Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,502
- 113,610
Wanabodi,
Mjadala wa IGA ya DPW kupewa Bandari yetu ya Dar es Salaam, unazidi kushika kasi.
Jana asubuhi nilipandisha bandiko hili Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do kuhusu hiyo IGA.
Jana hiyo hiyo ikatokea coincidentally Jukwaa la Wahariri likawaita wahusika wakuu kwenye mkutano na Wahariri, na kujibu maswali ya Wahariri.
Kwanza niwapongeze TEF kwa initiative hiyo, mkutano huo uliotangazwa live na media zetu mainstream na social media, umelisaidia sana taifa katika uelimishaji umma kuhusu jambo hili.
Tangu sakata hili lianze, serikali yetu haijawahi kuwa proactive hata mara moja kwa kujitokeza kuelimisha umma, siku zote, ni inakuwa reactive kujitokeza kujibu hoja.
Miongoni mwa wajibu hoja huo mkutano wa jana ni Wanasheria, kiongozi wa Jopo la Wanasheria, Hamza Johari na Mwanasheria wa Wizara.
Bandiko hili ni wito kwa serikali yetu tukufu na Sikivu, IGA imepingwa kwenye fronts kuu mbili, hoja za Kisiasa, na hoja za Kisheria.
Kwenye hoja za kisiasa ni watu mbalimbali wameibuka ama kuunga mkono ama kuipinga kwa hoja za kisiasa, hoja hizi zikijibiwa kisiasa ni sawa.
Lakini kuna hoja very solid za kisheria zilizotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, na hoja nyingine nyingi za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria mbalimbali, akiwemo Prof. Shivji, Rugemeleza Nshala, Mwambukusi na mawakili wengine wengi.
Hoja hizi za kisheria zimetolewa kwa maandishi zikiandamana na vifungu vya kisheria. Jana nimesikia zikijibiwa kwa kauli nyepesi nyepesi za kisiasa za maneno matupu bila vifungu vya kisheria to back up majibu hayo.
Natoa wito kwa serikali yetu Sikivu, hoja zote za kisheria kuuipinga IGA zilizotolewa kwa maandishi zikiwemo hoja za TLS, Prof. Shivji na Wengine wote Kupinga IGA, zisijibiwe kisiasa kwa kauli tuu nyepesi nyepesi za maneno maneno matupu!, hoja hizi nzito za kisheria, zijibiwe kisheria kwa maandishi zikiambatana na vifungu!.
Kufuatia IGA hii, katika kuiunga mkono, kumejitokeza wanasheria chawa wanaofanya uchawa wa kisheria kuitetea hii IGA.
Na mimi kwa vile ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nami nilitoa hoja zangu kuhusu hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambazo baadhi mpaka sasa bado hazijajibiwa popote!.
Kwa vile IGA ni utangulizi wa HGA, naomba kuendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa kwa kelele hizi, HGA, itakuwa nzuri.
Serikali Ijibu Hoja.
Paskali