what is it? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

what is it?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nova Kambota, Sep 20, 2010.

 1. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]WATANZANIA UPINZANI SI KUPINGA NI KUTOA MAWAZO MBADALA
  Inapofikia wakati watu wanapotoshwa kijinga jinga tu kuna hatari
  taifa likaangamia au kutoweka kabisa. Kwa jinsi vyama vya upinzani
  vilivyo Tanzania nachelea kusema kuwa maana ya upinzani haijaeleweka
  hata kidogo na kwenye makala hii nitaweka wazi ili nieleweke vizuri
  siwezi kuendelea kukaa kimya ilihali uwezo wa kuielimisha jamii ninao
  kwa maana hata mwanaharakati Martin Luther King Jr anasema kuwa wale
  wenye uwezo wa kuongoza wanapokaa kimya kwenye jamii sio tu kuna
  hatari ya kuongozwa na wajinga ,King anasema hata mawe yatatawala ,
  binafsi sioni sababu kwanini nifumbie macho propaganda zinazoendeshwa
  na vyama vya upinzani ambazo kimsingi hazina tija kwa Tanzania ya leo
  wala ya kesho, sasa naomba nizame kwenye mada yenyewe nayotaka
  kuidadavua na kimsingi nitangulie kusema kuwa katika uchambuzi wangu
  huu nitajitahidi kutoa ufafanuzi wangu kwa misingi ya hoja ili
  nikibidi kujibiwa nijibiwe pia kwa misingi ya hoja na sio hoja bali
  hoja zenye mantiki na mashiko pia.
  Upinzani hauna maana nyingine ila kuharakisha maendeleo ya wananchi,
  hata leo hii ukienda kwenye za magharibi vyama vya upinzani vimekuwa
  mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo iwe kwa
  kuihimiza serikali au kushiriki moja kwa moja katika kusaidia wananchi
  kujiletea maendeleo sasa hii ni tofauti na kwetu ambapo vyama vya
  upinzani vimekuwa mstari wa mbele kuongelea umaskini wa watu pasipo
  kusaidia watu hao kujiletea maendeleo, hapa kidogo inashangaza kuona
  kuwa kiu ya watu ni maendeleo sio kuambiwa wao ni maskini kwa kiwango
  gani lakini cha ajabu vyama vya upinzani hawalijui ili wao wanadhani
  kazi yao ni kuwaminisha watanzania kuwa ni maskini sana kuliko watu
  wote Duniani na wakitaka kuwa na maendeleo kama Marekani basi ni
  kuing’oa madarakani CCM huku wakishindwa kujadili kisayansi juu ya
  tofauti kubwa iliyopo baina ya Tanzania na Marekani kwa maana Tanzania
  ina miaka 49 ya uhuru marekani ina miaka 250 ya uhuru, usawa uko wapi
  hapa?
  Upinzani ni lazima kuisaidia seikali kutimiza vipaumbele vya taifa,
  nakumbuka falsafa ya rais wa awamu ya tatu wa Tanzani mzee Benjamin
  Mkapa aliyepata kusema kuwa, katika maisha ni muhimu kuwa na
  vipaumbele lakini ukikosa kutambua kipaumbele cha vipaumbele hakika
  wewe ni mjinga , hapa Mzee Mkapa anatufundisha kuwa katika maisha ni
  lazima kuwa na vipaumbele kwa mantiki hiyo kwenye uwanja wa siasa za
  Tanzania ni lazima kama taifa tuwe na vipaumbele ambavyo vitaungwa
  mkono na watanzania wote licha ya tofauti zao za kisiasa . Mfano mzuri
  ni swala la elimu , hili si jambo la kuendeshwa kisiasa hata kidogo,
  si jambo la kufanywa mtaji wa kisiasa kabisa, haiingii akilini kuona
  kuwa wakati serikali ya CCM imejenga shule za kata vyama vya upinzani
  vinapinga tu bila kutoa hoja za msingi sababu inayoimbwa kila uchao
  ni moja tu nayo ni hazina maana shule hizo hazifai kabisa. Sasa hapa
  kuna mambo ya kujiuliza, unawezaje kuitwa mume bila kuoa? Au unawezaje
  kuwa na shule bora bila kuwa na shule kwanza? Au tuseme unawezaje
  kuwa na nyumba bila msingi kwanza?, hapa kuna hatari kuwa vyama vya
  upinzani Tanzania havijui vipaumbele vya kitaifa ndio maana wanataka
  kutatua matatizo ya kielimu kwa mbinu za kisiasa(they seem to solve
  academic problems on the basis of political techniques) kwamba sasa
  badala ya kujadili jinsi gani ya kuboresha shule za kata ili ziwe na
  ubora sasa shule za kata zinataka kufanywa ndio sababu hasa ya
  kuiondoa CCM madarakani, hata rais Kikwete alipata kunena kuwa
  tusherehekee tofauti zetu lakini tubaki wamoja(let’s celebrate our
  differences but keep our unity) hapa nacholenga kukisema hapa ni kuwa
  lazima tuwe wamoja kwanza tofauti baadae(unity in diversity) na sio
  tofauti kwanza umoja baadae(diversity in unity), hivyo kwa mantiki ya
  kawaida nilitegemea hoja za wapinzani kuhusu shule za kata zilenge
  namna ya kuboresha shule hizo na sio wimbo wa hazina maana ambao
  tumeanza kuuchoka.
  Ni lazima kuunga mkono mambo ya muhimu , upinzani wenye tija ni ule
  unaounga mkono serikali kwenye mambo ya muhimu ambayo hayahitaji
  mijadala ya kisiasa ila yanahitaji utekelezaji wa wananchi wote licha
  ya tofauti zao kisiasa mfano swala la kilimo kwanza halihitaji
  mijadala ya kisiasa ila utekelezaji, hapa nategemea upinzani wenye
  tija kuwahimiza watanzania kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo na
  sio kupinga pinga tu bila hoja , kimsingi vyama vya upinzani vinapaswa
  kujua kuwa sio kila linaloasisiwa na chama tawala ni lazima lipingwe
  huu ni ujinga mambo mengine yanafaa kuungwa mkono bila kuangalia
  chama gani kimeliasisi jambo hilo, cha msingi kinachopaswa kuangalia
  je jambo hilo lina tija kwa taifa?
  Popularism inajengwa kwa hoja sio propaganda, hili ni jambo lingine
  ambalo ni muhimu vyama vya upinzani vikalifanyia kazi kwamba
  popularism(umaarufu kwa wananchi) hauletwi kwa propaganda bali hoja
  ambazo zinawagusa wananchi, hapa kuna la kujifunza kutoka kwa Obama wa
  Marekani ambaye umaarufu wake haukuletwa kwa propaganda bali hoja kwa
  maana hatari ya propaganda huwa zinaimbwa redioni na majukwaani na
  zinakinaisha lakini hoja huwa zinaishi mioyoni mwa watu na kukaa
  vichwani mwao. Mara nyingin upinzani wa Tanzania umejikita katika
  propaganda na sio hoja, nitoe angalizo kuwa Intelligent people discuss
  ideas(wenye akili zaidi hujadili hoja), Normal people discuss
  events(wenye akili za kawaida wanajadili matukio) and stupid people
  discuss people(na wajinga hujadili kuhusu watu), sasa kwa kawaida
  propaganga hujikita kwenye kuwajadili watu kila uchao huu kwa maana
  nyingine ni ujinga, upinzani wa Tanzania unapaswa kulijua hili.
  Upinzani sio upingaji, bila shaka hili ndicho ambacho kinanifanya
  niamini kuwa somo la upinzani halijaeleweka Tanzania kwa maana vyama
  vya upinzani vimejigeuza majukwaa ya kupinga serikali yachama tawala,
  huku ni kukosa maono kwa maana mpinzani sio lazima kupinga kila mda
  wakati mwingine ni busara Zaidi kuunga mkono , kutokana na hulka hii
  ya kupinga vyama vya upinzani vimekuwa havipo tayari kukubali hata
  matokeo ya uchaguzi , kila baada ya uchaguzi maneno CCM wameiba kura
  limekuwa ni kiitikio cha wimbo maarufu wa hakuna uwanja sawa wa
  kisiasa nchini. Vyama vya upinzani vinapaswa kuwa vyama mbadala na
  kutoa changamoto sasa ni wakati wa kuamka na kuwa vyama vya upinzani
  hai na sio kuendelea kuwa vyama vya upingaji.
  Naomba nimalizie makala yangu kwa shairi langu fupi nililotunga
  mwenyewe ili vyama vya upinzani waweze kukumbuka na kuzingatia haya
  niliyojadili kwa maana hata wanasaikolojia mabingwa duniani wanaamini
  mashairi ni moja ya njia kuu za kufanya mtu akumbuke kitu fulani,
  shairi langu ni kama ifuatavyo;
  UPINZANI SI UPINGAJI
  1. Inafaa kutambua , maana ya upinzani
  Yafaa kuzingatia, kuyaweka akilini
  Haifai kukandia, walio madarakani
  Kiu ya watu maendeleo, malumbano hawataki.

  2. Uzalendo si kelele, ni kupenda nchi yako
  Changamoto ziko tele, onyesha mchango wako
  Taifa lisonge mbele, kutoka hapa tuliko
  Upinzani sio kupinga, inafaa kutambua.

  Makala hii imeandikwa na Novatus Kambota wa Vijana Zaidi na Kuhaririwa
  na Gama , mwandishi wa makala hii anapatikana kwa anwani ya barua
  pepe; novakambota@gmail.com
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana-JF: have you noticed? We are being spammed!!!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Yeah, we are under spam attack, God help us!!!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  huwezi kuwa mpinzani kama hupingi, na huwezi kuwa mpinzani kama unakubali tu! Ukitaka ukubali tu bila kupinga unatakiwa uingie kwenye chama tawala. Maana ya upinzani ni kuonesha kasoro za watawala walioko madarakani siyo sifa zao (hilo ni jukumu lao na la mashabiki wao). Kuwa mpinzani siyo kuisaidia "serikali" bali kuionesha kuwa haifai na haiwezi. Mpinzani anayesifia serikali na chama tawala ili aonekane kuwa yuko fair bado hajakomaa katika upinzani kwani atajikuta anabakia kuwa "shabiki". Katika Tanzania tuna mifano kadhaa ya wapinzani waliodhania wakiisifia CCM basi CCM itawaonea huruma. Hivi kule kwa Cheyo pamoja na sifa zake zote kwa JK je wamemuacha awe mgombea pekee, vipi kule Vunjo kwa Mrema?

  Mpinzani asiye mpinzani
  Ni rubani asiye rubani
  Ni nani atamuamini
  Kushika ndege angani?
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  tofauti na kwetu ambapo vyama vya
  upinzani vimekuwa mstari wa mbele kuongelea umaskini wa watu pasipo
  kusaidia watu hao kujiletea maendeleo, hapa kidogo inashangaza kuona
  kuwa kiu ya watu ni maendeleo sio kuambiwa wao ni maskini kwa kiwango

  Nova naona siku hizi umeanza kujitahidi kuibua hoja lakini hazina nguvu kabisa. Mpinzani lazima atoe hoja za kumpinga mpinzani wake kama Mwanakijiji alivyoeleza. Kwa mantiki ya kawaida unaendelea kumwita mtu mpinzani halafu unataka wacheze timu moja, watazamaji watazame mchezo au vioja. Waache wapinzani wafanye kazi yao, na wewe jenga hoja ya kuwapinga katika hoja zao lakini si katika ujumla wa nafasi yao kama wapinzani
   
 6. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Bila shaka sijaeleweka kabisa.................nachotaka kukisema hapa upinzani ni zaidi ya kupinga.......upinzani ni kutoa hoja mbadala pia sio tu kulaumu kama serikali imeshindwa hili...........tupe mbadala sio kutuambia kushindwa tu kwa maana tunajua iliposhindwa na kwa mantiki ya kwawaida juhudi zinahitajika kurekebisha sio kujadili kushindwa kwa maana udhaifu si kuanguka bali ni kushindwa kuinuka baada ya kuanguka(weakness is not to fall but fail to stand after falling)...............naomba niage wanajukwaa tutaonana kesho sasa hivi naenda kuendeleza harakati mtaani.
   
 7. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ulikuwa unabipu sio?
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280

  FROM PENPALS!
  Posted: 16/08/2009, 12:21
  Iam a boy aged 20 years living in Arusha Tanzania East Africa iam looking for a girl of any age the one who will love the one to care me. For more about me visit www.novadream.blog.com and my phone number is +255766730256 talk to me and welcome to mt kilimanjaro the highest peak in Africa.
  Posted By: nova kambota
  Location: United Republic of Tanzania
  Email: novakambota@gmail.com
  KAKA VIPI HARAKATI ZAKO ZA KUTAFUTA A GIRL OF ANY AGE ULIFANIKIWA?


   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nini maana ya upinzani kwa lugha nyepesi!?
   
 11. S

  Safre JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Da anatafuta dem tena?
   
 12. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Naona hoja imehama bwana imekuwa sio maana ya upinzani tena ni kuhusu mimi kutafuta girl................aah...........binafsi sidhani kama hilo lililoibuliwa litatusaidia kuelewa maana ya upinzani hebu tujadili mambo ya msingi..............nimechambua kwa hoja inabidi nijibiwe kwa hoja sio mzahamzaha .........tuchambue mambo yenye tija kwa taifa ......tujadili kwa mantiki mzaha sio mda wake huu.............kama umeshindwa mada haijaeleweka ni heri kaa pembeni kwa maana kujiuzulu sio udhaifu tu wakati mwingine ni ujasiri kuyaacha yapite(resigning does not only mean you are weak , sometimes it means you are strong enough to let it go)
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ametoa mchango wake lakini naona kama anaota hasira,na jazba,kuona chama tawala ccm kimeshindwa kufanya yale walotarajia na sasa hawana la kujitetea ila nao wameanza kulaumu.
  Hoja hapa ni UPINZANI.
  Je,bila vyama vya Upinzania bungeni haya yote ya wizi wa mali ya umma EPA,TANGOLD,MEREMETA,RICHMONDULI,hatungeyajua.Lazima ukubali huu ukweli,kwa maana hiyo ninakuhakikishia bila UPINZANI bungeni hakuna utawala/uongozi bora,siasa safi,
  Jaribu kufikiria kwa kina,sababu kuu ya kuanzishwa kwa vyama vya upinzani duniani,wanajamiiForum wanajua sababu za kuanzishwa kwa vyama vya upinzani ndio maana wako makini katika kuchangia mijadala mbalimbali inayohusu siasa na uchumi nk nk.
  Nadhani kuna kitu kinakuuma kuona chama kinashindwa kumtetea mlalahoi wa Tanzania na kukumbatia matajiri kikidai ndio wanaokibeba ni kweli lakini tunatakiwa kutambua kuwa sisi tumeshachokwa na watanzania hata pale tunapotoa ahadi tunaonekana ni za kimagumashi za kuchakachua tuu kama walivyotuchakachua kwenye kura za maoni.
   
 14. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Ndugu technician hilo neno lako sisi sijui wewe na nani? na katika lipi? mimi sio mwanasiasa ila ni mwanaharakati..............hebu jadili hoja acha shutuma na ushabiki bwana kaka.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
   
 16. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Mzee mwanakijiji kwa busara zako natatizika kidogo kama kweli una fahamu what we mean by arguement? kwa maana inapasa ujikite kwenye hoja za msingi zilizomo ndani ya makala yangu pangua hoja bwana sio unatumia technicality kutaka kung'ang'aniza hoja yako ikubalike mi naona inafaa zaidi kutumia logic kuliko kukimbilie hiyo nukuu niliyokupa.............kwa maana unaonekana kuanza kuishiwa hoja sasa.
   
 17. M

  Mutu JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe unajiona una hoja kweli?Simple what is opposition part?
  The role of an opposition party is to oppose the government by criticizing government policies, suggesting alternatives and keeping the public informed about issues relating to government administration.
  Always the main role is what the name of organ go by which is oppose the government.

  Tatizo ulilonalo ni kuwa unataka kusema upizani iwe inasifia serikali no way no how!
  Ukirudi kwenye maswala ya kushauri wapinzani wanashauri kuna mawaziri vivuli wakilawizara bungeni na ktk kila bajeti huwa wanatoa critical contribution ,altarnatives.Dont tell me husikilizi bunge.Ila kinachokuuma ww ni pale wanapotekeleza jukumu lao kuu kupinga serikali.

  Unajiita mwana harakati sio mwanasiasi while you play politics and side with political part.
  Fanya uchunguzi akinifu kabla ya kuandika ,angalia tafsiri ya key words unazotumia .Kinachonishangaza habari zako unazoandika ati una mpaka editor wakati zinakuwa hoja zisizo kuwa na mshiko au ndio vipofu wawili .Ok nikiongea sana utasema naruka hoja yako ngoja niku anzishe thread yako.
   
 18. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Naomba kidogo nitunge shairi langu kwa lugha ya kiingereza ili nieleweke vizuri kwa maana naona watu wanashindwa kuelewa maana sahihi ya upinzani;

  OPPOSITION
  It takes bright people, to know opposition
  not violents, indeed not insults
  it is alternative way, of promoting development
  opposition is democracy and not lamentations.
   
 19. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Mimi na hoja tu ila zipo kwenye makala yangu ............narudia tena upinzani ni zaidi ya kulalamika.............upinzani wa kweli unajali vipaumbele vya taifa sio kuendesha propaganda kila uchao.............bwana Mutu hebu jaribu kuchambua hoja zangu sio kuniuliza iwapo na hoja au la? Mimi hoja ninazo za kutosha tu lakini hebu chambua hoja zilizopo kwenye makala yangu kaka.
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bado unakua wewe,
   
Loading...