William Malecela: Dissaster waiting to happen

William Malecela: Dissaster waiting to happen

Huyu ndiye mbunge mtarajiwa anayeenda kutuwakilisha Watanzania EAC. Hataki kusikia chochote kutoka kwa watu anaoenda kuwawakilisha sababu anadai hao watu wana chuki binafsi na wivu. Ama kweli ukipanda kokoto usitarajie kuvuna mahindi.
And he is coming from familia bora..... Can yo imagine.?
 
- Wala huwezi kunichafua wakari sijachafuka, mimi sio mchumi isipokuwa by professional ni Politician na ni Marine Engineer, kama ni ubaharia nimeufanya kwa level ya Assistant Engineeer,

HOWEVER: Siamini kwamba takwimu za EAC kwamba GDNP per capiter ya EAC inaweza kuwa $ 588, ndio maana ninasema tunahitaji kuwa makini sana na kuelekea kwenye one Currency kwa sababu kama tunaenda na this kind of takwimu kama the guidance then tutaumia tu!

William.

Classic
 
sasa kweli ukiwa mbunge simu si zitakuwa zimefungwa 24/7

kaka naomba utuweke wazi juu ya points hizo 8 zilizobaki tafadhali

yaani mpaka haya nayo tubembeleze?
 
Jamani ndiyo maana ID mbili za JF siziwezi. Unaandika lugha ile ile, unacheka vile vile, emotional vile vile...
 
william kuwa mkweli usaidiwe,ubunge huu umekuja baada ya neema kukataa kukusainia makaratasi ya kuendelea kuishi marikani? unataka kuwafanya watanzania wote hawana akili?
:yell::yell:
 
Ningekuwa mimi ndiye William ningekubali kukosolewa na hata kufundishwa nini cha kwenda kuwakilisha huko EAC maana najua hapa JF ningepikwa na kutoka nikiwa so smart. Kwenye Tanuru la Fikra- Facebook aliulizwa umekaa Marekani miaka 30 leo umerudi na kuutaka Ubunge tena wa EAC, Je unajua ama unaziweza panda shuka za siasa za Tanganyika ? Hajajibu mpaka leo.
 
huyu ni wale wale tu, wakina Nape, DR Mwinyi, Nchimbi wote ni watoto wa elite group wao kila kitu ni tambarare tu....Jumuia ya Afrika mashariki ili anza kuzungumzwa siku nyingi sana. katika pita pita yangu ya historia gavana wa Tanganyika katika ripoti yake ya mwaka 1937 kuhusu shirikisho aliandika kuwa Watanganyika hawako tayari kuungana na wakenya na waganda kwani wako nyuma mno kiuchumi na kielimu....Leo miaka 75 zaidi bado tunaimba taralila zile zile tu. We should draw a line somewhere and fight within....
 
mimi bado naendelea na hili mpaka nijibiwe maswali yangu yaliyobaki
 
william nakuomba kaka uje

sisi wote ni vijana na nchi inatutegemea
 
Kama amesema hayo namuunga mkono. Binafsi siungi mkono Tanzania kujiunga na EAC kwani tutapoteza vingi kuliko tutakavyofanikiwa. Go Malecela nakuunga mkono tunahitaji mtu mzalendo usije kubadilika tu ukifika huko.
 
Hilo nalo ni neno na wazo zuri saaana kwa kijana wa leo anatoka nje kutaka madaraka. Good comment!!
 
Huyu William nilikutana naye New York. He is a nice fellow;calm,sober,serious,quite unlike his father. I wish him luck katika huu uchaguzi.
 
316444_2385989848381_1209820481_32959751_2885080_n.jpg

Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia

Hoja zake kubwa ni hizi:

1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.

2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .

3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.

4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:

a) Kwa nini iliondolewa in the first place

b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana

c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service

d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake

5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?

6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.

7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?

Je william anajua:

a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!

b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo

c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?

d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.

8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?

9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.

10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.

In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.

William kama mawazo yako ni hayo then I give up!

Hapo red ni Tandahimba mkuu siyo tendahimba! Umechanganua vizuri sana. Huyu Malecela nadhani haijui Tanzania.
 
wengi wenu mnashutumu EA Federation tu. Mengine mleta mada yupo pouwa saaana.

Kaka Willy JIPANGE upya
 
Kama amesema hayo namuunga mkono. Binafsi siungi mkono Tanzania kujiunga na EAC kwani tutapoteza vingi kuliko tutakavyofanikiwa. Go Malecela nakuunga mkono tunahitaji mtu mzalendo usije kubadilika tu ukifika huko.

Mdondoaji,

Nadhani si sahihi kusema kujiunga na EAC TZ itapoteza. Ni uoga tu ambao waTz tumeujenga, na uoga ni kitu kibaya sana. Ni vizuri tutiwe changamoto. Tukiachwa miaka hamsini ijayo tutaendelea kuwa hivi hivi na huenda hali hata ikawa mbaya zaidi. Mataifa dhaifu sana ya ulaya kuliko Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na kadhalika yamefanya juu chini kujiunga na Umoja wa Ulaya na yanafaidika zaidi. Kama waTz tunajihisi kuwa dhaifu kujiunga na EAC kutatutoa kwenye udhaifu dhoofu bin hali. ''The only thing we have to fear is fear itself'' alisema rais Franklin Delano Roosevelt wa marekani. Wakenya, waganda, warundi na wanyarwanda wanaiheshimu Tanzania. Tanzania ina landlock Malawi, Zambia, DRC, Rwanda, Burundi na Uganda hii ni opportunity ya pekee sana.

Bandari ya Dar inaweza (kama ikiongozwa vizuri) ku generate income sawa sawa na GDP ya nchi nzima kwa sasa. Tanzania ina vivutio vya utalii bora kuliko nchi yoyote nyingine ya Afrika. Tuna dhahabu nadhani sasa ni nchi ya tatu kwa kuzalisha dhahabu kwa wingi baada ya Afrika Kusini na Ghana. Mgodi wa dhahabu wa Geita nadhani ulisherehekea (kama sikosei 2004/5) kutimiza tani 40 ya dhahabu huu ni mzigo wa semi trailer ya tani 40. Tuna ardhi ambayo asilimia 100 ni arable (yaani inalimika), na Tanzania inaweza kulima mazao ya aina nyingi kuliko nchi nyingi za Afrika. Tuna mito na maziwa ya maji baridi mingi ya kutosha kulima kwa kumwagilia na kulisha nchi na ziada kubwa kuuza nchi za nje (sasa hivi kuna upungufu wa chakula duniani labda hii ndiyo nafasi). Tuna idadi ya watu zaidi ya milioni 40 wengi wao wakiwa ni vijana ambao wana afya tele na nguvu ya kufanyia kazi, pia hawa watu ni soko la bidhaa (kama tungeliweza kutengeneza za kwetu za kutosha). Tuna madini ya chuma (Liganga), Nickel (kule Kabanga kwa wakwe zangu), tuna madini ya Uraninium (yanayotengeza mabomu ya nyukilia au kama tukitaka kuzalisha nishati), Tuna maji ya ardhini ambayo ni mengi kuliko yaliyo juu mita kadhaa tu kwenda chini. Tuna wanawake na wanaume wazuri (wanaopendana na kuendelea kuzaa), tuna mifugo mingi (kuna wakati Ng'ombe walikuwa sawasawa na idadi ya watu).

Mungu ameipa Tanzania kila kitu isipokuwa kitu kimoja tu UONGOZI. Lakini swali kwetu sote, nani anaweka uongozi madarakani? Si ni thithi wenyewe? Wakati umefika waTanzania tuamue kwamba hatima ya nchi hii haiko CCM, CHADEMA, CUF, DP, siju chama cha Cheyo ni nini,...UDP, cha Mrema? oh TLP na kadhalika. Hatima ya nchi iko mikononi mwetu. Kama wananchi watendelea kuuza shahada za kupigia kura, kuhongwa shs 1000 na wagombea, kutukanwa matusi halafu tunashangilia, kutokupiga kura, mabadiliko hayatatokea na tutaendelea kuogopa vinchi vidogo vidogo bila sababu za msingi. Tukumbuke watanzania mficha uchi hazai, tuendelee kuficha uchi wetu kama wanavyo suggest kina Malechela tuone tutafika wapi.

Tunawaogopa wakenya kwa nini? Zaidi ya nusu ya nchi yao ni jangwa. Tunaweza kuwalisha hawa, na mtu akikulisha utamheshimu tu. Wacha watengeneze Colgate tupigie mswaki, wacha wazungumze kiingereza kizuri na sie tujifunze kwao wao watajifunza kiswahili. Wala hili halinitii wasiwasi, tukiwa na shirikisho mfumo wa elimu utakuwa mmoja. Wanyarwanda, warundi na waganda wao bado wana matatizo makubwa tu ni opportunity kwetu. Tuache ubabaishaji.
 
EAC haikwepeki, inamkono wa waendesha dunia. Hivyo suala ni kujipanga na kuondoa sheria na sera mbovumbovu za kijima ili iwe rahisi kwa sisi kwenda kupeleka bidhaa kenya, uganda na sudan ya kusini.

It is possible if Tanzania as country decides to go own-financial dependence. This is the only hope if majority wishes to stay out of the East African Federation. We should not politicize economic necessities with illusions. If politicians aren't serious and focused we better go now otherwise it will be disastrous!

My take: It doesn't make sense to decide not to act while we are doing none!

????
what will happen when our incumbent/any other TZ politician is promised to be a first federal leader? Will the system support or abstain from federation?
 
Huyu William nilikutana naye New York. He is a nice fellow;calm,sober,serious,quite unlike his father. I wish him luck katika huu uchaguzi.

Hahaha,

Ganesh acha vituko, eti "quite unlike his father".

William ana character flaws beyond the pale.

Eti anakwambia hiyo picha siyo alivyo kweli, "alivishwa" tu na producers wa reality TV show.

Well, guess what? Ukishakubali kuvishwa umekubali, huwezi kulaumu producers wa TV show.

Kesho atatuambia "ule mlungula niliokula sio mimi kikweli, niliambiwa na wakubwa tu kukubali". Kauli kama hizi zinamuonyesha hana character wala intelligence ya kutaka kuwakilisha watu.

Huyu kwa mtaji huu anaweza kuambiwa kuua akakubali, na kesho akajitetea "mie sio muuaji, niliambiwa tu na wakubwa kuua".
 
316444_2385989848381_1209820481_32959751_2885080_n.jpg

Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia

Hoja zake kubwa ni hizi:

1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.

2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .

3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.

4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:

a) Kwa nini iliondolewa in the first place

b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana

c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service

d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake

5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?

6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.

7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?

Je william anajua:

a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!

b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo

c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?

d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.

8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?

9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.

10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.

In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.

William kama mawazo yako ni hayo then I give up!

MPISHI WA KWENYE MELI ANATAKA UBUNGE??HIVI KWA SABABU MTU ALIWEZA KUTUMIA LILE LI MWIKO LIKUBWA KUWASONGEA UGALI MABAHARIa MELINI BASI ANAFIKIRI ANAWEZA KUWA MBUNGE.HIVI JAMANI HATA KWA SURA TUU HUYO ANAFAA KUWA KIONGOZI??UNAJUA MPISHI NI MPISHI TUU CHEK HATA POZI LAKE
 
Back
Top Bottom