Ndugu yangu Mwanakijiji, ni kweli kama unataka kumsaidia mtu ni vema kumkosoa kwa yale mabaya hayafanyayo na pia vyema kumpongeza kwa yale mazuri aliyoyafanya. Ninaamini waliokuwa karibu naye huwa wanamueleza na kumkosoa kama vile ile hotuba ya wazee wa Dar. Ilikuwa kali mno kuliko suala lenyewe. Ninachokisema hapa ni kuwa huyu ni kiongozi wa nchi yetu, ni msemaji mkuu wa nchi yetu, amechaguliwa kwa kura nyingi, tumpe heshima yake jamani. Mimi hata angekuwa rais anatoka CHADEMA bado tungempa heshima yake kama rais wetu. Tumheshimu rais wetu ndugu zangu. Mimi si mwananchama wa chama chochote ila napenda kusisitiza kuwa lazima kuwaheshimu viongozi wetu.
Tuangalie na maneno tutumiayo hasa wakati wa kuchangia mada kama hizi. Kwa mfano mtu anaka anafikiria eti Rais akifa achukue nani nchi. Kwa hasa binadamu ukae kuwazia fulani kufa???????. Huu si ustaarabu hata kidogo. Naombeni pia ile mada iondolewe maana haina maana.
Ndugu yetu Kikwete amefanya mengi ya kusifiwa, kweli yawezekana kafanya mengine si ya kupendeza ila ametijahidi sana kwa kipindi hiki, tusibiri kipindi cha pili atasukuma ngwe salama naamini hilo.