Wimbo wa miaka 50 ya UHURU.Umeonyesha ujinga wa wasanii wa BONGO.

Baba Matatizo

JF-Expert Member
May 5, 2011
334
64
Nimehuzunika sana kuona wasanii wa bongo fleva wakiimba wimbo huo ambao hauna maana kwa MTANZANIA WA HALI YA CHINI.JE wasanii wetu wametumia akili kusifia miaka 50 ya uhuru kwa kusema eti tuna amani,sijui nini nini....

Wameisifia SERIKALI wakati hakuna lolote.....Kweli wasanii wa bongo fleva ni MAJUHA KABISA. Waje huku kijijini kwangu waone jinsi tunavyo lala na njaa ndani ya miaka 50 ya uhuru.Kifupi waneniudhi sana.
 
Diih nakuunga hoja mjomba,ile pale dhik zao 2 pale ndo zimewachoresha vle,WAMECHEKESHA SANA
 
Ni wimbo upi? ila nakumbuka kuna ka-wimbo fulani kameimbwa pale UWANJA WA TAIFA... ndo hako???
<br />
<br />
Kuna baadhi ya vipande vya video wamerekodia uwanja wa taifa.kwa kweli WAMENIUDHI SANAAAA.DHIKI ZINAWAPONZA.Kesho TAZAMA TBC Utawaona bila wasi.
 
JF ni kuponda 2??! Hamna chembe cha zuri hata moja?? Duh! Sio kihivyo bwana.
 
Sasa wasifu nini? Hivi leo unajisifu miaka 50 ya uhuru, tuna wizara ya ardhi, wamepima asilimia moja tu nchi? Majirani zetu kama kenya umeme ukikatika, watumiaji wanahaki wa kuwashitaki kwa hasara watakayopata
 
JF ni kuponda 2??! Hamna chembe cha zuri hata moja?? Duh! Sio kihivyo bwana.

Sio kuponda, umeuona Wimbo wenyewe lakini? maudhui yake yanatuambia tujivunie kitu ambacho hatuna, inawezekana kweli hii?
 
Amlipaye mpiga zumari ndiye achaguaaye wimbo...ulitegemea waimbe nn kama wametumwa na ka'governement'??
 
mwenye mp3 ya huo wimbo naomba auweke jamvini maana wengi tuko mbali kidogo na tv..
 
mtu kama sugu hawez shiriki katika unafiki wa kuwatukana wakulima na wafanya kazi kiasi kile.

Wasanii wengi wanapenda waonekane katika runinga na si vinginevo ili waonekane hawajachuja kitu ambacho si kweli.

Wamesifia but effect yake ni kubwa kwa jamii.
 
Njaa tu wale ila hatujajua alie waorganise akagharamia vitu vyote alitaka wimbo uwe katika maudhui gani. Mie nahisi ni serikali ndo imewagharamia ili waisifu.
 
Hako ka-song nilikacheki once na sikukapenda hata kidogo.sijui ni amani gani wanaiongelea,hakuwezi kuwa na amani hapa mwanza when siku 3 sasa jiji zima halina umeme.3 gud f****ng days!
 
Kuna kitu ambacho inabidi ukielewe baba matatizo ile ni idea ya mtu au kikundi cha watu kilichoamua kuangalia upande mmoja wa hatua zilizopigwa tangu tupate uhuru hata kama ni hatua moja wao waliona inastahili pongezi sasa sijui wasanii waliokabidhiwa mashairi tu na kuimba wanahusika vipi na malalamiko yako!

Mbona wao binafsi wapo wengi tu wanaoilemisha jamii kwa kuikosoa serekali tena kwa maneno makali!au ulitaka wagome wasikubali kuimba eti kwa sababu idea ni mbaya? Tuache siasa kwa mambo yasiyohitaji siasa na kaa ukijua ile ni buruduni tu iliyoandaliwa kuipongeza miaka hamsini ya uhuru yapo mazuri yaliyofanyika kubali au kataa na wao ndio waliyoyalenga na sio lazima kukosoana kila mara hata katika birthday ya kihistoria kama hiyo!
 
unategemea wangekashifu serikali?
Nimehuzunika sana kuona wasanii wa bongo fleva wakiimba wimbo huo ambao hauna maana kwa MTANZANIA WA HALI YA CHINI.JE wasanii wetu wametumia akili kusifia miaka 50 ya uhuru kwa kusema eti tuna amani,sijui nini nini....Wameisifia SERIKALI wakati hakuna lolote.....Kweli wasanii wa bongo fleva ni MAJUHA KABISA.Waje huku kijijini kwangu waone jinsi tunavyo lala na njaa ndani ya miaka 50 ya uhuru.Kifupi waneniudhi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom