I'm pulsed as well.
1.00 USD = 1,295.99 TZS
Two weeks ago was 1,156
.
kwa muda wa wiki wa wiki moja sasa, thamani ya shilingi ya tanzania imeshuka kwa kasi ya ajabu, mfano mwanzoni mwa mwezi huu ilikuwa exchange RATE KAMA HIVI $ TO SHILING 1138/=, LEO KWENYE BENKI YA STANBIC MBEYA ILIKUWA ALMOST SHS 1300/= KWA DOLA!
KUNA NINI? MBONA BEI YA MAFUTA IMESHUKA KWENYE SOKO LA KIMATAIFA, NI NINI KIMEIPATA SHILINGI? TUNAOMBA WACHUMI WATUSAIDIE, ISIJE IKAWA KUNA UFISADI FULANI UNAFANYIKA KUSHINIKIZA BEI YA PETROL IPANDE KWA KISINGIZIO CHA KUANGUKA KWA THAMANI YA SHILING
Kwi kwi kwi hao wafanyakazi wanaishi na kutumia vitu ambavyo shilingi ikianguka vitakuwa bei kubwa mno. Hawatakubali kuendelea na mishahara ile ile ya zamani. Pia lazima ujue kwenye production yoyote mishahara inachukua asilimia ndogo tu ya matumizi ya viwanda au biashara nyingine.
Kwa theory yako basi Wazimbabwe wenye dola nje wanafaidi wakizituma kule kwao ambako shilingi yao imeanguka vibaya?
Kushuka kwa pesa ya nchi kunakuwa na faida kubwa kama tu mnauza vitu vingi nje kuliko mnavyoagiza kwa maana ya kwamba vitu vyenu vitakuwa cheaper na hivyo ku attract wateja zaidi. Lakini hata hapo bado inflation inaweza kupanda na hivyo kuja na matatizo yake mengine.
Tatizo ni kwamba tuna-import zaidi ya ku-export resulting to an unfavourable balance of Payment position ndio maana currency yetu haina thamani. Halafu tatizo ni kwamba our values of imports are too high kwa mfano, mtu aki-import Land Cruiser VX yenye thamani ya millioni mia je tutahitaji ku-export mazao kiasi gani ili tubalance na importation ya hio gari? ni kiasi kikubwa sana. na huu ni mfano mmoja tu bado hatujahesabu vitu vingine vya thamani mno ambavyo vinaletwa nchini. Nchi hii inahitaji 'industrialisation' phase kama nchi zingine zote zilizoendelea. Hao mafisadi japo wajenge viwanda na hizo pesa kuliko kuzipeleka nje.
Why shilling is depreciating at alarming speed!
Najua utakuwa unagonga kichwa ukutani na kusema: HIRI LIJAMAA BWANA RINARETARETA UBISHI TU KATIKA MASUALA YA UCHUMI.
Zakumi,
Hapana mkuu hapa ni kueleweshana tu. Kila mtu kuna vitu anajua kuliko mwingine. Tukiunganisha pamoja ndio uzuri wa JF. Wakati mwingine kubisha ndio njia ya kujua.
Uchumi ni mgumu sana. Mwaka jana nilisoma financial strategy, mimi kama Engineer nilikuwa naona mambo mengi ni madudu tupu.
Lakini thanks to credit crunch, kwa kusikiliza radio/TV tu nimejifunza mengi kuliko miezi sita ya kuhangaika na hiyo financial strategy.
Ningelikuwa na uwezo wa kurudia hilo somo sasa wangenikoma kwi kwi kwi!!! (It doesn't matter what you know, but when did you know it).