Willibrod Slaa amkacha Tido Mhando

Willibrod Slaa amkacha Tido Mhando

Status
Not open for further replies.
Acha zako, na alivokuwa TBC alikuwa team gani ?

Wamebanwa hao sasa wanatapatapa watasingizia kila mtu huyo anayeropoka ni mfuasi wa membe ambaye ndiye anafadhili hizo fujo zote za Slaa.
 
Nilikataa aina ya uongozi wa Lowassa kabla hata ya Richmond; Richmond ilithibitisha tu kile ambacho nilikuwa tayari nimekiona kwake kama kiongozi; udhaifu uliopitiliza wa kiongozi; yaani viongozi wenye kutumia nguvu za vyeo kuliko ushawishi wao wenyewe. Na hata alipojiuzulu katika kashfa bado nilizidi kuamini kuwa labda angetumia ule muda kujijenga kama kiongozi; badala yake miaka karibu nane ya kuwa mbunge hakuleta hoja yoyote rasmi (zaidi ya hotuba za kuonesha yupo), hakuleta mswada wowote wa kujaribu kutatua matatizo, hakuwahi kufanya lolote la kusahihisha madudu akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (kabla na baada ya kubadilishwa muundo wa kamati).
Nani anakumbuka uenyekiti wa Lowassa kulinganisha na Uenyekiti wa Zitto kwenye Kamati ya Bunge? Ni kitu gani Lowassa alikisimamia katika kuhakikisha vyombo vya usalama vinatenda haki? Ilipotokea Opresheni Tokomeza na ile nyingine Lowassa alisema nini cha kuonesha ni kiongozi kweli kweli anayejali haki za raia na za binadamu? Ni lini Lowassa alilaani matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya Rais wasio na silaha wenye kuandamana tu?
Na hapa wala hatujagusa suala la ufisadi! Kote huko Lowassa alikuwa na ndoto moja tu; mipango yake yote ilikuwa inaelekea kwenye lengo hilo la ndoto - kuwa mgombea wa Urais. Haikujalisha iwe chama gani, alikuwa ameamua kugombea urais liwalo na liwe. Ndoto hii sasa imetimia.
Lakini mimi bado ninamkataa kwani hata ssa naona aina ile ile ya uongozi wake; aina ya uongozi ambao unasumbua sana nchi zetu hizi. Si mtu wa kufuata sheria wala kuheshimu taratibu; anaamini (kwa vitendo vyake) kuwa yeye ni Taasisi. Kiasi kwamba hata CDM wamekubali kuwa yeye ni taasisi - siyo tena CHADEMA-MABADILIKO bali NI "LOWASSA-MABADILIKO"; yaani, Bila Lowassa CDM isingeweza na haiwezi kuleta mabadiliko!
Nimeendelea kumkataa na sijaona sababu hasa ya kwanini niamini ataongoza mabadiliko wakati rekodi yake yote kama mwanasiasa na mtumishi wa serikali hakuna hata moja linaloonesha kuwa yeye ni mtu wa mabadiliko! NONE.
Kwa hiyo sisi wengine tumeendelea kumkataa, na kukataa aina ya uongozi wake. Tulipomkataa akiwa CCM hatukuambiwa tunatu miwa CDM au na yeyote yule, tulipomkataa na hadithi zake za Kasungura hatukuambiwa tunatumiwa na yeyote. Lakini leo kuendelea kumkataa akiwa amehamia upinzani tunaambiwa tunatumika. Tungeuwa tunatumika kama tungekuwa tumebadili msimamo wetu kwa ajili ya manufaa ya kisiasa ya aina fulani (kwetu au kwa wenzetu). Hatujabadilika.
Waliobadilika wapo, wanajijua na wanajulikana. Lakini hawa hawatumiki! Wamebadili kutoka kuita ukweli uongo, giza nuru na uadilifu ufisadi na sasa wanaimba wimbo tofauti kabisa lakini watu hawaoni tatizo - well, wamesema "mabadiliko"! Kwamba kubadilika kutoka vitu ulivyoamini kwenda vitu vingine kabisa kinyume na vile vya awali ndio "mabadiliko yenyewe". Kwamba, kuwa tayari kuchagua jiwe kuliko kumkataa Lowassa ndio kubadilika kwenyewe, kwamba kuwa tayari kuacha yote uliyosimamia ili umkubali usiyewahi kumsimamia au ambaye hakuwahi kusimama nawe ndio mabadiliko!
Kweli Lowassa - Mabadiliko na Mabadiliko - Lowassa. Lowassa ameweza kubadilisha wengi na wanajijua amewabadilisha. Tatizo ni kuwa yeye hajabadilika! Ndoto yake ni ile ile, maono yake ni yale yale, na lengo lake ni lile lile. Unaweza kubadili mbinu, unaweza kubadili mikakati na hata kubadili watu; lakini ukibadili kanuni basi huna tena cha kusimamia.
Mimi sijabadilika
Lowassa hajabadilika
Nani amebadilika?
Unamjua, unawajua.
Umebadilika?
 
Hivi wewe umemeza sabuni gani? povu lote hili kisa lowassa tu?hata kama hajabadilika sisi hatuitaki ccm
 
tehe...tehe...tehe...!kastaafu siasa vibaya aisee...!anaropoka hvyo mpaka watumishi wa mungu anawachafua unadhani atapona.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom