Macbook pro
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 665
- 902
Habarini za wakati huu ndugu wana-MMU,
Hongereni kwa Majukumu na kwa Changamoto mnazopitia kwani hizo ndio Maisha menyewe. Ni muda umepita toka niweke post yangu hapa MMU.
Mimi ni kijana (31), asili yangu ni kanda ya Ziwa nikimaanisha Geita ila naishi Musoma kwa sasa. Katika maisha yangu ya utotoni nilibahatika kuona maisha waliyokuwa wakiishi wazazi wangu. Hivyo nimekua hivyo mpaka nafikia utu uzima ndipo nikawa nimeanza mambo ya mahusiano.
Nirudi nyuma kidogo, nimewahi kulelewa na Babu yangu mzaa Baba na mimeona mengi kwenye maisha yao ya ndoa. Babu yangu alikuwa ni mtu kupenda wanawake sana (Womaniser) lakini hii haikuwahi kuleta mgogoro nyumbani kwani Bibi hakuwahi mfuma ila sisi wajukuu tulikuwa nmtunaona harakati za Babu yetu.
Na hata mzee wangu naye vivyo hivyo naye alikuwa mtu wa kupenda wanawake, yaani kusema tu ukweli ni kwamba wazee wangu karibu wote waliwahi kuoa zaidi ya mke mmoja (Polygamists) lakini mwisho wa siku hao wake wa pili walikuwa wanaondoka mke wa kwanza anabakia na ndio wako nao hadi sasa. Nikiwa nakua nilikuwa nachukia ishu za wazee wangu kuoa mke wa pili, Nilikua nashangaa mnoo kwanini wanashindwa kubaki na mke mmoja tu. Imeisha hiyo.
Nirudi kwangu, Baada ya kuanza ku date nilikuwa mwaminifu hapo mwanzoni ila baadae nilikuwa natamani wasichana wengine. Nikawa najitahidi nisifukuzie ili tu nisiwe nao. Nikiwa kwenye early 20's nilibahatika kupata msichana ambaye baadae alinicheat na jamaa mmoja alikuwa Fundi radio na niliumia sana ila baada ya hapo sikukoma nikadaka mrembo mwingine huyu hatukukaa sana akaanza ingiza iahu za dini tukawa tumeachana, kwani tulikuwa imanj tofauti.
Nimefika chuo nikapata mdada hivi nikawa naye kwenye mahusiano na hiki kipindi sikua na pesa sana hivyo sikua napenda kuwa na mademu wengi. Nilipomaliza chuo tu nikabahatika nikapata kazi, shughuli ikaanza.
Nilikua na mrembo mmoja wa kingoni, alinipenda sana yule dada niseme ukweli ila mimi nilikua sio saana. Ila baadae nikampenda sana tu lakini hapo hapo nikaona kadada kengine kazuri tu kakiiraki nikawa na date nako hapo wapo wawili sasa .
Sasa hiyo hali ya kutokuaridhika na mwanamke mmoja imenitawala hadi sasa. Nimeoa juzi juzi tu ni miezi kadhaa ila tayari nina mchepuko ambaye huwa napiga mara kwa mara huyu ni Single mother. Ila kuna muda naamua kabisa kuachana naye ila ndio hivyo nikinuniwa huku na wife namuwaza huyu mrembo naye hana shida ananipa ushirikiano kwani huwa namjali pia pale anapokuwa na changamoto. Sasa nikipata ki trip cha kutoka huwa inakua kama fungulia mbwa yaani naweza Chapa hata mademu watatu au wanne mpaka narudi (ila natumia mpira).
Kuhusu mke wangu, aliwahi fuma meseji za mdada namsifia sifia na kumtongoza ukaibuka ugomvi ila baadae niliacha kuwasiliana na yule dada nikawa kama nimetulia ila sasa hivi tena kimewaka tena hamu ya kuchepuka ipo juu sana. Na nikishapiga hata ile hali ya kujutia sina tena. Na huyu mwanamke wa tatu kayi ya wale ambao nimewahi kuwa nao kwenye mahusiano na wote tuliachana kwa sababu yangu kucheat. Sasa hata hii ndoa siku nikifumwa nahisi tena tunaachana.
Ndio napata hili wazo kwamba labda ndoa sio kitu nilipangiwa, maana wanawake watatu niliwahi kukaa nao (ile sogea tuishi) wote waliniacha baada ya ishu za kucheat maana ugomvi ulikuwa mwingi sana. Nakuja kwenu nataka mnisaidie nifanyeje labda huenda nikatulia au hii hali ikatulia au namimi natakiwa nijiunge tu na Chama cha KATAA NDOA??
Naombeni msaada wa mawazo, chochote ambacho unaweza nishauri. Mind you, nimefanya sana kuomba kwa Mungu anisaidie hadi sasa wapi penyewe nina mtoto mmoja wa Nje ndoa daah . Ila Namshukuru Mungu mama wa mtoto hana matatizo na mimi nahudumia mwanangu kama inavyotakiwa.