Hakuna aliyemtuma Mary chatanda ni uropokaji wake tu ndio umemponza. Kama kuna mtu kamtuma basi atakua MAKAMBA au TAMBWE HIZA maana akili zao zinafanana. Najua JK anapingana na kauli hiyo ndio maana kamtuma WASSIRA akajikoshe kwa maaskofu MWANZA wakati wa kumsimika Askofu Mkuu mpya wa mwanza. Kwa wale waliokuwepo pale kawekamo- mwanza au waliofuatilia kupitia television wamesikia kauli ya WASSIRA akiwaambia maaskofu waikemee serikali inapoenda kinyume na kuhatarisha umoja wa watanzania na amani ya taifa. Sio kwamba Wassira alitamka maneno hayo bila kujua nini Mary chattanda alisema jana. Kauli hiyo imesemwa makusudi kuwaonesha maaskofu kwamba wanapingana na kauli ya chattanda. CCM wanapaswa kumwajibisha chattanda haraka iwezekanavyo.
Nimesikitika zaidi leo baada ya kusikia kauli ya chattanda kwenye habari ya channel ten sa moja jion. Chattanda anasema maaskofu kumtambua au kutomtambua meya haiwasumbui chochote (haiwaumizi kichwa) kwa kua maaskofu hawana madiwani kama vyama vya siasa. Najua mary chattanda kwa kauli alizozitoa zinaonesha upeo finyu wa uwezo wake wa kufikiri, anawaambia maaskofu waache kuingilia siasa akiamini kwamba kitendo cha wananchi watatu kuuawa bila hatia ni suala la kisiasa. Mary chattanda anashindwa kuelewa kwamba "man is a political animal" kwa sababu anaathiriwa na maamuzi ya kisiasa kaatika nyanja mbalimbali za maisha na kwamba siasa anayoizungumza inapenya katika nyanja hizo za maisha kama vile za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Mary chattanda anatakiwa aelewe kua nyanja zote hizo nilizozitaja zinaathiriwa na maamuzi ya kisiasa kwa namna moja au nyingine. In other words political decisions influence social, economical, and cultural undertakings, as a matter of fact there is no way one can separate religion and politics.
Mary chattanda haoni tabu meya wa Arusha kunyimwa ushirikiano no maaskofu kwa sababu kwa mujibu wake maaskofu hawana madiwani kama vyama vya siasa. Anasahau kwamba mbali na kuhubiri injili maaskofu kupitia makanisa na taasisi zao mbalimbali wanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii kwa ujumla. Huduma kama za shule, hospitali, vituo vya kulelea watoto pamoja na miradi mbalimbali ya makanisa vimekua chachu ya maendeleo ya taifa hili kutokana na serikali pekee kushindwa ku meet demands za watanzania. Leo mary chattanda anasema maaskofu kutomtambua meya is not an issue anawaambia wavue majoho wakafanye siasa kama alivyofanya dr slaa, tena anaongea kwa tambo na nyodo. Huyu mama ana laana na sijui ni muumini wa dini ipi maana hana hofu ya Mungu hata kidogo, I guess she is a pagan. Kwa aliyoyasema ata akiomba msamaha hastahili kupata msamaha wowote. Bahati mbaya zaidi ametoa kauli hiyo kwa niaba la chama (CCM) na chama katika ngazi ya taifa hakijatoa kauli yoyote that means it stands as a party standing.