Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,039
- 3,486
Wanajukwaa
Mada tajwa hapo juu inahusika moja kwa moja kwa mjadala mpana.
Ombi kwa
1. Serikali kuu
2. Makamu wa rais muungano na mazingira
3. Tamisemi
Kwanza mamlaka husika ipongezwe kwa kutumia jeshi usu kusimamia mazingira ya eneo lote lla wilaya ya Kisarawe dhidi ya wavamizi na matajiri waporaji wa ardhi kwa ushawishi rupia kwa wenyeji wasio na ukwasi. Msitu wa Kazimzumbwi umedhibitiwa vuzuri sana kuanzia Vikindu Mkuranga hadi Kisarawe ijapokuwa kuna baadhi ya maeneo yanavamiwa kimya kimya na watu kisha viongozi wa kisiasa wa ngazi za juu wakipendezwa na maeneo hayo nao wananunua na kujenga kisha serikali kuhalalisha ukaaji watu.
Serikali isifanye kosa kama ilivyofanya kwa kuzembea msitu wa Mabwepande kumegwa kidogo kidogo hadi kwa sasa kimebaki kipande kidogo sana katikati ya makazi ya watu hivyo kushindwa kusafisha hewa za ukaa zinazozalishwa na uchafuzi wa mazingira, viwanda nk hata hali ya hewa inashindwa kuwezesha mvua za kutosha kunyesha maeneo makubwa ya mkoa wa Dar Es Salaam. Imebaki mvua inanyesha Mabwepande, Bunju, Tegeta, Madale, Msumi, Mbopo, Kinondo, Mbezi Msakuzi na Kwembe pekee.
Barabara ya lami iliyosimama tangu 2021 inayoelekea Masaki, Mkamba, Maneromango hadi mbuga ya utalii ya Nyerere huko Selous ikamilishwe maana wananchi wa huko wanalalamika sana kwamba wameikosea nini serikali yao? Huko ndiko mojawapo ya barabara utakuta mabasi ya miaka ya 70 na 80 (Leyland Albioni, Benzi) wanatumika kana kwamba hawana haki ya kwenda na mabadiliko ya vyombo vya usafiri vya kisasa.
Halmshauri ya wilaya ya Kisarawe itunzwe vizuri kimazingira ni urithi mzuri kwa vizazi vilivyopo na vijavyo kwa kuhifadhi misitu na uharibifu wa ardhi maana ndio eneo lililo juu sana katika usawa wa bahari