Winnie Madikizela Mandela alipokuja Dar 1990

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,780
Reaction score
14,873
standing-in-open-car.jpg

Kwanza nimtakie mapumziko ya amani, Winnie Madikizela Mandela, dada shupavu sana kuwahi kutokea Afrika.

Tulimsikia sana miaka ya 1960s, 70s , na 80s tukiwa mashuleni, akiongoza maandamano haya na yale huko Sauzi.

620x349

Pamoja na kipaji cha ujasiri, jamani Winnie alikuwa mzuri,mzuri, mzuri sana.
Alikuwa mzuri almost like a doll, and she was a doll!

Hivyo basi tuliposikia Mandela atakuja Dar mwaka 1990, mimi nikajiambia, ni lazima nikawatie machoni, hawa watu maarufu.

Nilijipanga pale Azania Front, na nikapata nafasi nzuri kuliona ROLLS ROYCE la Ikulu, lililowabeba Mandela , Winnie na Mwalimu, gari la wazi.
Watu walikuwa wengi, wengi,wengi.

Gari lilipopita pale Azania Front, akatokea bwana mmoja, si wa makamo yupo mbele, akapiga kelele kwa nguvu,
"TOTO HILOO LA UHAKIKA"
Watu wakacheka na kushangilia kwa nguvu, nahisi hata Mwalimu alisikia na kupungia.

Ndio mara ya kwanza na ya mwisho kumuona Mandela na Winnie.

UPDATE
Leo ndio mazishi ya Winnie, na katika hotuba yake, Rais Ramaphosa ame comment kuwa, kati ya ambavyo Winnie alijaliwa kuwa navyo ni uzuri wake wa asili.
Rais Ramaphosa amesema Winnie alikuwa mzuri, mzuri, mzri sana.
Na wanawe Winnie wameonyeshwa wakitabasamu huku watu wakishangilia.
Baadaye baada ya kuwataja wapigania uhuru waliotangulia, kwa haraka Rais Ramaphosa alionekana akifuta chozi.

RIP Winnie.
20180414_133842.jpg

Muda huu angalia SABC TV, mazishi yanendelea.
 
Hakuna aliye mkamilifu. Note even Mandela was. Ingawa sasa hivi media za magharibi zinamuonyesha kama mama aliyekuwa mkaidi, muuaji nk. Nasema, hawa wote hawana hata chembe ya uzuri waweze kumkashifu huyu mama. alisimamia utu wa mwafrika kwa nguvu zake zote. Kipindi ambacho ilikuwa ni jinai kufanya hivyo. Hivi ni wanawake wangapi wenzi wao wanaweza kukaa gerezani miaka 27 na wakabaki walivyo?? Mwenyezi Mungu ndo mlipaji na muweza wa yote.

Wanasema eti alikuwa violent. Hivi kweli kwa utawala wa Makaburu mtu angeweza kutumia njia gani kupambana nao? Apartheid itself was violent!

Naamini huyu mama angekuwa mweupe hakika vyombo vya habari vya magharibi vingetoa taswira tofauti. Nimefarijika sana kuona serikali ya Afrika Kusini imeamua kumpa heshima zote anazostahili kama mpigania uhuru na utu wa taifa lake. Mwenyezi Mungu wa rehema ampokee na kumsamahe mapungufu yake yote. Amina.

Apumzike kwa amani mama Winnie Mandela!
 
Namkubali sana huyu Mama!
Madiba alimwacha akiwa hot na miaka20+ ongeza 27yrs! Aisee no wonder she had affairs! Tena wangekuwa wengine baada ya Madiba kufungwa Maisha ndo wangezaa kabisa but she didn't!
Kuwa Violent ilikuwa lazima kwa mazingira ya ubaguzi dhidi ya weusi!
She was tough indeed!
R.I.P Winnie Mandela!
 
Anaweza kulaumiwa kwa mengi! lakini ni mama aliyevumilia mengi kwa mtazamo wangu! aliachwa na Mandela akiwa bado mbichi, Mandela akaenda jela! jamani sitetei makandokando aliyoyafanya lakin kama binadamu alihitaji faraja baada ya mapambano na makaburu. Pumzika kwa amani mwana mwema wa mama Afrika ambaye hukujua kupendwa kwa sababu uliyempenda alikuja akakusaliti kwa kumpenda Graca. aliwasamehe makaburu akashindwa kukusamehe wewe uliyeendeleza mapambano ili asisahaulike gerezani! Yote maisha🙁
 
Mkuu naikumbuka sana siku ile alipokuja Marehemu Mandela na mke wake. Ilikuwa ni siku ya mvua, enzi hizo tukiwa wanafunzi wa sekondari, tuliruhusiwa kutoka mapema ili tumuone huyo gwiji wa Afrika ya kusini.

Mimi nilisimama pale pembeni ya wizara ya elimu, msafara ulikata kona pale wizara ya ardhi. Tuliwashangilia sana RIP Mandela na RIP Nyerere.

Mwaka huo huo 1990 akaja nchini RIP Papa John Paul, ilikuwa mwezi wa tisa, ibada ikafanyika pale jangwani.
 
View attachment 733998
Kwanza nimtakie mapumziko ya amani, Winnie Madikizela Mandela, dada shupavu sana kuwahi kutokea Afrika.

Tulimsikia sana miaka ya 1960s, 70s , na 80s tukiwa mashuleni, akiongoza maandamano haya na yale huko Sauzi.

620x349

Pamoja na kipaji cha ujasiri, jamani Winnie alikuwa mzuri,mzuri, mzuri sana.
Alikuwa mzuri almost like a doll, and she was a doll!

Hivyo basi tuliposikia Mandela atakuja Dar mwaka 1990, mimi nikajiambia, ni lazima nikawatie machoni, hawa watu maarufu.

Nilijipanga pale Azania Front, na nikapata nafasi nzuri kuliona ROLLS ROYCE la Ikulu, lililowabeba Mandela , Winnie na Mwalimu, gari la wazi.
Watu walikuwa wengi, wengi,wengi.

Gari lilipopita pale Azania Front, akatokea bwana mmoja, si wa makamo yupo mbele, akapiga kelele kwa nguvu,
"TOTO HILOO LA UHAKIKA"
Watu wakacheka na kushangilia kwa nguvu, nahisi hata Mwalimu alisikia na kupungia.

Ndio mara ya kwanza na ya mwisho kumuona Mandela na Winnie.
Hivi ccm ilishatuma hata salamu za rambirambi ?
 
Mkuu naikumbuka sana siku ile alipokuja Marehemu Mandela na mke wake. Ilikuwa ni siku ya mvua, enzi hizo tukiwa wanafunzi wa sekondari, tuliruhusiwa kutoka mapema ili tumuone huyo gwiji wa Afrika ya kusini.

Mimi nilisimama pale pembeni ya wizara ya elimu, msafara ulikata kona pale wizara ya ardhi. Tuliwashangilia sana RIP Mandela na RIP Nyerere.

Mwaka huo huo 1990 akaja nchini RIP Papa John Paul, ilikuwa mwezi wa tisa, ibada ikafanyika pale jangwani.

Mkuu kumbe na wewe ...uliingia mjini mapema. Hongera zako.

Miaka hiyo Dar Es Salaam wengine tunaisikia kwenye Radio Tanzania! (wengi wetu radio maarufu ilikuwa KBC- Mambo mbotela!)

Huyu Mungu huyu? Ni wa wote aiseee!
 
Nimekuja Dar mwaka 1978, miaka 40 iliyopita. Nimekulia mitaa ya Gymkhana, nimecheza ndani ya viwanja vya ikulu.
 
Anaweza kulaumiwa kwa mengi! lakini ni mama aliyevumilia mengi kwa mtazamo wangu! aliachwa na Mandela akiwa bado mbichi, Mandela akaenda jela! jamani sitetei makandokando aliyoyafanya lakin kama binadamu alihitaji faraja baada ya mapambano na makaburu. Pumzika kwa amani mwana mwema wa mama Afrika ambaye hukujua kupendwa kwa sababu uliyempenda alikuja akakusaliti kwa kumpenda Graca. aliwasamehe makaburu akashindwa kukusamehe wewe uliyeendeleza mapambano ili asisahaulike gerezani! Yote maisha🙁
Well said...
Kuna Tuhuma za barua aliyomwandikia Dali Mpofu (aliyekuwa kijana mwanasheria wa ANC wakati huo na inaaminika alikuwa na affair naye japo haijathibitika)
Kama kweli ile barua ni ya "Mama Winnie" kwa Mpofu inaonekana aliumizwa sana na kukosa mtu wa kumfariji na huwezi kumlaumu moja kwa moja kwa aliyofanya!
 
Back
Top Bottom