why do u cheat??

Amen wanandoa tunalisubiri kwa hamu!!!baba paroko
 
tatizo kubwa ni tamaa,
wapo wanaopewa kila kitu huko kwenye nyumba zao lakini bado ana cheat.
sijui labda ni kupata experience mpya.
lakini hiyo yote imesababishwa na watu KUSHINDWA KUZUIA TAMAA ZA MWILI.
 
Jamani wanandoa muache uzinzi mtaua wenzi wenu. sababu ya kuwa mbali na mwenzio isiwe kikwazo. mfano mimi ni msichana lakini nimekaa miaka 2 bila kukutana na mwenzi wangu na cjacheat. na si kwamba wanaume hawanifuati wanakuja wengi sana ila sina interest na kwanza naona kero tu. kwann ucheat wakati unae mwenzi wako?

the only solution ni kuchange yourbrain frequency(kama radio hahaaaa) towards kucheat. hakuna cha nature wala nn. JUS SAY NO TO TAMAA ZAKO VIZURI VIPO VINGI JAMANI NA HAVIISHI KILA CKU WANAONGEZEKA KWA UZURI
 

Sisi ni binadamu tuna akili na utashi wa kuyacontrol mazingira. Naona ku-cheat ni tabia ya mtu tu wala hakuna lingine. Kama mwenzi wako unampenda unamuheshimu na kumthamini. Hebu jiulize, kwenda huko nje ya ndoa yako vipi na mwenzi wako atoke nje? Si cha mazingira wala nini, kama unaona mazingira siyo mwafaka kwako ondoka ili Usije tumbukia kwenye zinaa. Kukosana katika ndoa ni jambo linalotokea, ila kutoka nje ya ndoa siyo suruhisho bali kuongeza balaa tu. Usitegemee mtu kutoka nje huko atakuletea raha katika ndoa yako. Ni nyinyi wenyewe mnapaswa kuyasuruhisha matatizo/tofauti zenu na kusonga mbele.Ukisema utoke nje km vile kukomoa haina msaada wowote bali kuendelea kujilaumu hasa pale unapojuwa mwenzi wako ni mwaminifu.

Hamuoni haibu kuvua nguo mwanaume mzima kwa mtu asiyekuwa mkeo? Kwa mwanamke, hauoni haibu kumvulia mwanaume mwingine nguo zako na kumfungulia miguu yako wakati mumeo unajuwa yupo na anakupenda? Huwa mtu unajisikiaje ukirudi nyumbani unavyotoka kuzini? Hamkumbuki ahadi mlizoziweka mbele ya Mwenyezi Mungu? Huoni kama huyo mwanamke unayelala naye akimjua mkeo ni kama amemvua nguo mkeo? Huoni kama huyo mwanaume uliyelala naye mkionana naye wewe mdada/mama ukiwa na mumeo ni kama Umemvua nguo mumeo?. Hebu kuweni na haibu jamani, Mpende Mkeo/mumeo ndo huyo Bwana aliyekupa. Kuonja onja nje hakukuongezei kitu chochote katika ndoa yako bali kuleta mikosi katika familia. Tulizike na wana ndoa wenzetu.Matatizo yanayotuzonga tuyazungumze na kuyamaliza. Nampenda Mke wangu, majaribu kama yananizonga na naona ni hatari najitahidi kuyakimbia, na kumwona mke wangu ndiye mzuri tu kwangu huwa anafanya assumption wanawake wengine wameshachakachuliwa kwa hiyo haitatest km ya mke wangu. Ni mawazo tu lakini.
 
--una roho ya uzinzi??
--mkeo/mumeo kakuudhi??
--una laana ya kutoka nje ya ndoa kwenu??
--ukuwa umejiandaa kuoa/kuolewa sasa cha moto unakiona??
Goodmorning
najua na mengine mengi tu yawezekana wewe ni muathirika wa kutoka nje ya ndoa....ndugu zangu leo hii tuanze kuangalia jinsi gan ya kutatua matatizo ya watu ili tuwe na baraka majumban mwetu..akuna anaependa kuona wanandoa wakiwa kwenye magari wakiangalia opp sied like if jaman nafika saa ngapi...ni kweli atukatai ndoa ni nzito na ngumu na inaitaji swala la commitment kweli na si kuoa ama kuolewa sababu babu bibi amezeeka asife bila kumuona mjukuu wapo wanaooa kwa sababu ndugu wote wameoa ama kuolewa bado yeye,wapo wanaofunga ndoa sababu ya kutoa GUNDU kwenye familia yaani kwao akuna aliewahi kusikia ndoa wote wanazalishwa/wanazalisha majumban mwao na kuendelea kuishi bila ndoa wachilia kubariki hata baada ya kujifungua....lakini je haya yote yanatulazimu kucheat na hili ndio soln ya ndoa yenye matatizo..la hasha kwenu wapendwa binafsi naomba nianze kwa kusema kucheat sio soln ya shida zilizopo kwenye ndoa..zitabaki hiyo hivyo na haziishi zaidi ya kuongeza matatizo anyway sihukumu kwa kucheat la hasha Lengo ni kupata sabbu za kucheat ba ukiwa kama mwanandoa angalia sababu hizi na uangalie tutasaidianaje kuachana na kucheat....

Mi huwa nachaet tu, sijui kwa nini...
 
finest and mfamaji n others who are into the nature concept..ni kama mnapingana na MUNGU kwamba kuna uzinzi na uasherati,wen God created you alikupa only one kathing and that means ni kwa mmoja kaka lasivyo angekupa mia,.cheating is both sides ila most men have lost their screws that make them human beings,kuna tofauti kubwa kati ya mwanadam na mnyama,so unature wa mwanaume utaly kwenye taking care of his family co kusaidia kuridhisha wengine..fear God...P.DIDDY U SAID SMTHINGS SO GOOD,THNX
 
finest and mfamaji n others who are into the nature concept..ni kama mnapingana na MUNGU kwamba kuna uzinzi na uasherati,wen God created you alikupa only one kathing and that means ni kwa mmoja kaka lasivyo angekupa mia,.cheating is both sides ila most men have lost their screws that make them human beings,kuna tofauti kubwa kati ya mwanadam na mnyama,so unature wa mwanaume utaly kwenye taking care of his family co kusaidia kuridhisha wengine..fear God...P.DIDDY U SAID SMTHINGS SO GOOD,THNX

Can you i ask you a hand for marriage:tonguez:
 
my dear FL1

hii ni kwa maombi huku akitumia juice ya alovera yenye kopo la rangi ya njano usiogope bei inasaidia kuweka brain stable kwa ajili ya mitikisiko ya ndoa, naona hata tukimjazia neema za ndoa atabaki na nature na anapoelekea atakwambia MR II Baada ya nature,ngoja tusubiri ma dear wengine tutajazia

"Tabia ni rangi ya ngozi huwezi kuibadili"
BUT GOD IS GREAT!
 
Kucheat sio kusema ni uzinzi au tamaa. Kuna vitu vingi vinachangia mtu kufanya analolifanya.. Wajameni msijidanganye eti kwa sababu mbele ya mchungaji mliapa basi kila mmoja alikuwa mkweli wakati ule wa viapo. Wengi wanaoa na kuolewa kwa sababu nyingi mojawapo ni 'kiherehere' msemo wa mkuu wa nchi hahahah wakati hawajamalizana na ya ulimwengu.. Kuwa mwaminifu 100% ndani ya ndoa ni 1 out of 10. Mimi siwashangai wanaocheat labda ana sababu yake ya msingi ya kufanya hivyo.
 
Kucheat sio kusema ni uzinzi au tamaa.

basi kutoka nje ya ndoa ndio TAMAA/UZINZI hapo tuko pamoja
 
Jamani wanandoa muache uzinzi mtaua wenzi wenu. sababu ya kuwa mbali na mwenzio isiwe kikwazo. mfano mimi ni msichana lakini nimekaa miaka 2 bila kukutana na mwenzi wangu na cjacheat. na si kwamba wanaume hawanifuati wanakuja wengi sana ila sina interest na kwanza naona kero tu. kwann ucheat wakati unae mwenzi wako?

the only solution ni kuchange yourbrain frequency(kama radio hahaaaa) towards kucheat. hakuna cha nature wala nn. JUS SAY NO TO TAMAA ZAKO VIZURI VIPO VINGI JAMANI NA HAVIISHI KILA CKU WANAONGEZEKA KWA UZURI

miaka miwili bila kukutana na mwanaume??? haya niambie hiyo plan B uliyokuwa unaitumia
 
uzinzi tu ndo unawasumbua hamna lolote,
ulimbukeni wa kushindwa kucontrol tamaa za kimwili,
kutoka nje ya ndoa yako takatifu ni ushamba,period!
Hebu nipe contacts zako........watu tunahangaika hapa kumbe kuna watu kama ninyi. Yaani hapa mama hakuna kuchit ni wewe tu bimdogo na my wife
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom