Mimi nimesoma hicho kitabu, na nimekuwa nikisoma hata makala zake alizokuwa akiliandikia gazeti la Rai. Kwa kweli hoja alizotoa katika kitabu hicho ni nzito, tena nzito sana. Pia hicho kipindi cha Channel Ten nilikiangalia, nikatamani kitudiwe. Hata Makwaia aliyekuwa akimhoji Shao alipigwa na bumbuwazi kwa data alizokuwa akimwaga, na yule daktari wa UDSM Doctor Lwaitama naye alikaa kimya akimsikiliza. Pembeni yake alikuweko mwandishi wa siku nyingi anayeitwa Tagalile. Aliyoyasema katika Channel ten mbona madogo? Uianza kusoma kitabu hicho hutakiweka chini. Hata mimi namkubali, tena namkubali sana.