magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,201
- 3,322
Amani kwenu Members wote.
Wimbo wetu wa taifa wakati unatungwa ulizingatia zaidi masilahi ya kisiasa hasa kutokana na Msaada wetu Kwa nchi zingine ambazo zilikuwa hazijapata uhuru.
Ile sehemu tunayoimba Mungu ibariki Africa, tulizingatia zaidi kuimarisha uhusiano wetu na mataifa mengine. Na Kwa wakati ule hatukuwaza umuhimu wa matumizi mengine Kwa wimbo huo.
Kwa sasa wimbo wetu unatumika kwenye michezo, siasa nk. Kwa maoni yangu sioni kabisaa haja ya kuendelea kuacha hicho kipande cha kuibariki Africa. Mfano Jana wakati tunacheza na Morocco, tuliomba Mungu ibariki Tanzania, Lkn hapohapo tukaomba aibariki na Africa(akiwemo Morocco). Sasa Hayo maombi gani!? Yaani unaomba baraka Mungu akubariki ushinde halafu hapohapo unamuombea baraka mpinzani wako!?
Kimsingi maombi ya kuombewa na mtu mwingine yana nguvu zaidi kuliko ukijiombea mwenyewe, Ndo Maana watu wanaenda kuombewa makanisani na misikitini.. Tuache kuwaombea baraka tunaoshindana nao, wataomba wenyewe halafu Mungu Ndo ataamua kuliko sisi kuonekana tupo tayari kuwatakia baraka washindani wetu.
Najua wazee wa system wamejaa hapa jukwaani wamshauri rais tuondoe Hayo maneno ya kuwatakia baraka wenzetu. Maana hata kwenye uhalisia hatuelewani na kila nchi iliyopo Africa, sasa Kwa nn tunawabariki!?
Nawasilisha.