Je, kulikuwa na ulazima gani Tanzania kuchukua wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wimbo wa Taifa? Kwanini tusingetunga wa kwetu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,335
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Suala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je, kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
 
Enock Sontonga, raia wa Afrika Kusini, aliyetunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ iAfrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905.

Sauti ya wimbo huo imetumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini zimetunga nyimbo nyingine.

Check hapa pia.

Thread 'Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake' Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Swala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
Tazama ramani mrefu kinoma, ni kheri tuache hivyo hivyo maana hizo kamati sijui wanakway wa kutunga, kuhariri na kupata wimbo wa taifa watakula pesa zaidi ya pesa ya sensa. Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume waambie waache tu hasara ni kubwa kuliko faida.
 
Kabisaa kakaa
Maana vipindi vingine tunavitunga wenyewe afu kibunda wanakinyoosha wao wenyewe.

Waambie huu wimbo tunaupenda na hatuna mpango na nyimbo ingine.

Maana utakuja kuskia Melodi bilion moja kutoka Canada na Gita milion miatisa kutoka uturuki.
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Swala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
FB_IMG_1665001786724.jpg
 
Hata jina Tanzania likitungwa na mhindi, akaweka hadi jina lake na jina la jumuiya yake ya Ahmadiya
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Swala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
Tuna mengi ya msingi ya kushughulika nayo zaidi ya wimbo wa taifa.
 
Nakumbuka kuna siku watu wa South Africa walikuwa kwenye campus ya Mazimbu SUA ili kitembelea makaburi ya wapendwa wao, utaratibu ambao huwa wanaufanya kila mwaka.

Hapo nilipata mafasi ya kufahamu Historia ya uhusiano kati ya South Africa na Tanzania. Wakati wa harakati za kupambania uhuru wanajeshi wa South wa SA walipata hifadhi Tanzania sababu nchini kwao ilikuwa ngumu sana kufanya maandalizi ya kijeshi.

Hayati Nyerere na Hayari Mandela walielewana sana na walishirikiana kwenye juhudi za kumpinga mkoloni. Ndio maana hata nyakati flani Nyerere alipewa nafasi ya kuhutubu kwenye bunge la South Africa.

Hii ilisababisha ma-baba hawa wa taifa kuwa na vitu vingi vinavyofanana sababu walikuwa bega lwa bega nyakati zote hizo, nenda Mazimbu morogoro ma-comrade wengi wa Afrika Kusini wamepewa hifadhi pale.

SIO WIMBO TU, HATA RANGI ZA BENDERA ZA MATAIFA HAYA MAWILI ZIMEFANANA.
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Swala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
Nyakati, mkuu 'Buji', nyakati ndizo zimebadilika.

Wakati ule , moto ulikuwa wa 'PanAfricanism'.

Pengine leo hii ungeambiwa kwamba Tanzania itatumia raslimali zake adimu, na kujitoa mhanga, na kwa kweli kujiweka katika hali hatarishi kama tulivyowahi kujiweka nyalkati hizo katika ushiriki wetu wa ukombozi wa nchi kusini mwa bara hili, jambo hilo leo hii lingeonekana kama la kipuuzi.

Ni katika hali hiyo hiyo, katika mawazo ya nyakati zile, haikuonekana kuwa jambo la ajabu kutumia wimbo huo.
 
Nyakati, mkuu 'Buji', nyakati nzo zimebadilika.
Wakati huo, moto ulikuwa wa 'PanAfricanism'.

Pengine leo hii ungeambiwa kwamba Tanzania itatumia raslimali zake adimu, na kujitoa mhanga, na kwa kweli kujiweka katika hali hatarishi kama tulivyowahi kujiweka nyalkati hizo katika ushiriki wetu wa ukombozi wa nchi kusini mwa bara hili, jambo hilo leo hii lingeonekana kama la kipuuzi.

Ni katika hali hiyo hiyo, katika mawazo ya nyakati zile, haikuonekana kuwa jambo la ajabu kutumia wimbo huo.
Nimeridhishwa pakubwa na jawabu lako. Asante sana
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom