Mkereketwa_Huyu said:Hiki chakula sidhani kama ipo siku nitakuja kukipenda. Yaani kufanya tunda kuwa chakula, hiyo hapana
[mention=Mkereketwa_Huyu]Hiki chakula sidhani kama ipo siku nitakuja kukipenda. Yaani kufanya tunda kuwa chakula, hiyo hapana
Vyakula vingi vyenye asili ya mimea hutokana na TUNDA...
Mathalani,
Vyakula vyote asili ya mkunde kunde (maharage, choroko, kunde n.k)
Vyakula vyote vyenye asili ya nafaka (mahindi, uwele n.k)
Sasa iweje sababu ya kutopenda NDIZI iwe ni kwa kuwa lenyewe ni TUNDA...sidhani kama hiyo ni sababu ya msingi!
CC: Kongosho
Ha ha ha ha, mie mwenyewe sipendi kabisa ndizi za kupika
Huwa naonja wakati nasubiria ugali au wali
Ndizi hazishibishi, hata ule beseni
Hivi mtu unaweza ukawa hukipendi halafu ukawa unakila huku ukisubieia kingine?
Halafu kuonja kwako unaonja Sahani mbili au tatu, huku fact unayoitumia kutokipendea "eti hazishibishi hata ule beseni".
cc: watu8

Hili ndili jiugonjwa langu mkuu... Hapa tu kachumbari na mboga za majani ndo vimekosekana kuukamilisha huu mlo wangu!
Kongosho ni Msukuma best, angalia hata jibu alilokupa hapo juu...hawa watu ni mashine nyingine inapokuja suala la kupeleka pwani...
Kuna wakati kulikwa na mashindano ya kula.."Nani anaweza kula Ugali pasipo Mboga?", basi wakajitokeza washiriki kadhaa lakini fainali wakaingia Msukuma, Mpare na Mmakonde.
Akaanza Mpare, akasema yeye anaweza kula ugali kwa harufu ya samaki...basi wakamuwekea ugali pale na bakuli lenye mchemsho wa samaki, Mpare akaula ugali wote akamaliza....watu wakampigia makofi sanaaaa.
Akafuatia Mmakonde, akasema yeye anaweza kula ugali kwa picha ya samaki...basi ikatafutwa picha ya samaki na Mmakonde akaufuta ugali wote kwa hisia ya picha tu....watu wakampigia makofi sanaaaa zaidi ya Mpare.
Mwisho ikawa zamu ya Msukuma....jamaa alipoulizwa utakulaje ugali wako, Msukuma kwa lafudhi ya Kisukuma akasema, "mimi naomba mniletee UGALI MKUBWA na pembeni mniwekee UGALI MDOGO"...Msukuma akala sahani zote mbili, ule UGALI MDOGO ndio akaufanya kama mboga....
Nadhani unaweza kujua ni nani aliyeshinda hapo....

Mmh, unanifahamu?
Umenitisha, umejuaje napenda pilipili?
Mkuu ndizi ni zaidi ya tunda. Personally nikila ndizi mbivu au mbichi sioni kama vile nakula tunda. Suala kama ndizi ni tunda tuu au ni zaidi ya tunda limeshafika mpaka mahakamani.
Tafuta na uisome kesi moja mashuhuri sana ya United Brands vs European Commission. United Brands walikuwa ni major suppliers wa ndizi kwenye Umoja wa Ulaya. Walikuwa wana-import ndizi mbichi na mbivu.
Kwenye kesi hiyo, mahakama ilikuwa inaamua, pamoja na mambo mengine, soko la ndizi (relevant product market) in the context of competition law.
United Brands walidai kuwa soko la ndizi limejikita tuu kwenye matunda. European Commission wakadai kuwa ndizi ni zaidi ya tunda na kwamba the relevant product market siyo matunda bali ni ndizi.
Mahakama iliamua kuwa soko la ndizi ni tofauti na soka la matunda. Mahakama ilisema zao la ndizi lina special attributes kama mwonekano, taste, ulaini na kutokuwa na mbegu.
Mahakama iliongeza kuwa zao la ndizi ni muhimu sana kwa watu kama watoto, wazee na wagonjwa. Zaidi ndizi hazizalishiwi kwa msimu kama matunda ambayo yanapanda na kushuka bei kulingana na msimu wao.
Hii kesi inaonyesha tofauti kubwa iliyopo kati ya ndizi na matunda. I am sure hata wataalamu wa afya na lishe (achilia mbali Wahaya na Wachaga) watakuambia kuwa ndizi ni zaidi ya tunda. Usitake kuniambia hii ni miti ya matunda.
ugali
wanayakanda baada ya kutoa mikono huku, lazima u-enjoy tuKuna maandazi ya Kizanzibar hayo...sijui huwa wanayakanda na tui la nazi...ni matamu balaah!!