Nilikuwa na takribani miaka miwili sikuwa nimeenda Dar (Jiji kuu la kibiashara,Tanzania)....
Two weeks ago, nilikuwa huko na kukaa siku mbili.
Nilienda kwa usafiri wa njia ya barabara na nilianza kuingia mjini kuanzia Mbezi, Kimara all the way to Ubungo na kisha City center.
Kuanzia Mbezi sikushangaa sana ubovu wa barabara na shughuli kutokuwa ktk mpangilio maalumu.....
Nilidhani labda ni kwa sbb ya ujenzi wa upanuzi wa barabara hii ya Morogoro all the way to Chalinze unaofanyika (na sijui kama itakamilika kweli kwa sababu niliona mkandarasi kama yuko slow sana. Sijui sababu ni nini)
Baadaye nilitembelea maeneo mengine ya jiji. Nilipita mitaa ya Msimbazi, Kariakoo, Shule ya Uhuru ambako kuna shughuli zisizo ktk mpangilio za biashara za wamachinga kiasi ambacho kama unatembea kwa miguu, utakiona cha mtema kuni....
Baadaye nikapanda ferry nikavuka na kuingia Kigamboni....
Inasikitisha sana kuwa nadhani katika jiji la DSM, Kigamboni labda ndiyo eneo la hovyo kabisa lililosahaulika kwa kila kitu; miundombinu ya barabara, huduma ya maji nk
Kwa ujumla nilishangaa kidogo kuona jiji hili kubwa kabisa, ni miongoni mwa miji chakavu na michafu kabisa ukilingqnisha na miji kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Moshi nk....
Pamoja na ngonjera na majigambo ya ya RC wa mkoa huu, Ndg Albert Bashite Malyangili a.k.a Makonda, sikutegemea kuona mji usio na taratibu na miundo mbinu rafiki kwa jamii ya watu wote iwe waenda kwa miguu, waendesha bodaboda, wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa nk
Ninachotaka kusema ni kuwa moja ya indicator ya umaskini ni utaratibu wa maisha ya watu wa kila siku kwa kuzingatia mpangilio wa shughuli zao.....