Who is Mary Chitanda?

Inawezekana dada yako au hata mama yako alishajaribu ndo maana wataka na mimi nikajaribu,hapana! tumetofautiana sana,mi Mwenyenzi Mungu kanipa uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi,zaidi kanipa elimu na kazi nzuri sina sababu ya kujaribu kuwa malaya manake hata kwake sitakuwa na la kujibu safari yangu duniani ikiisha. Sijakuomba ushauri na sijitetei kwakuwa Jamii forums si baba yangu wala mama,wala mume wala Mungu........ni sehemu ambayo niko kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kujifunza,kupokea taarifa na kutoa maoni yangu kwa kile nachofikiri.Wape ushauri wanaotaka,si mimi,nikiomba waweza toa.......

''hilo nalo neno''
 
Neno la Mungu linasema wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu,am not exceptional because of a single post at JF and i will never be.Nimeshasema samahani na hilo pia Mungu ameliona. Tofauti na wewe I hate nobody na Mungu anisaidie,and i think you should seek forgiveness for hating wanadamu ambao wote tuna mapungufu! and you should be fair,kwakuwa yupo aliyenitukana kabla,sikuanza tu kusema hayo hapo juu ila kwa kuwa mimi ni mwanamke,mbele za Mungu tu sawa.


Unajua hata kuomba msamaha ni ujasiri, nafurahi kwa kuelewa hivyo, but leo JF imekosea the above quote u replied is not mine, i hate nobody.
 
kama unakili kwamba uwezo wake ni mdogo unadhani nini kimemfikisha hapo alipo? mbona hatujakusema wewe? kila mmoja anapewa haki yake regardless kwamba ni mama au baba. Ndio sababu anasenwa na makamba pia kwani yeye ni demu pia?!

Hapo highlight, Chupi mkononi, ni maharage ya Mbeya a.k.a soya au siku hizi yapo ya njano maji mara moja!! Gademu, sheeeeeeet.
 
"Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

"Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa,

Alisema kwa mujibu wa sura ya 287 ya kifungu cha 35 1 D wabunge wa viti maalumu wanatokana na idadi ya kura za chama husika, lakini ni wapi wafanye kazi zao ni uamuzi wa mamlaka husika ya chama kilichowateua na kutoa mfano kuwa kwa upande wa CHADEMA kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu.

Fuatilia hilo then tunaweza endelea jadili.

Michelle, ni kweli CHADEMA iliandika barua kutaka ufafanuzi kwa Mwanasheria Mkuu. barua hiyo ilijibiwa kama ulivyosema ILA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai alikataa ushauri huo na kusema mpaka apokee maelekezo kutoka TAMISEMI. Ni mpaka ijumaa iliyopita (baada ya maandamano ya Arusha) barua ikatoka kwamba uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo na wabunge Mh. Grace na Mh. Lucy ni wajumbe halali!! Siku zote walikuwa wamepingwa!!


Kifungu cha sheria hapa chini kinaeleza vizuri kuhusu ujumbe wa baraza la madiwani kwa wabunge wa viti maalumu.

(e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the municipal council.

CHADEMA upatikanaji wa viti maalumu hutokea Kamati Kuu ya Taifa ('an organ of a political party). Mamlaka (Jurisdiction) ya kamati Kuu ya Taifa ni nchi nzima. Hivyo basi Kamati Kuu ya Taifa CHADEMA inaweza kumpangia Mbunge wake wa Viti Maalumu Halmashauri yoyote kulingana na mahitaji ya Chama.

Ukisoma kipengele hicho hakuna mahali popote ukazi 'residence' umetumika kama kigezo cha ujumbe wa Halmashauri kwa wabunge wa viti maalumu. Kwa suala la mary Chitanda CCm Mkoa arusha walikuwa wanatumia 'ukazi' kama kigezo!!

Hata kama wewe sio mwanasheria tafadhali kisome hicho kifungu halafu toa tafsiri yako.

Utaratibu wa CCM ni tofauti na wa CHADEMA. Wao CCM wabunge viti maalumu wanapendekezwa (nomination) na organ za chama chao kwenye Mikoa. Organ ya CCM iliyompitisha Mary Chitanda iko Tanga (sina uhakika ni jumuiya ya wanawake au nini) lakini sio organ iliyopo Arusha. Mbunge wa Viti Maalumu wa Arusha kupitia CCM ni Catherine Magige na yupo.

Huyu ametokea Arusha lakini anaishi Dar sasa kama tukitumia tafsiri ya ukazi ilitakiwa awe Dar na sio Arusha.

Tatizo lilipo ni mapungufu ya sheria i.e sheria kushindwa kuwa wazi kuhusu ujumbe. Tafsiri iliyotolewa si sahihi. Kama Mary Chitanda anaingia kwenye Halmashauri ya Arusha kwa sababu ni mkazi wa Arusha basi si sahihi kwa Mh. Grace na Mh. Lucy kuingia Halmashauri ya Hai kwa sababu si wakazi wa Hai.

Huo ni mkanganyiko wa wazi wazi. Ni kutokana na siasa za maridhiano na kuponya madonda sheria inapindishwa haifuatiliwi!!

Utata hu ungemalizwa kirahisi sana na mahakama endapo tu haya mawili yasingekuwepo (without prejudice and with due respect);

1. Upendeleo (imaprtiality) wa mahakama zetu

2. Kucheleweshwa (delay) kwa maamuzi

Ndio maana CHADEMA wakarudi kwenye Nguvu ya Umma kutaka suluhisho.

Kifungu husika cha sheria (kinachofanana na sheria namba 8 ya 1982

43. Decision of questions as to membership of council
(1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

(a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

(b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

(c) a person claiming to have been a candidate at the election;

(d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

(e) the Attorney-General.

Kwa hiyo Michelle, tatizo ni tafsiri ya sheria na tabia ya watendaji (Attorney General na Mkurugenzi wa Halmashauri) kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa sababu tu wamepokea maelekezo kutoka kwa watu fulani badala yake wanalazimisha mamabo. Kwa nini wasingelipeleka suala hilo mahakamani ili kupatiwa ufumbuzi badala ya kulazimisha uchaguzi? Kulikuwa na haraka gani??

Ni lazima sheria ziheshimiwe na pale ambapo tutaanza kutafsiri sheria ili mradi itusaidie malengo fulani yaliyotokea Arusha yatatokea tena na tena!!
 
Back
Top Bottom