Habari MMU.
Jumanne jioni tulipata mgeni nyumbani kwetu (Housegirl). J5 asubihi nkamuacha wife na hsg home nkaenda kazini. Kabla ya kumleta yeye ndiyo alikuwa anamtaka na kusistiza ni muhimu atusaidie shughuli za hapa Home anachoka sana. Alionyeshwa picha tuliyotumiwa kwa email na kumhoji maswali kwa simu kabla sijatuma nauli (100,000) aje. Hsg katoka mbali sana Bukoba tulimpata kutokana ya kuwa ni mdogo wa Hsg wa rafiki yangu.
Cha ajabu ni kuwa toka alhamis wife aliniomba tumrudishe kwao eti hamtaki, mi nkamsihi ampe mda amzoee. Aliendelea kusema hamtaki mpaka jana usiku ukazuka ugomvi mkubwa kati ya mimi na yeye. Mwanamke haelewi kasimama kidedea Hsg aondoke. Hakuna kosa alilofanya mdada wa watu tena mpole sana. Namuuliza mke wang tatizo ama kosa lake hana hata moja anachojua yeye binti arudi kwao. Eti jamani utamfukuzaje mtu bila Kosa?
Mpaka sasa sababu kubwa ni kuwa roho yake inamchukia na anahisi si mtu mzuri. Kwa kuwa namtetea na sioni mantiki ya Hsg kufukuzwa jana kazusha kuwa nimempenda na nataka nitembee nae. Kila ninalomwambia aelewi mpaka sasa yeye kang'ang'ania Hsg lazma aondoke. Naona aibu kwa rafiki yangu aliyotutafutia kumrudisha tena kwako huyu bint tena bila kosa. Pia sitaki wanaume wenzangu ambao wananikubali waone kuwa naburuzwa na mwanamke.
Kilichonifanya niandike hapa ni kuwa kasema kama Hsg haondoki mpaka kesho basi ataondoka yeye aniache naye. Mimi nafikiria kukomaa kama anaenda na aende sitaki anipande kichwani au nakosea? Nishaurini jamani maana tatizo ni kwa nini analotaka lake na ni lazma liwe?
UPDATE
- Ahsanteni sana kwa ushauri wenu ingawa ni tofauti na nlivyofikiria nimefuata mawazo ya wengi.
- Nimeongea na rafiki yangu aliotutafutia na alimuomba nimpeleke kwake na ndivyo nlivyofanya asubui hii ya leo nimempitisha ninavyoenda kazini, Kwa sasa binti yupo na dada yake kwenye nyumba moja.
- Kuna wengine walihoji kuhusu hsg kuwa na email, Mkisoma maelezo hapo juu utajua kuwa dada wa hsg tuliyeletewa anafanya kazi kwa rafiki yangu, Picha ilitoka kwa dada yake na best yangu ali scan na kututumia ili tumu aprove kabla hajaja. Wife aliiona picha na kuongea naye kwa simu.
- Mpaka sasa hana sababu yeyote ya maana ya kumkataa.
- Kwa mlioomba Hsg kidogo itakuwa ngumu, best kakataa kwa usalama wa binti maana yeye ndio anawajibika kwa wazazi wake.
Mwisho wa yote nilijishusha na kukubali kushindwa. Leo nimefanya anavyotaka yeye sasa namsubiri kwa hamu aanzishe jingine tena.
Ahsanteni kwa mawazo yenu. Si mjaji wa huku sana hivyo sitaweza kujibu maswali yenu papo kwa hapo.