Who is Geor Davie? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who is Geor Davie?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by utemi, Jun 9, 2011.

 1. utemi

  utemi Senior Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
  Nasikia ni Nabii,
  Je, huduma yake ipo wapi?

  [​IMG]

  =============
  ============
   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bongo inaongoza kwa "manabii" pori, na huyo ni mmoja wao!

  =================

  [​IMG]

  ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie' wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako' lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa' iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

  [​IMG]


  Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
  [​IMG]
  Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
  Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.


  [​IMG]

  Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK'.

  "Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona," alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

  [​IMG]

  Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
  "Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?" alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

  [​IMG]
  Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
  "Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud," alisema Fred Mushi.

  [​IMG]

  Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
  [​IMG]


  Bravo Hongera ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie'
   
 3. I

  IRAQW MINING Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni noumer mazee!yupo A city maeneo ya kisongo.
   
 4. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  jamaa msanii kinoma. Nilihudhuria mkutano wake mmoja pale Biafra miaka minne iliyopita, jamaa akaanza kusema eti kila mtu aandike jina la mtu anayehisi amemruga kisha yeye Geordavie atafanya dua itakayomfanya huyo mrozi wako apooze na kuteseka hadi mauti yamchukue.
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale ni mwenyeji wa Singida mi nlianza kumfahamu miaka ya tisini alikuwa tarishi pale world vision, Arusha alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la Siloam Gospel Assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi Uhuru Arusha.

  Kwa kipindi hicho mi nlikuwa mwanafunzi wa primary tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'' ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana ka kuvaa mabagi na kunyoa pushback kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha.

  Si kumsikia tena hadi miaka ya kuanzia tisini na sita hivi alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao ka watano hivi wa kuzugia.

  Kituo hichi kilikuwa majengo karibia na Sacon Opposite na kanisa la KKKT Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha, aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko kisongo mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu ka ''mji wa Daudi'' kwa kweli huduma yake imejaa contrervasial saana maisha yake pia yana utata.

  Means jinsi anavyiobehave pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh.

  Simkubali na hii ni kutokana na matunda yake yaani tabia huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design ka yake ila sijui? Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu.
   
 6. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu hebu eleza zaid kuhusu huduma yake ya sasa ni ki2 gan kina kupa walakini, weng wanao jiita manabii mi huwa siwaelew maana hawahubir wokov bal uponyaj na mafanikio. kakobe namkubali asilimia 100 coz anafundisha kwel ya neno la MUNGU
   
 7. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mkuu uliyosema ni ukweli kabisa, mi nipo Arusha Majengo so jamaa namjua sana, alikataa jina la Kasambale coz wazungu walikuwa wanapata shida kulitamka, sasa hivi hana nguvu sana na kusanyiko lake kwa sasa ni ukiwa mtupu.... hana watu..!!! waliokuwa wana msaidia huduma wametawanyika na kufungu huduma sehemu mbalimba kisa ni jamaa kula wake za watu... kuna jamaa mmoja hapa sakina ni dereva wa tours (jina ninamwifadhi) amechukuliwa mke na huyu Geor Devil... mke wa jamaa alikuwa msaidizi wake.......
   
 8. L

  Losemo Senior Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unawtafuta wa nini hawa mkuu. Hawa wote ni manabii wa siku za mwisho. Don`t west yr time. Shika sna kile ulichonacho asije muovu akakunyang`nya
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Hivi we hujui kwamba VITABU VYOTE viliandika kuhusu ujio wa MANABII WA UONGO? Huyu naye alishaandikwa. Anafuata mpango! Hana jipya! Usiende kupoteza pesa zako bure. Kwani Mungu ana haja gani na pesa zetu ilhali yeye ANAMILIKI KILA KITU DUNIANI? Hivi nyie HAMUELEWI?
   
 10. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kwanza kipindi cha kufundisha neno ni kidogo sana ktk ibada ni ka dk 15 tu, muda mwingi ni miujiza na blah blah, halafu ana injili ya vitisho ka vile usipotoa sadaka biashara yako itafilisika na vitu ka hivyo, na ktk mahubiri yake hujisifu sana na kutumia kauli ka Roho mtakatifu ni mbabe n.k kama unalijua neno ukisikiliza mahubiri yake utaguna mpaka ung'ate ulimi. Mbali na hayo ana kashfa nyingi sana za uzinzi na hadi kuna ndoa amezivunja na ushahidi uko, pia jinsi anavyowatreat wasaidizi ni vituko
   
 11. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Sawa sawa si mke wa yule kijana mtoto wa yule mzee wa kiarusha anayekaa kibanda maziwa sakina. Pia hata watoto wake ambao huwatumia kwenye huduma mh! Hawana ushuhuda kabisa kuna yule mkubwa Niki a.k.a Nisher kulikuwa na post yake ktk jamii photos ka usher wa bongo. Hivi kuhusu wasaidizi wake waliohama na watu na kwenda kufungua huduma zao vp? Kuna mmoja anaitwa Channel yuko kisongo mbele ya Ngurumo kidogo mwezi wa 12 nilikuwa kansani kwake ktk mahubiri yake alidai kuna majambazi na wachawi toka Ngurumo ya Upako walitaka kumuua duh! Dini bana siku hizi ka siasa. Tumwachie Mungu tu, ila tutawatambua kwa matunda yao
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nilishawahi kuona bango lake hapo Arusha la Kutangaza mkutano wake wa injili akijiita MTUKUFU MHESHIMIWA NABII GEORDAVIE!!!!!
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Bukudu ameeleza vema na amekuwa makini ili uongeze na zako....kifupi jamaa ni msanii kwa sana tu na yuko kifedha zaidi ukienda kanisani kwake usiopo angalia utajikuta umetoa sadaka pesa yote uliyoenda nayo.

  Mfano kila msitari ukikugusa unatakiwa ukatoe sadaka kwa kumbia kwenda mbele na kutoa pesa na kushika nguzo, utata mwingine nilio uona masharti yake kama unaenda kanisani kwake hutakiwi kula chochote na mkifika nikuimba mpaka atakapo kuja.

  Mfano umefika saa mbili halafu yeye akaja saa saba na tangu saa mbili ulikuwa unaimba tu na kusimama/kukaa akija ndiyo hivyo tena itambidi uongezee na kukimbia kimbia huku vilio kwa kwenda mbele halafu jaama anaanza kukuombea anakushika kichwa na kukusukuma utaacha kuanguka.

  Kuna siku mimi nilienda lakini nikapiga chai yangu vizuri nikasubili nianguke tuliimba mpaka saa tisa ndiyo tukatoka kanisani nikajiuliza sana kuwa hata huku kuanguka kwa watu mara nyingine siyo mapepo ni njaa tu na uchovu.

  Kingine ulinzi wake sija wahi kuona mtumishi mwingine anae lindwa kama huyu jamaa ana mabaunsa kama zaidi ya 15 wanao valia suti nyeusi au nyeupe na miwani mieusi sijui ni kwasababu alimlamba mke wa Mbunge wa Arusha wa zamani(Mh. Felex Mrema) hivyo ana wasiwasi na maisha yake.
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yapo sana tu pale stand kuu...
   
 15. utemi

  utemi Senior Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mbali na hayo ana kashfa nyingi sana za uzinzi na hadi kuna ndoa amezivunja na ushahidi uko, pia jinsi anavyowatreat wasaidizi ni vituko[/QUOTE]

  Mkuu ebu elezea kidogo kuhusu hili....
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huyo ni mmoja wa wale manabii waliotabiriwa kuwa watatokea nyakati za mwisho.....
   
 17. W

  Wisson Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa nyie mliowai kwenda kwenye izo ibada zake aliwai kuwasomea sadaka alizopata?!! Mimi ni Mkatoliki na kila kanisa ninaloenda Jumapili lazima waseme Jumapili iliyopita sadaka ilikuwa shilingi ngapi.

  Nimeshughudia mara nyingi mapato na matumizi yakisomwa kila mwisho wa mwaka. Waumini wa kawaida wanaongoza halmashauri ya kanisa husika ndo hufanya kazi hii sio mapadre wala watawa wengine.

  Kama hili halitokei kwenye kanisa lako au ilo la geordavie (ngurumo ya upako) ni kwanini mliowai kwenda huko mnakubali kuibiwa? Ni kwamba hamna akili au mna mileha ya KIFISADI?

  Hapa ndo naona umuhimu wa haya makanisa yanayochipuka kila uchao yawe yanafanyiwa "Auditing" otherwise ni uizi na utapeli mtupu.

  Geodarvie alikuwa maarufu sana, nakumbuka dada mmoja mwaka 2006 nilipomaliza tu Chuo na kufika Arusha alinishawishi sana niende ila nikagoma kwenda.

  Baadae niliyoyasikia yanayofanyika huko nilishukuru MUNGU kwa kukataa ule mwaliko. Ukikosa maarifa unaangamia sababu hata kwenye Dini siku hizi majizi na matapeli yamejaaa. Lazima tuwe makini sana jamani
   
 18. utemi

  utemi Senior Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  252508_213815088649455_100000628976775_663505_1350309_n.jpg 149137_140171606032710_132279533488584_188196_2575409_n.jpg

  Mke wa GeorDavie ni yupi katika hawa?
   
 19. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  natumia simu ila nimeona hizo picha mke wake ni huyo waliepiga naye picha ana ka mtandio wa kijani ni mtoto kutoka ukoo wa kina Malewo,
   
 20. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Wazee wa kanisa na wasaidizi wake huchagua yeye mwenyewe, kwani hujui kuwa ni nabii anaona wenye mioyo safi wenye nia ya kumtumikia Mungu? Na amekuwa na kawaida ya kufukuza na kubadilisha wasaidizi na wazee wa kanisa wake mara kwa mara, ndo maana hata akagombana na kina Channel ambao wamefungua makanisa na kuhama na watu wake kibao. Kwa sasa watoto wake ndo wasaidizi wake wakubwa na ndo wanahusika sana
   
Tags:
Loading...