Wiki moja kabla ya Machozi... Zitto???


Hoja hiyo hapo juu ni NZITO sana tu...Na kusema ukweli kama hayo hapo juu ni kweli...Basi pamoja na yote yaliyokwisha tokea...Something gotta be done.
Na kweli kama nilivyosema hapo awali...Usalama wa Taifa nao umegawanayika...Na wale wanaomlaumumu Zitto pale anapotembea na chakula na maji yake..Basi wana wivu kuwa hawawezi kumwua kirahisi...Na badala ya hao viongozi wakuu wa nchi kuchukulia hii ni PORORJO...Basi wananchi WAANDAMANE mpaka HAKI itakapopatikana na UMAFIOSO HU KUWEKWA BAYANA.
 
Heshima Mbele

Mimi ningependa ieleweke wabunge tulionao hasa hawa vijana ni watu muhimu kwetu na tunawahitaji kwa miaka mingi na siku zijazo hivyo ni muhimu wakalindwa kwa gharama yeyote na tusipende kudharau hata jambo dogo.

Tena leo nimependezwa na michango ya Mbunge Halima Mdee sijui siku nyingi hakuwepo alikuwa wapi Big up Halima wachemshe hao wazee hasa huyo fisadi Londa
 
Serikali inaonekana imeshikwa pabaya..Sasa baada a issue waliyotaka iwe ya kisiasa kugeuka na kuwa ya kitaalam kwa wana jf wasioyumbishwa..Naona wamemtumia MKURUGENZI WA MASHTAKA KUWAPIGA WAZALENDO STPOP wasizungumzie kuhusu mambo ambayo karibia yawakute wengine ambao wako hai kama kina Zitto...Kina Zitto nawaonea HURUMA SANA..Ila Mungu yuko na nyie kwani kama ni KUFA basi wangeshawaua kitambo..Lakini wakati wa Mungu kamwe hauwezi kuzuiliwa ukishafika!

Habari za Wangwe sasa zapigwa `stop`

2008-08-07 09:56:26
Na Romana Mallya


Vyombo vya habari pamoja na taasisi nyingine, vimepigwa marufuku kufanya upelelezi kuhusu ajali liliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CHADEMA, marehemu Chacha Wangwe.

Badala yake, vyombo hivyo vimetakiwa kuacha kazi hiyo ya upelelezi ifanywe na Jeshi la Polisi.

Onyo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Eliezer Mbuki.
Aidha, Bw. Mbuki amevitahadharisha vyombo vya habari na taasisi kuwa, kama vitaendelea kuandika habari hizo, vitawajibishwa.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Bw. Mbuki alisema habari zinazoendelea kuzungumzwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, zinaweza kuleta madhara baada ya upelelezi wa polisi.

Marehemu Wangwe, alifariki dunia kwa ajali ya gari Julai 28, mwaka huu wakati akiwa safarini kutoka mjini Dodoma kuja jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Deus Mallya aliyekuwa pamoja na marehemu Wangwe, tayari amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari la marehemu akiwa hana leseni na kwa mwendo wa kasi na hivyo kusababisha gari hilo kupinduka na kumuua Mbunge huyo.

``Endapo vyombo vya habari vitaendelea kuandika habari hiyo na baadaye kuonekana kuwa vilipotosha ukweli, itasababisha vyombo hivyo kuwajibishwa,`` alisisitiza.

Alisema kutokana na madhara hayo, wahusika wanaweza kuwajibishwa kwa kuvuruga upelelezi na kuingilia uhuru wa Mahakama.

Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa, wameripotiwa kumtuhumu Mallya kuwa ni jasusi aliyewahi kupata mafunzo hayo nchini Libya.

Mkurugenzi huyo wa Mashtaka, aliyasema hayo alipotakiwa na Nipashe kutoa msimamo wake kuhusu habari zinazoendelea kuandikwa na kuibua mambo mbalimbali wakati kesi hiyo ikiwa tayari imefikishwa mahakamani na polisi wanaendelea na uchunguzi wao.

``Mimi nadhani tuliachie Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ya kupeleleza tukio zima la ajali na vyombo vingine navyo visubiri upelelezi huo, kwani kwa kuendelea kuibua mambo na baadaye kuonekana ni uongo yanaweza kuleta madhara na kuwajibishwa`` alionya.

Aidha, Bw. Mbuki alisema Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Bi. Sakina Dotoo alitoa maelezo mazuri kwa vyombo vya habari, hivyo hakuna haja ya kurudia kwani maelezo yake yanajitosheleza.

Alisema Bi. Sakina alisema kuwa, lengo la jukwaa hilo ni kuleta usawa wa habari na kwa kila mtu na jukwaa hilo halifungamani na upende wo wote wa chama cha siasa na aliahidi kuwa watasimama katika msimamo huo.

SOURCE: Nipashe
 
Mi nashangaa sana..mbona wanamuandama zitto wa watu.....wakati kuna mtu anaitwa Slaa anatamka kabisa hadharani kua ana habari nyeti za nzito za wwatu wazito lakini sisikii wakimfuatilia kama Zitto...au wanamuogopa???
 

Mzee umefika mbali, punguza munkari mzee, taifa hili ni letu wote tukianza kuwanyonga da! hapo si tutazua kitimtim?
 
.....wakati kuna mtu anaitwa Slaa anatamka kabisa hadharani kua ana habari nyeti za nzito za wwatu wazito lakini sisikii wakimfuatilia kama Zitto...au wanamuogopa???
__________________
Mkuu huyu Slaa ni mteule wa Mungu au kwa kifupi ni Nabii ambaye hata upange vp huwezi ukamfikia mbinu zako zinayeyuka.Angalia vizuri ile list of shame ya Mwembe Yanga alimtaja na Muungwana lakini hakuna kesi yeyote waliyo mfungulia huyu Mtikila kasema Muungwana Gaidi tayari wamesha mfungulia kesi.Huyu mkuu hawawezi kumfanya lolote lile alisha pewa upako.
 
niliandika huko nyuma na hapa narudia, atakayeitumbukiza nchi kwenye mauaji, kiburi, umwagaji damu siyo mwingine bali ni rostam aziz, nilisoma mahojiano yake kuhusu mtikila, mtu nuyu ana dharau kali, anaamini kuwa pesa zake zimemweka mbali sana, anajiona yuko mawinguni na sisi tupo huku chini tukinyoosha mikono na kuomba toba kwake. ni mbaguzi rejea maelezo yake kuhusu mtikila kuwa haweza kumjibu kwa kuwa ananuka, yaani mtikila nanuka kwa kuwa ni mweusi tii.

mtu huyu na wote wanaombaba ni iterwhamwe kama rwanda, naomba kama mna nafasi someni makala ya padri privatus karugendo kwenye gazeti la mwanahalisi la jana, ROSTAM AZIZI NI NANI?
 

Maadui wa zito ni
miundo mbinu mibovu inayoelekea kigoma,barabara hazipitiki,reli nayo ndiyo hiyo hadi inabidi upande juu ya dari.
Wananchi masikini kule hawewezi nunua hata kandambili FUNZA ZINAWAMALIZA vidole kule kigoma .Hao ndio maadui wakubwa wa zito

Hakuna adui mwingine labda kama ameonekana kwa sijui ramli ama lamuli akipaa masafa mafupi.
 

na wananchi wengine hawakabiliwi na maadui hao isipokuwa Zitto tu?
 
Mimi ningependa sana kuona
1.Ahadi za Zitto aliwaahidi nini wananchi wake wakati wa uchaguzi na nini amefanikisha kati ya ahadi zake.Naamini suala la buzwag halikuwamo ktk ahadi zake za direct kwa wananchi
2.Pia vivyo hivyo kwa DR SLAA.

Nitashukuru sana DR SLAA na ZITTo mkinipa ahadi zenu wakati wa uchagunzi mkuu kwa wananchi ili na mafanikio yenu hadi sasa ili UMMA uwaelewe bayana nini kwanini, wapi lini.ASANTE.
 
na wananchi wengine hawakabiliwi na maadui hao isipokuwa Zitto tu?


wao ndio tumewakabidhi B52 ,ndio maana wanaposema bungeni wanalindwa na sheria na mkao mmoja tu ni zaidi ya mshahara wa polisi wa mwezi mnaowataka wafanye uchunguzi makini.
 
Hii nayo VIPI? Au hamjasoma magazeti?


http://www.raiamwema.co.tz/08/08/06/1.php
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…