georgemwaipungu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 2,779
- 589
Nyie watu bana, huenda ikawa hii ni dhambi ya CCM kuwapa elimu isiyowasaidia. Mnakuwa ni watu wa kuropoka hovyo na kuelekea kule wakubwa zenu wanawaamrisha!!!
Asubuhi napitia comment nyingi baada ya taarifa kuwa Slaa atakuwa Azam tv, watu mnaonesha kutopenda hicho kitendo na kudai mnapuuza hicho kitendo na hamtakiangalia kwa sababu mnajua ni CCM ndio wamelipia kipindi.
Sasa hivi mmepata taarifa za kipindi kutorushwa mnaonesha mlikisubiri kwa hamu maana mlijua Slaa angekabwa maswali na Tido!!
Hii akili huipati popote isipokuwa kwa watu wanaojidanganya wanaweza kuchambua vitu, bila kufahamu kuwa hawawezi na hawatoi nafasi ya kuoneshwa kuwa hawawezi.
Kipindi ni recorded na kuna watu walileta taarifa ya kuona vipande vya hayo mahojiano vilivuja, sasa kutorushwa kwake inatakiwa tuwaulize Azam ni nani anahusika, je ni CCM wameona yana Athari kwao ama UKAWA kuna point zimekuwa nzito kwao ama AZAM wameona mahojiano yamekiuka maadili?!!
Tulia wewe mbona unatetemeka na kukosa mwelekeo?