Tatizo lako kubwa unaonekana unataka ukiweka mada hapa basi kila mtu akubaliane nawe na asikupinge,ndio maana unajiaminisha kua mtu akikupinga au hata kutumia lugha ya kuudhi eti anakua amekuja na ID nyingine! sidhani kama una ushahidi na hilo bali umeamua tu kujiaminisha ili kujifariji,huwezi kukubalika na kila member na kwa kila mada tambua hilo kwanza,
Halafu inaonekana kuna sehemu umepewa ukweli na dawa imekuingia kisawa sawa ndio maana umeamua kuja na kuanzisha hii thd kama utetezi wako,kujisafisha na kutafuta huruma za watu "sympathy" huwezi kukubalika kwa kila thd na kila member tambua hilo!
Halafu mtu akipingana na wewe siku zote hua nakuona unakimbilia kuleta screen shot ya page ya huyo member anayepingana nawe na hua unamdhihaki kua eti ni member mgeni na kajiunga jf hivi karibuni tu! ni nani aliyekuaminisha kua akili ya mtu hua inapimwa kwa kuangaliwa ni lini kajiunga na jf? vipi kuhusu wale ambao sio member wa jf kabisa?