuangalie jinsi ambavyo taarifa hiyo tunaiwakilisha kwa jamii.Yapo mengi ambayo ningetamani kuyaainisha lakini nadhani kwa haya machache wengi mtanielewa na kwa wale ambao nadhani wamefanya hivi iwe fundisho kwa wakati mwingine litokeapo jambo wajue jinsi ya kuweza kuliwakilisha kwa jamii.
Mungu ailaze roho ya marehemu Hussein Ramadhan-Sharo Millionea mahali pema .Amina
 
mtzd

Member
Joined
Jan 29, 2010
Messages
81
Points
95

mtzd

Member
Joined Jan 29, 2010
81 95
iweke hiyo picha unayozungumzia tuione
Nadhani hujaelewa niliyoandika ndugu yangu,na we unataka kuwa kama Tomaso,mimi sina na siwezi kuweka picha kama hiyo,ukitaka kuiona itafute .Siko hapa kuiweka bali kuwarekebisha wale waliofanya hivyo.
 
mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Messages
4,435
Points
2,000

mizambwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2008
4,435 2,000

Mkuu Invisible unatoa muongozo gani? Naona zimeshatinga hata humu!
Nafikiri wanaharakati wa haki za binadamu wanaweza kusaidia kushawishi kuwepo na sheria maalum za kudhibiti matumizi ya picha hizi kwenye vyombo vya habari.
Ndugu zangu,

Kumekuwa na tabia ya kuweka picha za marehemu tena zingine zilizoharibika kutokana na ajali kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari.Binafsi nitoe wito wa kuacha tabia hii ambayo pengine hata sisi tulio hai tusingependa kufanyiwa.

Nimeona nitoe wito huu baada ya kuona picha za Marehemu Sharo milionea kwenye blog moja.Sio kitu kizuri kufanya vile tena bila ridhaa hata ya ndugu.

Tuungane kupinga hili maana pengine sheria zetu zina mapungufu juu ya swala hili.Mwisho naomba wamiliki wa hizo blog watoe picha hizo mara moja kwa heshima ya Marehemu.

./././././././../Network searching./././././././././../././././././././
 
Last edited by a moderator:

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Messages
4,435
Points
2,000

mizambwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2008
4,435 2,000
[
B]Binafsi sijaona tatizo,

Kweli tumeondokewa na kipenzi lakini:-

(1) Mbona hatukulalamika zilipowekwa picha humu JF zikionyesha mabaki ya marehemu Mwangosi (Ambazo zilikuiwa ni nyama tu siyo mwili)

(2) Mbona kila mara hapa JF huwa tunapenda ushahidi wa kuwekewa picha ili tuamini, leo imekuwaje tena wajameniiiiiiii!!!!!!!

Twnde mbele turudi nyuma ........ TAFAKARI......... au kama ndio tunaanza leo, hata mimi napenda hiyo sheria / utaratibu upitishwe lakini huko nyuma hatukuwa na utaratibu huo kwenye mitandao yote.[/B]

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
 
CBSai

Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
20
Points
0

CBSai

Member
Joined Apr 1, 2012
20 0
umbeya tu. Hakuna blog yoyote walioweka picha
Naungana na wote WALIOLAANI KWA NGUVU ZOTE kuwekwa kwa picha ya marehemu kwenye mitandao ya kijamii, ni utoto na ulimbukeni wa hali ya juu sana, kama mtu umeguswa kwa namna yoyote omboleza kistaarabu. Moja ya mtandao hao hadi sasa bado wameweka hiyo picha ni http://www.globalpublishers.info/ nenda huko utakutana na hiyo picha, si ustaarabu wala uungwana, marehemu ana heshima zake pleaseeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,689
Points
2,000

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,689 2,000
Wabongo malimbukeni wengi!Mtu kaweza kufungua kiblog uchwara chake basi imekuwa shida, viherehere vimewajaa! Hata weredi wa kutoa habari hawana mburula wakubwa hao. Hata kama mtu kafa lakini heshima yake lazima apewe.
 
Forum statistics

Threads 1,392,768
Members 528,684
Posts 34,117,507
Top