Winnie Madikizela Mandela alipokuja Dar 1990

Winnie Madikizela Mandela alipokuja Dar 1990

Mkuu, mbona unataka kuchekesha watu humu ndani. Mandela alitoka jela mwezi february mwaka 1990, akaja nchini mwetu katika kipindi hicho hicho. Akapokelewa na Mwalimu Nyerere, kama sijakosea mzee Mwinyi ambaye ndiye alikuwa ni rais, hakuwepo nchini.

Mwaka 1994 ndipo alipoanza urais wake. Wewe ni mtoto mdogo usiyejua chochote, sasa ni bora kabla hujaleta dharau, ukatafuta kueleweshwa na waliokuzidi umri kabla hujaandika kitu mbele ya jamii.
[emoji2] [emoji3] [emoji1] Tatizo vijana wanaovaa milegezo hawajui historia mkuu wao wanarukia makala tuu sawa na kurukia train kwa mbele nimecheka sana
 
Wengi wenu mnashindwa ku appreciate mentality ya freedom fighter akiwa war front.
Winnie alitendewa unyama naye ilibidi awe mnyama kusurvive hadi miaka 81.

Wengi sana wenzake walipotea kitambo.
Fuatilia hata Maisha ya mke wa kwanza wa Samora Machel, Josina Machel.
Alikufa mchanga kabisa wakati wa kupigania uhuru.
RIP Winnie, you survived agaist all odds.
She was a freedom fighter i give her props for that.
But she was so flawed as a person and that will always tarnish her history.
 
20180414_133842.jpg

Rip Winnie.
 
Anaweza kulaumiwa kwa mengi! lakini ni mama aliyevumilia mengi kwa mtazamo wangu! aliachwa na Mandela akiwa bado mbichi, Mandela akaenda jela! jamani sitetei makandokando aliyoyafanya lakin kama binadamu alihitaji faraja baada ya mapambano na makaburu. Pumzika kwa amani mwana mwema wa mama Afrika ambaye hukujua kupendwa kwa sababu uliyempenda alikuja akakusaliti kwa kumpenda Graca. aliwasamehe makaburu akashindwa kukusamehe wewe uliyeendeleza mapambano ili asisahaulike gerezani! Yote maisha🙁
Alikua na uwezo wa kwenda gerezani kwa Mzee na akakaa nae faragha hata kwa siku tano au wiki. Huyo mama ilikuwa na ulevi tu wa kutoa papa. Still hata baada ya mume wake kutoka gerezani bado akawa na makandokando. Unakumbuka alitumbuliwa uwaziri akiwa wapi na nan? Soma historia utajua. Kwangu mie huyo mama ni mpuuzi tu hana lolote.
 
View attachment 733998
Kwanza nimtakie mapumziko ya amani, Winnie Madikizela Mandela, dada shupavu sana kuwahi kutokea Afrika.

Tulimsikia sana miaka ya 1960s, 70s , na 80s tukiwa mashuleni, akiongoza maandamano haya na yale huko Sauzi.

620x349


Pamoja na kipaji cha ujasiri, jamani Winnie alikuwa mzuri,mzuri, mzuri sana.
Alikuwa mzuri almost like a doll, and she was a doll!

Hivyo basi tuliposikia Mandela atakuja Dar mwaka 1990, mimi nikajiambia, ni lazima nikawatie machoni, hawa watu maarufu.

Nilijipanga pale Azania Front, na nikapata nafasi nzuri kuliona ROLLS ROYCE la Ikulu, lililowabeba Mandela , Winnie na Mwalimu, gari la wazi.
Watu walikuwa wengi, wengi,wengi.

Gari lilipopita pale Azania Front, akatokea bwana mmoja, si wa makamo yupo mbele, akapiga kelele kwa nguvu,
"TOTO HILOO LA UHAKIKA"
Watu wakacheka na kushangilia kwa nguvu, nahisi hata Mwalimu alisikia na kupungia.

Ndio mara ya kwanza na ya mwisho kumuona Mandela na Winnie.

UPDATE
Leo ndio mazishi ya Winnie, na katika hotuba yake, Rais Ramaphosa ame comment kuwa, kati ya ambavyo Winnie alijaliwa kuwa navyo ni uzuri wake wa asili.
Rais Ramaphosa amesema Winnie alikuwa mzuri, mzuri, mzri sana.
Na wanawe Winnie wameonyeshwa wakitabasamu huku watu wakishangilia.
Baadaye kwa haraka Rsis alionekana akifuta chizi.

RIP Winnie.
View attachment 744340
Muda huu angalia SABC TV, mazishi yanendelea.(saa 9.15 mchana)
 
Mtupe na scandal zake za kupenda "thresome"


Ni miongoni mwa sababu kwanini mzee wa watu alikufa bila kumsamehe
 
Wewe utakuwa umetoka kule kwetu ziwani. RTD ilikuwa haipatikani vizuri. Mambo Mbotela - Je, huu ni uungwana? Wakongwe tuko wengi ati.
Na tangazo la mafuta ya kimbo, royco michuzi mix na sabuni ya jamaa...muda wa taarifa ya habari walikuwa na kawimba kao kalifuata baada ya sauti nene ya hii ni KBC, Nairobi....
 
TOTO HILOO LA UHAKIKA safi sanaaaaaaaaaaaaaaah
Jamaninkwa uhakika Winnie alikuwa mzuri sana.
Hata Rsis Ramaphosa kashuhufia leo, kwamba kulikuwa na balizi wa nchi fulani alikaribishwa kumsalimia Winnie.
Katika kupeana mikono, bslizi hakuuachia mkono a Winnie mpaka akakumbushwa na wapambe,
"mheshimiwa kuna wengine m
Wanasubiri kumpa Winnie mkono".
Uzuri wa Winnie ulimtia kiwewe.
 
Kuna hi misemo ya kisasa, mmoja unasema hivi, "kuna na mke mzuri sana ni sawa na kua na shamba la maembe karibu na shule" Hope hi ndio iliosababisha usimwone Winnie wakiwa na mzee Madiba
Sio kweli kifungo cha miaka 27 ndo kilikua doa ktk ndoa yao
 
Udhaifu kama binadam sote tunao!
Tuwe wakweli Winnie alipambana sana...alipigania kijasiri mumewe aachiwe huru pia...
Uzinifu na makando kando mengine hata..kwao huyo anayemsema vibaya pia hapo!
Anastahiki kuenziwa....
Kwa life la wakati ule SA...wote waliishi kama mashetani!
 
Aliwahi kuwapa papa baadhi ya watu wakati Mandela ananyea debe nyuma ya nondo
Iliyouma zaidi ni pale Mandela alipotoka jela huyu mama alitaka kusafiri kwenda Uingereza na basha wake. Mandela akakataa. Mama akaenda alipopiga simu ikapokelewa na basha. Swali najiuliza hivi President kabisa mke anasafiri nje ya nchi bila usalama wako kujua au wewe mwenyewe kuambatana nae? Anyway ilikuwa life style tofauti. Hivi mke wa Rais kirahisi rahisi tu
 
Back
Top Bottom