Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!

Dah. hii ni kali kupita zote
 
huyu mkuu wa iki kitengo cha BIG RESULT NOW ndo aliyeitrick serikali kuwaingiza wahindi ktk shirika hili na kwa kutumia leseni ya ttcl wakaanzisha celtel leo hii JK kamuona wa maana anampa kitengo cha BRN.
 
  • ASANTE SANA KWA MAELEZO YENYE MAANA NA YAMENIFUNGUA KWELI MAANA NILIKUWA SIJUI BAADHI YA VITU.WE NEED TO PROTECT OUR TTCL

Pole TTCL
 
safi sana umeeleza vizuri na hakuna cha kuongeza hapo labda nikukumbushe wakati TTCL ikiwa iko sambamba na zain waliweka alama ya mfanao wa nike chini ya neno TTCL kuonyesha sasa inaenda kufa ila baada ya kujitenga ttcl walirudisha ile logo yao ya kale na ndo inayotumika mpaka sasa hivi

Ni kweli kabisa alichokieleza mkuu Shingo, mwezi wa 6 mwaka huu nikimgda na jamaa mmoja mzalendo yuko ttcl. Nilimlaumu sana makumuliza kwanini wanasuasua kutoa hudama nzuri ya simu za mkononi, akaniambia kuwa wasingeweza kwani Celtel (Airtel) waliizuia ttcl isitoe huduma hiyo. Pia alinipa habari njema kuwa mwishoni mwa mwaka huu ktna huwezekano ttcl wakato huduma hii kwa kasi mpya, ikiwa ni pamoja na GSM.
 
Last edited by a moderator:
kitu kikishakuwa `public owned` baaas lengo la kufanya biashara ili kupata faida linapotea,mixer hizo hujuma kibao lazma waachwe na mitandao mingine ,haki ingekuwa hela za watu ndo zimewekwa hapo na wanasubiria dividends kila mwaka ttcl wangekuwa zaidi ya mbali sana,in my opinion partial privatization could be a solution
 
wanayoimaliza TTCL wamo ndani ya TTCL na pia mikataba mibovu ilyoingizwa kampuni wengi wanakwamisha maendeleo ndo mana upande wa data kila siku ni mauzauza wakati kila kitu kipo kuna watu wanatakiwa waachie nafasi zao wamekaa tu bila faida yoyote hawana uelewa wala fikra ya kuchambua na kujua nini sokoni kunaitajika wamekaa tu maofisini
 
Mkuu hatuongelei monopoly ni kwamba private companies ziingie pia ila TTCL nayo iwe kwenye ushindani..., competing on the same level field lakini cha ajabu ni kwamba they have everything lakini hawataki kabisa ku-compete kwenye mobile phones..., na sio kwamba hawawezi. Which brings some people to think probably wana share kwenye hizo private companies au they gain something by TTCL not doing well. labda wabadilishe mfumo na waanze kuwalipa ma CEO wao kulingana na performance na profit

tatizo kubwa linalozikumba ofisi za serikali na wafanyakaz wake ni kujua kwamba mishahara yao haitokani na uzalishaji bali kodi sie wengine tulio ktk private sector!!! kukubali kusdhindana na kupata faida kunaitaja kujituma na kuchemsha bongo kwa mtu mwenye uhakika na mshahara ni ngumu sana kufanya ivyo!!

na lingine tukatae tusikatae ni ajira za kujuana, sijawai ckia ttcl wanatangaza ajira lakini kila cku wafanyakaz wanaingia na kutoka, hapa linazaa tatizo la incompetence, serikalini kuna shida kubwa sana ya competence wafanyakaz wengi uwezo ni mdogo either kwa kupata ajira za kujuana au kukimbilia job security maana serikalini hakuna kupima perfromance ukifika kazini asbui jion unatoka ushaingiza cku.

hata cku moja huwez endesha shirika technical kwa icompetent people utakua exposed tu, ndo mana kwa tendency hii ya watu wengi kua incompetent mashirika yanaiyoitaj technical capability na akili nyingi kubwa kuliko siasa yanafail mfano no hili ttcl,nasaco, uda, mecco,bandari, air tz, tazara, reli, all manufacturing industries, tanesco etc kwa watu dhaifu unaweza endesha mashirika au taasis zisizoitaj akili nyingi kama bank, bima, mifuko ya jamii , tume mbalimbali , ofisi za serikali nk
 
acha uongo
 
Nashauri haya mashirika ya uma yawe listed DSE kuleta tija kwenye uwendeshaji.
 
Halafu kuna watu wanataka CCM iendelee kutawala,Hiki Chama kinachoongoza serikali kimejaa watu wenye akili fupi na wasiojitambua hata kidogo.Wakati mwingine hata hao Wazungu wanaoshirikiana nao kuyahujumu mashirika ya umma huwa wanashangazwa kiwango cha ujinga kilichowatawala hawa viongozi wetu,hii ni aibu!!"
 
Dah nikisikia ttcl ilipofika natamani waliosababisha ifike wafe mana wamekosa uzalendo ivi hii nchi inaongozwa na walevi wa gongo au mana mambo ya kipuuzi yanafanyika af yanafumbiwa macho mfano mzuri ni general tyre,zzk Mbeya na kiwanda cha mbolea tanga yani ccm ni corrupt af na viongozi wake ni corrupt!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Halafu kuna watu wanataka CCM iendelee kutawala,Hiki Chama kinachoongoza serikali kimejaa watu wenye akili fupi na wasiojitambua hata kidogo.Wakati mwingine hata hao Wazungu wanaoshirikiana nao kuyahujumu mashirika ya umma huwa wanashangazwa kiwango cha ujinga kilichowatawala hawa viongozi wetu,hii ni aibu!!"
eti akina lukuvi, wasira, sophia simba, nchemba,...... Ndo think tank ya selikali!! Hakyanani kwa hiyo "cream" mabua lazima yavunwe.
 
Tatizo sio ttcl, tatizo mkataba ambao serikali ili ingia na celtel (msi) ambao unaifanya celtel kuwa na share ya 40% ndani ya ttcl, wakati wote wanafanya biashara zinazofanana yaani internet na simu. prof msola alikuwa anataka kuvunja mkataba huo wenye share waliopo serikalini wamehakikisha haludi pale wizarani.( msi) ni warioba, salim, maua daftari,Ttcl kila ikifanya mipango yake msi wanapinga au wanachelewesha inapitwa na wakati, dawa ni kvunja mkataba kati ya TTCL na MSI ili ttcl ijiendeshe yenyewe
Platinum warioba yumo!!
 
TTCL wamesambaa Tanzania nzima iweje wapitwe na vikampuni kama Halsted.?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom