Why always me.............?

Why always me.............?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Bahati haina kwao popote inathibiti
ili niwe na upeo nasubiri siipati
moyo nimesema nao isipokuja sijuti,

sihusudu wapatao ingawa mimi sipati
sihusudu wenye vyao siihimizi bahati
toka kale hadi leo naingoja haizuki

najuwa ntaipata utapofika wakati.....
Ila taipata lini kusubiri nimechoka
 
::
Bahati haipangwi
Inatafutwa
Bahati haigangwi
Ni majaliwa
Bahati haina hodi
Inatafutwa
Bahati haipendelei
Inataka juhudi
Bahati haijali wakati
Huja bila taarifa
Bahati hailingani
Kila mmoja ana yake
Bahati hailalamikiwi
Itakufuata ikipenda.
=
 
Najitahidi jaribu bahati yanikataa
Yanifanya niwe bubu napoteza ushujaa
Nishauliza mababu wanijuvye linofaa
Juhudi zilizosibu matunda hazijazaa
Nifanyeje?
 
U kitaka usiwe domo zege sharti ufunge redio kwenye mdomo...

U tamke maneno matamu yatokayo pasipo kikomo....

Bahati tunayo wachache tumejaliwa.
 
Misitari imetulia kama maji mtungini
vina vinaelea kama meli baharini
watunzi mu dhabiti kama jeshi ngomeni
 
Bahati?
kwamba uokote furushi la noti?
Bahati itafute mwenyewe mkuu,
komaa kama hauna akili nzuri ndo utajiona mwenye bahati
hivi hivi utalia lia tu.
 
Bahati haina kwao popote inathibiti
ili niwe na upeo nasubiri siipati
moyo nimesema nao isipokuja sijuti,

sihusudu wapatao ingawa mimi sipati
sihusudu wenye vyao siihimizi bahati
toka kale hadi leo naingoja haizuki

najuwa ntaipata utapofika wakati.....
Ila taipata lini kusubiri nimechoka

Nikisikia nyimbo hiyo mie nafsi yangu hupoa kabisaaaaaaaaaaa..
 
Bahati yanikimbia kila nikiikimbia
Bahati yanichukiaa kwake siwezi ikaribia
 
Wafurahika na nn moyo wangu kumia
Tena wanicheka nn ww umekamilia
Hebu nipe tathmini kipi umejionea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom