Winnie Madikizela Mandela alipokuja Dar 1990

Winnie Madikizela Mandela alipokuja Dar 1990

Achana na Midemu ya Jamii Forums inayojichubua Winie Mandela alikua mzuri mzuri mzuri mno!
 
Huyuu mama hakubahitika kuwa na watoto ???

Ameacha watoto na wajukuu; binti yake mdogo utadhani ni photocopy

620x349


Madiba kwenye harusi ya Zindzi (uzuri uko kwenye damu)..

130626201133-13-mandela-family-horizontal-large-gallery.jpg
 
Papa aliwasili jumamosi jioni, akaenda moja kwa moja pale saint joseph kwa ajili ya misa.

Kesho yake jumapili asubuhi tukaenda jangwani kwa maandamano. Ni kama jana tu lakini naongelea septemba 1990, kina Wema Sepetu na Diamond walikuwa bado hawajui nini kinaendelea duniani.
Kuishi kwingi kuona mengi.
 
Anaweza kulaumiwa kwa mengi! lakini ni mama aliyevumilia mengi kwa mtazamo wangu! aliachwa na Mandela akiwa bado mbichi, Mandela akaenda jela! jamani sitetei makandokando aliyoyafanya lakin kama binadamu alihitaji faraja baada ya mapambano na makaburu. Pumzika kwa amani mwana mwema wa mama Afrika ambaye hukujua kupendwa kwa sababu uliyempenda alikuja akakusaliti kwa kumpenda Graca. aliwasamehe makaburu akashindwa kukusamehe wewe uliyeendeleza mapambano ili asisahaulike gerezani! Yote maisha🙁
Kilichomuudhi Mandela, pamoja na kusahau yaliyopita wakaanza maisha upya baada ya kutoka gerezani, bado alikuwa anachepuka!
Hapa inahitaji mtu mwenye roho ya chuma kuvumilia!
R.I.P. Heroine Winnie
 
Siku moja nilikuwa mitaa flani,

Mara bibi mmoja makadirio kama 70+ hivi nilimuona anafungua app ya JF kwa simu yake nikahamaki,

Nikajifanya kama sijui vile nikamuuliza samahani bibi unatumia application gani hiyo akanionyesha

Ilibidi tu nimtanie kwamba wewe utakuwa Sabinaa mke wa Nyani Ngabu basi bibi wa watu akacheka kinoma

Huu uzi nimeamin kuna wazee sana humu

Halafu nimegundua wengi wao ndo wale wa mashati ya mboga mboga
 
Siku moja nilikuwa mitaa flani,

Mara bibi mmoja makadirio kama 70+ hivi nilimuona anafungua app ya JF kwa simu yake nikahamaki,

Nikajifanya kama sijui vile nikamuuliza samahani bibi unatumia application gani hiyo akanionyesha

Ilibidi tu nimtanie kwamba wewe utakuwa Sabinaa mke wa Nyani Ngabu basi bibi wa watu akacheka kinoma

Huu uzi nimeamin kuna wazee sana humu

Halafu nimefundua wengi wao ndo wale wa mashati ya mboga mboga
Usijali mkuu!
Unashangaa ya juzi 1990?
Ulizia njaa ya mwaka 1974, watu tulipokula unga wa yanga.
Au kwa raha zako ulizia maasi ya jeshi mwaka 1964.
 
Walivotoka huko DSM, wakaja Jamhuri, Morogoro
 
Sorry, swali nje ya maada hasa hapo kwenye bold. Tujaalie umri wako? Mengine yaelekea umefanya kusimuliwa au kusoma tu sehemu na waandishi hao ni wale waliokua against with this African queen, ANC walikua na pesa nyingi hivyo kweli!?


Nikuambie umri wangu ndio ujue kama nina hakika?

Kwani mbona wengi tunajua Adam aliingia nyumbani mwa Hawa, kuna mtu hapa ana umri wa kulishuhudia hilo?

Nimesema Winnie alipiga hela za chama unasema ANC ilikuwa na pesa ngapi, kwani nimesema aliiba a billion dollar?

Winnie alikutwa na hatia mahakamani, na akafukuzwa kwenye Jumuia ya chama.

Unasema vyombo vya nje vinampakazia. Dunia ilimpenda sana Mandela mfungwa, Mandela Rais, na mstaafu, vyombo vya dunia havina sababu ya kumchafua mkewe Winnie for no reason.

Tena Wazungu walimpenda sana Winnie kwa sababu alikuwa anakataa ule uke wa Kiafrika, kwenye interviews miaka ya 70 alikuwa anasema yeye sio mbeba maua kwenye kivuli cha Mandela. Kwanza alikutana na Mandela ofisini kwa Oliver Tambo, kwa hiyo yeye mwenyewe Winnie alishapagawa kwenye harakati kitambo, Mandela hamwelezi kitu maisha haya. Hizo quality za mwanamke kidume Wazungu wanapenda sana lakini ali disappoint kila mtu.

Winnie aliharibu legacy yake kwa kuanza kuteka wenzie, kuua, kula hela za chama, na kutoka na viana sheria vya chama nusu ya umri wake.
 
Mkuu kumbe na wewe ...uliingia mjini mapema. Hongera zako.

Miaka hiyo Dar Es Salaam wengine tunaisikia kwenye Radio Tanzania! (wengi wetu radio maarufu ilikuwa KBC- Mambo mbotela!)

Huyu Mungu huyu? Ni wa wote aiseee!
Leo hii unatamba tu kona za masaki
 
Asante mkuu. Nakumbuka mie nilikuwa pale mnazi mmoja kwenye zile trafic light nikiwa na uniform yangu ya Tambaza sec school by then nilikuwa form three yaani nilikuwa na hamasa kubwa sana ya kumuona huyu gwigi na mpambanaji wa ubaguzi wa Rangi barani Africa. Cha kushangaza ilikuwa ni Mara yangu ya kwannza kumuona Mwl Nyerere live. So niliua ndege watatu kwa jiwe moya hahah asante sana kiongozi

I was right there Lumumba/Uhuru Street.
 
Siku moja nilikuwa mitaa flani,

Mara bibi mmoja makadirio kama 70+ hivi nilimuona anafungua app ya JF kwa simu yake nikahamaki,

Nikajifanya kama sijui vile nikamuuliza samahani bibi unatumia application gani hiyo akanionyesha

Ilibidi tu nimtanie kwamba wewe utakuwa Sabinaa mke wa Nyani Ngabu basi bibi wa watu akacheka kinoma

Huu uzi nimeamin kuna wazee sana humu

Halafu nimegundua wengi wao ndo wale wa mashati ya mboga mboga
Mashati ya mboga mboga[emoji33] [emoji33] [emoji33]
Huyo uliemuona ni Kasinde
 
Umesema ulimuona mwaka 1990. Na wakati kipindi icho South Africa ndio moto ulikuwa umewaka na Mandela yupo Lupango. Mandela alitoka jera mwaka 1994. Aliyekusimulia iyo hadithi mwambie hakusimulie tena
Hapana mkuu Mandela alitoka mwaka 1990 mwezi Feb nafikiri lakini uhakika 1990!! Mwaka 1994 ndio alishinda uchaguzi mkuu na kuwa rais wa SA, naona umechanganya kidogo hapo. Amandla....
 
Back
Top Bottom