Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

yup! Niliambiwa na moja ya staff kuwa hata TTCL mobile ilicheleweshwa kwa makusudi ili kampuni nyingine zisiende mrama maana ingekuwa cheap sana. Je inawezekana uongozi wa juu kuna mapandikizi yaliyopo kwa interest ya kampuni nyingine?
Hata wafanyakazi wa chini hawapo motivated sana! So what should we do ili tuiokoe kampuni yetu?
Mbona sasa wapi kwenye mobile na hawako cheap kihivyo
 
Sasa hivi wapige chini management yote walete wazungu kama walivyofanya waarabu na iondolewe kwenye mfumo wa ruzuku ijiendeshe yenyewe hapo labda tutafika
 
Data price should be halved to ensure majority of pple in Tanzania accrue the benefits cyber world brings.
 
TTCL imeachwa ikafa kifo kibaya na sisi Watanzania wenyewe. Na its no wonder ikaja kufa kabisa tukabakiwa na stories & tales that tuliwahi kuwa na shirika kama hilo. Celtel ndio alikuwa wa kwanza kumuumiza TTCL kipindi hicho na viongozi hawakusema lolote walifumba macho. Kuna kipindi Mhe. Zitto ali~raise hili swala ila kama kawa likapotezewa. Bahati mbaya hatuna desturi ya kutunza na kulinda mali zetu watanzania
 
It's simple. TTCL lilikua shirika la serikali. Mashirika ya kiserikali ni ngumu kuwa competent kwenye market kwa sababu wafanyakazi wa serikalini na management kwenye ayo makampuni sio competent. Ni ngumu kuajiri wafanyakazi ambao ni competent kwenye mashirika ya kiserikali kwa sababu maslahi ni madogo kulinganisha na mashirika binafsi. Private sectors zitazidi kuongoza maana maslahi ni mazuri na watu competent ndio wanakimbilia uko. TTCL ni moja ya mashirika ya kiserikali yenye changamoto iyo.
 
Please dont mislead people in this forum.

1. Wireless modem ni TSH 50000/=
TTCL has best rates for internet services. Check out this
2. 2Gb bundle for only 30000/= Broadband adsl
3. 4gb bundle for only 60000/=

Lakini from the orignal thread, matatizo ya TTCL yameletwa na serikali yenyewe na sio management wala wafanyakazi. Serikali imefanya utapeli na MSI-Detecom kwa kuuza hisa 35 kwa dola mil 65 badala ya 120.

Ni serikali iliyodhoofisha juhudi za kuanzisha kampuni ya mobile ya TTCL iliyokuwa na jina la Celnet na mtaji ukatumika kuanzisha Celtel wakitumia rasilmali za TTCL.

Ni serikali iliyoleta management ya kigeni Saskatel ya Canada ambayo iliishia kuchota fedha za wazalendo na kuondoka bila kuleta ufanisi hata kidogo.

Haya yote ni matokeo ya viongozi wasiokuwa wazalendo wenye ubnafsi na wanaotaka TTCL ife ili makampuni ambayo wao wana hisa kubwa kubwa yashamili.

Someni vizuri hiyo habari kamili.
Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru
Nimelia sana niliposoma habari hii, i wish i could be a president even for 24 hrs
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!
Kwakweli nchi hii kulikuwa na mambo ya ovyo sana ovyo kabisa! Acha Magufuli atunyooshe tu, maana hamna namna sasa!
 
Duuuh mi niko nje ya mji lakini mnara umesimama mujarabu kabisa nimekuta nikiipenda TTCL

Niendelee nione watatubadilikia au wataendelea kufanya mujarabu
 
Mkuu sio kwamba hawawezi kuwa successful bali hawataki kuwa successful, they are not running a company as profit oriented no one cares..., and no one is accountable..., so long they get their salaries.

Its the same reason why Air Tanzania is not the leading Airline Company...
Hili ni ttzo karibu katika kila sekta Tanzania,watz hatuko self motivated,mtu mpaka asukumwe na hawezi kujishurutisha mwnyw kufanya kitu,na hili cjui chanzo ni nn hasa,cjui ni malezi!
 
hapa shida siyo TTCL mi nadhani shida ni hujuma za viongozi wenye hisa kwenye makampuni mengine ya simu, hawa jamaa wanajua kabisa TTCL ikiacha itawale soko ni nini kitatokea kwa makampuni yao. mi nafkiri tukipata viongozi wanaojua wajibu wao kwa taifa basi shilika hili litakuwa ni moja ya mashirika wanayojivunia watz.
Maneno huumba.
 
Binafsi sipendi haya makampuni ya umma yawe na monopoly....mara nyingi yanakuwa inefficient na mwishowe gharama inakuwa kubwa kwa watumiaji. Wakati TTCL ipo dominant wengi mnajua simu ilivyokuwa ishu...ni kama Tanesco ilivyo sasa hivi. Sasa hivi ukiomba servive line ya Tanesco...inakubidi kusubiri mwezi mzima ukiwa na bahati...la sivyo ni kuanzia miezi mitatu na kuendelea. Hivyo ndi ilivyokuwa TTCL wakati ikiwa na monopoly kwenye soko la simu.
Duh
 
  • Thanks
Reactions: SMU
For obvious reasons... Like having a board of directors full of the dumbest individuals making final decisions.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom