Why always me?

Kwanza acha kulia, Mungu ndie anayemjua wako na si vinginevyo

Kutamaniwa ni sehemu ya maisha, Hili lisiwe tatizo kwako
Kwa nini wanakuja na kuondoka unatakiwa kuitafuta hiyo sababu
Zipo nyingi, Unachagua sana kwa vigezo sio vyako, au una majini mahaba (Spiritual Husbands), au Unatamaa ya kuitwa mke kabla ya wakatio wa bwana, na mengine
Ukisha jua sababu ifanyie kazi na Mungu atakuonyesha wako
 
Pole bibiye jibu la wapi unakosea unalo tatizo unashindwa kuwa katalia wanaume na hicho ndo kitakacho kuliza tena.Ukimpata mwingine mpe ukweli na wala usimvulie mpaka kieleweke
 
Dah! Aisee haya mambo Mungu tu asaidie pole sana friend sasa inabidi utulie mwombe Mungu sana na wala usiwe na haraka na haya mambo,ipo siku yatajiset tu na utapata mtu mkweli na mwaminifu na atakupenda sana!
 
akina dada huwa wanadai kwamba wana-take time kumchunguza mwanaume kabla ya kumkubali na ndiyo maana 'chasing period' inakuwa prolonged; cha kushangaza ni kwamba kila siku wanakuja na vilio...
 
pole sana, take a break, think then urudi kwa umakini kidogo.
samahani sana wadada, unajua mimi sielewi sana mara nyingi mtu anaposema amekuwa na uhusiano na mtu kwa muda kadhaa kumbe mtu ana familia na alikuwa hajui...........
inawezekanaje unakubali kulala na mkaka hata hujui background yake? labda kama unataka ku-have fun, otherwise kama ni serious unataka kuwa na uhusiano na huyo mtu mi nadhani kabla hamjafika mbali mnaongea sana kuhusu nyie na kumzungusha kwingi kunasaidia kujua kama huyo mtu kweli hana commitment sehemu nyingine.
tatizo siku hizi mnadhani ukimzungusha sana mkaka atakimbia, kama akikimbia akimbie tu, huyo hakuwa wako, na hata akikupata kama ni mkimbiaji atakimbia tu.............. tena hiyo ndo itakuacha kwenye maumivu makali, bora hata akikimbia kabla hamjafika mbali...........................
tunatakiwa kujifunza jinsi ya kuingia kwenye mahusiano, vinginevyo tutaishia kila siku kuwalaumu hawa wakaka wakati sisi wenyewe hatujichungi.............................
umewasikia wanasema akijileta .............................., kwa hiyo wanaona kila siku kama tunajipeleka tu kwao.
 
Dah, pole sana dada. Unachotakiwa kuelewa ni kuwa haya mambo hayana formula! Kwa mfano wewe hapo unaweza kukuta kwa nyakati tofauti umewahi kutosa mwanaume ambaye angekuwa mume bora kbs kwako. Jiangalie mwenyewe kwanza unaowakubali unawapata ktk mazingira gani na ni watu wa aina gani? Mara nyingi mnawadengulia watu sahihi na kuangukia kwa wakware! Na % kubwa ya wadada wanaangalia hela kwa mwanaume kama vile hicho ni kigezo cha 'mtu sahihi'....Angalieni post nyingi za wadada humu. Na kwa wanaume wengi; Ukimpenda kwa sababu ya cheo, hela nk, sahau kupendwa na yeye! Mpende mwanaume akupende, tamani material yoyote aliyonayo mwanaume, na yeye akutamani!!
 
Tatizo kubwa ni kuwa wewe ni mzuri sana wa sura na umbo, na wazuri wa aina hiyo mara nyingi huwa wanatamaniwa tu. Hata mke wa mtu akiwa mzuri wa aina hiyo hutamaniwa.

The point is, kabla hujatamaniwa hutopendwa, kwa hiyo kutamaniwa kwako ni advantage kwako na si disadvantage, ukitaka ushauri zaidi ni pm.

Mkuu,we noma.
 
ndo u go to church to say some prayers, Mungu ni mwaminifu atakusaidia.,
I have been there sweetheart i know exactly what u feel.
Committ yourself into God's hands and let him make the lead.

mhhhhhhhhhhh
 
Pole mrembo, binadamu sio wote wanao fikiria wenzao au kujua mapenzi yanauma vp,sahau yalio pita jipe mda wakupumzika
na jaribu kujishighulisha sana na wala usimpigie huyu jamaa hata kama una maswali 101 jikaze kike,na ikitokea ukipenda tena basi usipende 100%...
 
Ooh! Pole mpendwa, mi nafikiri wadada huwa tunafanya choices ambazo si sahihi. Usiruhusu moyo wako kumpenda mtu ambae bado hujamuelewa/ kumfahamu vizuri. Tusiingie katika mahusiano kwasababu wanatuambia wanatupenda. Sometimes inabidi tuwe tunapingana na hisia zetu, yaani hata kama unaona umekufa umeoza kwa jamaa lakini jamaa haeleweki ni bora kutoingia kabisa katika hayo mahusiano. Mwisho kabisa, usiwaamini wanaume hata kidogo.
 
Back
Top Bottom