Who is MIZENGO PINDA? (private & Public)

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
847
Huyu ndiye tumeteuliwa na JK kama PM wetu mpya. Sasa kikosi cha CSI cha JAMBO FORUMS ingieni kazini

Mizengo&

Tunataka kujua:

Wasifu wake wa kielimu

Kikazi

Mafanikio yake

Voting pattern yake

Aliyofanikiwa

Aliyoboronga

na Mwishowe na muhimu zaidi tunataka kuona PRIVATE LIFE yake kama vile je ni Muadilifu? ana business interests zipi? na mengineyo

haya tena Pandora's box ifunguliwe
CV ya Pinda

Mizengo Kayanza Peter

Mpanda Mashariki Constituency

Born 12 Aug 1948- 60 Years of Age

EDUCATION
University of Dar es Salaam LLB 1971 1974 GRADUATE

EMPLOYMENT HISTORY

Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Minister 2006
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Deputy Minister 2000 2005
State House Clerk to the Cabinet 1996 2000
State House Assistant Private Secretary to the President 1982 1992
State House Security Officer 1978 1982
Ministry of Justice State Attorney 1974 1978

[ Retrieved on 6/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
 
Private life yake tena? Si private hiyo! Ya nini kuileta humu?

Lowassa alipokuwa anamtumia mwanae kama front ya Richmond tuliambiwa hiyo ni private life yake

sasa huyu Mizengo ambaye atakuwa ana enjoy maisha kwa pesa za walipa kodi ni muhimu kwetu kujua maisha yake yote. Siku atakapo kuwa normal civilian ndipo tutacha kumjua kwani atakuwa hayupo katika payroll ya ma taxpayers

Sikiliza huyu Mizengo haiwezekani akawa ni Clean kama ambavyo unataka tuamini na only time will tell kama ni Mizengo au atakuwa ni Mizengwe

in the mean time we cant give him an open cheque
 
Private life ninavyoelewa mimi ni maisha yake nje ya kazi. Kama ana mtoto aliye na umri wa zaidi ya miaka 18, huyu tena si sehemu ya private life yake. Akifanya madudu ahukumiwe kama individual. Mimi sijasema Mh. Pinda ni clean. Kwanza simjui, nitasemaje hivyo. Wasiwasi wangu ni kuwa unachotaka kifanyike ni kile kinachoitwa muck-racking! Badala ya kuangalia yale yenye impact na utendaji wake tutapoteza wakati kusikiliza tuhuma za ajabu ajabu. Kama kuna ushahidi kuwa ametumia nafasi yake kujinufaisha yeye au wale walio karibu yake, by all means ilete. Hayo mengine kama yapo tumwachie yeye na Mungu wake. Ni nani katika sisi aliye malaika wa kutupa jiwe la kwanza?
 
Je ni mwadilifu?

Je hajajilimbikizia mali?

Je hana scandali?

Je hana nyumba ndogo kila mkoa/wilaya?

Je Ni Wakurugenzi wapi wa Wilaya na Watendeji wengine yeye aliowapendelea?

Je kwa mda alivyokuwa waziri- ni amekuwa na mafanikio gani?

Is he a clean man?
 
Private life ninavyoelewa mimi ni maisha yake nje ya kazi. Kama ana mtoto aliye na umri wa zaidi ya miaka 18, huyu tena si sehemu ya private life yake. Akifanya madudu ahukumiwe kama individual. Mimi sijasema Mh. Pinda ni clean. Kwanza simjui, nitasemaje hivyo. Wasiwasi wangu ni kuwa unachotaka kifanyike ni kile kinachoitwa muck-racking! Badala ya kuangalia yale yenye impact na utendaji wake tutapoteza wakati kusikiliza tuhuma za ajabu ajabu. Kama kuna ushahidi kuwa ametumia nafasi yake kujinufaisha yeye au wale walio karibu yake, by all means ilete. Hayo mengine kama yapo tumwachie yeye na Mungu wake. Ni nani katika sisi aliye malaika wa kutupa jiwe la kwanza?

Mjomba as long as huyu mtu anaishi kwa pesa za walipa kodi hatokuwa immune from invasion ya Private life yake. Kama hupendi then live it lakini in my book he should not be immune na kuna watu kafanyanao kazi na kuna watu wtataka kusettle some scores hivyo mwanangu stay tuned

Alikuwa na Lowassa wakati bosi wake anaiba (allegedly) je alifanya nini huyu?
 
Kwangu mimi ninaona atakuwa mtu safi, sijui labda huko jimboni kwakwe...Hata hivyo mhe. Rais hawezi akachagua uozo wakati tayari kuna scandal kali kama hiyo iliyo kwisha toke...
Sijui,... jamani chimbeni...Who is Mizeng/we/o Pinda?????
 
Sasa utamhukumu kutokana na watu wanaotaka ku'settle scores' na si utendaji wake? Tukifanya unavyokazania tuta'triviliase' kila kitu. Ninavyofahamu mimi, haihukumiwa ofisi ya waziri mkuu bali waziri mkuu. Ingekuwa hivyo, basi wote wangeombwa kujiuzulu. Tusiendekeza siasa za mchangani. Tusikimbilie kubomoa kabla ya kujenga.
 
kwa huyu rais tuliyenaye you cant rule anything out
 
Sasa utamhukumu kutokana na watu wanaotaka ku'settle scores' na si utendaji wake? Tukifanya unavyokazania tuta'triviliase' kila kitu. Ninavyofahamu mimi, haihukumiwa ofisi ya waziri mkuu bali waziri mkuu. Ingekuwa hivyo, basi wote wangeombwa kujiuzulu. Tusiendekeza siasa za mchangani. Tusikimbilie kubomoa kabla ya kujenga.

Unfortunately kwa wanasiasa tulionao sasa hatuwezi kuwaamini hata kidogo na hili si kosa la watanzania bali ni lao wenyewe. Kama kungekuwa na mwanasiasa mwenye akili then tusingekuwa tunaongelea au tusingekuwa tuanadadisi huyu mheshimiwa
 
Je ni mwadilifu? Ndiyo

Je hajajilimbikizia mali? Ndiyo anamiliki nyumba ya kawaida kabisa Mikocheni

Je hana scandali? Kabisaaa

Je hana nyumba ndogo kila mkoa/wilaya? Hapana

Je Ni Wakurugenzi wapi wa Wilaya na Watendeji wengine yeye aliowapendelea? Hakuna kwani wakati huo yeye hakuwa na nafasi ya kuteua wala kuamua dhidi ya nafasi hizo, alibanwa sana na PM aliyeng'atuka yaali Mamvi

Je kwa mda alivyokuwa waziri- ni amekuwa na mafanikio gani? Ya kawaida

Is he a clean man? Yes
__________________
 
Huyu jamaa amevaa suti kama ki two bit mafiosi, jamani mpelekeni shopping PM mpya atatia aibu.
 
Huyu jamaa amevaa suti kama ki two bit mafiosi, jamani mpelekeni shopping PM mpya atatia aibu.

Haya sasa tumeanza na suti yake! Kweli tunamtaka Chiluba mwingine? Tumeishaanza trivilisation. Bado waliomuona bagamoyo mlingotini!Iko kazi.
 
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Mbunge wa Mpanda Mashariki (CCM), Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya Edward Lowassa aliyejiuzulu nafasi hiyo juzi.

Uteuzi huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa, umewaacha watu wengi midomo wazi kwani waziri mkuu huyo mteule hakuwa miongoni mwa orodha ndefu ya watu waliokuwa wakitajwa kumrithi Lowassa, licha ya gazeti hili na gazeti dada la THISDAY kumtaja.

Katika barua yake jana kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Kikwete alisema kwamba amefanya uteuzi huo kwa kufuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 51 (2) toleo la mwaka 1977.

Wabunge 282 wa Bunge hilo walimpitisha Pinda kwa kura 279, wakati ambapo kura mbili zilimkataa na moja iliharibika. Ni ushindi wa kiwango cha asilimia 98.9.

Kabla ya uteuzi huo, Pinda alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu akishughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), na utendaji wake ulionekana tangu awali kuwaridhisha wengi.

Akizungumza kabla ya kuthibitishwa, Pinda ambaye alisema kwamba yeye ni mtoto wa mkulima tena mtoto wa kwanza, alisema kwamba nafasi hiyo ni kubwa lakini akamhakikishia kwamba angejitahidi kuitekeleza.

Pinda, ambaye ni mwanasheria kitaaluma aliyehitimu shahada Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974, alisema kwamba amekuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Rais Julius Nyerere kwa miaka saba tangu mwaka 1978 na kisha kuendelea na wadhifa huo katika miaka yote 10 ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi kabla ya kuendelea tena kwa miaka mitano katika serikali ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa.

Mwaka 1995 aliwahi kuwania ubunge katika jimbo la Mpanda Mashariki lakini akashindwa katika kura za maoni. Hata hivyo, aliwania tena nafasi hiyo mwaka 2000 ambapo alifanikiwa kushinda na kutwaa tena jimbo hilo katika uchaguzi wa mwaka 2005.

"Mimi si mwanasiasa, lakini katika kipindi nilichokaa na wanasiasa wakongwe, nimeweza kujifunza mambo mengi, na hasa katika wizara hii kupitia kwa Ngwilizi (Hassan), Rais Kikwete (wakati akiwa waziri) pamoja na Lowassa (Edward) ambapo wizara yangu iko chini yake," alisema.

Alisema kwamba atahakikisha kwamba analinda misingi ya katiba na kujenga mshikamano miongoni mwa wabunge kwa maslahi ya Watanzania wote.

"Nitabadilika kimadaraka, lakini kihalisia nitaendelea kuwa Pinda yule yule… Ninachowaahidi ni kwamba, nitahakikisha nalifanya Bunge hili kuwa moja. Yanapokuja masuala ya maslahi ya taifa, Bunge lote liwe moja kama zilivyo nchi za wenzetu kama Israel na hata Marekani," alisema.

Aidha, baada ya kuapishwa, waziri mkuu mpya alisema, atajitahidi kusimamia na kudhibiti dalili zozote za maovu ndani ya serikali.

Pinda alisema kwamba yale yote yaliyotajwa na kupendekezwa na kamati teule ya Bunge kuhusiana na kashfa ya Richomond yanapaswa kufanyiwa kazi kwa msingi wa kuleta mabadiliko kwa maslahi ya taifa.

"Vyombo vya dola vimetajwa. Takukuru, polisi na kadhalika. Haya yote yanapaswa kushughulikiwa na nina hakika yakifanyiwa kazi kwa makini nina hakika tunaweza kufika kule tulikokusudia," alisema.

Aidha, alisema kwamba umoja ndani ya Bunge na serikali ndivyo vitu vitakavyoweza kujibu yale ambayo wananchi wanataka wafanyiwe.

"Hoja siyo vyama vingi, nadhani Bunge la Jamhuri ya Muungano linajitosheleza kwa sababu lina watu makini. Kwa hiyo hoja hapa ni kutekeleza masuala ya msingi kabisa ambayo wananchi wetu wametutuma kwa maslahi ya taifa," aliongeza.

Aliomba wabunge wote kushirikiana na kuheshimiana ili kuweza kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa taifa.

Pinda alihimiza Watanzania wote kushirikiana kufichua maovu ili kujenga taifa lenye maendeleo.

Aliwataka watu kuondoa hisia kwamba kamati teule ilitoa mapendekezo kwa chuki na ubinafsi na kusema kwamba kamati hiyo ilitenda kazi yake kwa ukamilifu, huku akiahidi kwamba hata yeye ataweza kuwajibika ikiwa yatampata kama hayo.

Kuteuliwa kwa Pinda kumekuja kufuatia Rais Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuhusishwa katika ripoti yak amati teule ya Bunge kwamba alihusika katika mkataba wa Richmond na Tanesco.

Waliojiuzulu pamoja na Lowassa ni pamoja na waziri wa zamani wa wizara ya nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha ambaye kwa sasa alikuwa waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na waziri wa sasa nishati na madini Nazir Mustafa Karamagi.

Mawaziri hao wote wametajwa kwamba walishiriki kwa kiasi kikubwa kuiingiza Tanzania kwenye mkataba mbovu wa Tanesco na Richmond, kampuni ya Marekani ambayo ilikuwa imepewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura tangu mwaka 2006.

Hata hivyo, mkataba huo ambao ulihaulishwa kwa kampuni ya Dowans ya kutoka Arabuni, umeleta hasara kubwa kwa taifa ambapo Tanesco sasa imeongeza tarifu za umeme kwa asilimia 21.7 ili kuweza kulipa gharama za milioni 152/- kila siku kwa kampuni hizo za kigeni.

Zitto Kabwe, alipongeza kuteuliwa kwa Mizengo Pinda akisema kwamba ndiye aliyefanikisha mgogoro uliokuwa umejitokeza Kigoma baada ya uchaguzi mkuu kufikia kwenye muafaka wa kuunda halmashauri ya pamoja.

“Kwa hali ilivyotokea, ingekuwa kwenye nchi nyingine, hali ingekuwa ya vurugu, lakini kwa misingi ya katiba, hali imeweza kuwa ya utulivu na Rais akafanya uteuzi wa msaidizi wake kwa kipindi muafaka,” alisema Zitto.

Pinda ataapishwa leo na Rais Jakaya Kikwete saa 5 asubuhi mjini Dodoma.

Wakati huo huo, Spika Sitta jana alitangaza kuwa baraza jipya la mawaziri litatangazwa Jumatatu.

ends
 
Haya sasa tumeanza na suti yake! Kweli tunamtaka Chiluba mwingine? Tumeishaanza trivilisation. Bado waliomuona bagamoyo mlingotini!Iko kazi.

Hakuna swala la trivialization, ulimuona kwenye confirmation speech kaka? Suti na vest with no shirt uliona wapi mazee? .Huyu sio brotherman mpiga disko au muuza sigara, huyu ni Waziri Mkuu na inabidi avae as such.

Unaweza kwenda Paris Club watu wakakupiga bao sababu ya issues za presentation tu, kwa hiyo siyo trivial hata siku moja.Si lazima awe flashy and all that, hatutafuti supermodel vitu vya kawaida vinavyoendana tu, kama jacket shirt and tie, even a jacket with a shirt and no tie au hata suti za kichina il mradi kitu kinachoeleweka, siyo jacket and vest, labda kama anataka kuwa Andre 3000 wa fashion TZ.
 
Mmeanza wana JF,hata hamtoi nafasi ya kuangalia kinachoendelea,saa nyingine ni sisi wenyewe wabongo ndio tunasababisha viongozi wetu wawe wezi. Kulikoni alivyovaa pinda? ni watu wangapi baba zao hapa wanaenda kwenye mikutano ya hadhara walivyovaa utacheka? mbona condoleeza Rice alivyovaa ule mkoti mrefu jana huko afghanstan hamjasema chochote? Kwa maana nyingine kuhoji sana juu ya watu walivyovaa,nyumba wanazoishi n.k ni kuwatuma waanze kuiba maofisini. Ndio tatizo letu bongo,mtu akiwa kwenye ofisi nyeti akatoka na utajiri wa kawaida tu au akawa na maisha ya mtanzania wa kawaida tunamwona fala,eti alizubaa wakati akiingia ofisini ana gari moja akatoka ana mashamba ekari 50,gari 6,nyumba 4 safi,suti kila kukicha na kitambi tunasema fisadi. Hebu tuchunge kauli zetu sometimes. Halafu ukichunguza sana utakuta sisi Afrika ndio huwa tunacomplicate sana mavazi kuliko hata viongozi wa mataifa makubwa duniani,ambao sometimes hata wanatokeza na tshirt in public.
 
Augustoons,

Chiluba aliwahi kununua suti za 1 m USD toka Uswisi!

Pinda anavyovaa tosha kabisa- hii vaa ya mitai ya Ulaya wakati moyni umeficha ufisadi- je yote haya ya nini?

Kama tuna vazi za Kitaifa basi angelivaa- hii ya kuvaa mitai kwenye joto kama Bongo sikubaliani nalo!
 
Hakuna swala la trivialization, ulimuona kwenye confirmation speech kaka? Suti na vest with no shirt uliona wapi mazee? .Huyu sio brotherman mpiga disko au muuza sigara, huyu ni Waziri Mkuu na inabidi avae as such.

Unaweza kwenda Paris Club watu wakakupiga bao sababu ya issues za presentation tu, kwa hiyo siyo trivial hata siku moja.Si lazima awe flashy and all that, hatutafuti supermodel vitu vya kawaida vinavyoendana tu, kama jacket shirt and tie, even a jacket with a shirt and no tie au hata suti za kichina il mradi kitu kinachoeleweka, siyo jacket and vest, labda kama anataka kuwa Andre 3000 wa fashion TZ.

Pundit,

Unabore na mambo yako ya suti. Mnafuatilia hata mambo yasiyo ya maana halafu mnataka tusiwe na mafisadi?

Kama unataka bingwa wa kuvaa si tunaye rais? Unataka kila mtu ashinde kwenye shopping Harrods?

Huyu jamaa inaelekea ni muaminifu au sio mpenda sana utajiri. Hii ni sifa ndogo, kubwa lazima awe creative na kuja na ideas mpya. Hatutaki akina KAWAWA wengine ambao hawaharibu kitu lakini pia hawafanyi lolote la maana.

Binafsi afadhali kuwa na mtu anayekuja na mawazo mapya na yakafeli kuliko mtu aliyekaa kama kisiki bila crfeativity.

Kwenye dunia ya globalization what matters is about ideas, new ways of thinking and creativity.

So longer hatembei uchi mimi sina matatizo kabisa na anavaa nini.
 
Back
Top Bottom