Wakazi wa kawe? Mbona swali linaeleweka?
Tuhabarisheni mazuri ya mh. Mdee jimboni kwake?
Huu siyo wakati wa ku-review nini wabunge wamefanya kwenye majimbo yao bali ni wakati wa kusimamia serikali ya sisiemu imefanya nini!!!Ok?
Wakazi wa kawe? Mbona swali linaeleweka?
Tuhabarisheni mazuri ya mh. Mdee jimboni kwake?
Nothing apart from collecting a huge MP's payout! No water services at Bunju B (mradi 20,000), even a response or a follow up on the matter, she has forgotten why we chose her, a typical TZ MP, forgettenng their responsibilities, what a mess, I fear and shudder for the rest of the opposition IF they come into power, "changa la macho wakongwe"!
Tutolee mfano wa mbunge CCM wa Dar ambaye ni mfano wa kuigwa. Tuelezee vizuri amefanya nini kwa watu wake.
Mimi sijaribu ku-benchmark Performance ya Halima Mdee na wabunge wa CCM; kwanza naona hiyo ni sign mapema ya udhaifu... hauwezi kusema na kusimama jukwaani na kusema kwamba wabunge wa CCM hawafai halafu ukija kuulizwa umefanya nini unaanza kuuliza hao amabao hawafai wamefanya nini.... Wabunge wanaosema wako tofauti na wataleta mabadiliko makubwa lazima waweke Benchmark yao juu zaidi.... hata ukiwa shuleni hauwezi kupata "D" halafu ukasema lakini wenzangu wamepata "F"; sisi tunataka Changes za ukweli natunataka watu wa "A"...... Nimeshasema mimi sina ushabiki wa ki-chama I am merely an innocent observer..... siko upande wa CCM na siko CDM niko upande wa Maendeleo... Kwa mchango wake bungeni juu ya Maslahi ya kitaifa kwa ujumla mimi sina tatizo na Mheshimiwa Mdee, lakini kwa wapiga kura wa Kawe walio mchagua bado naona hajawafanyia lolote la kumsifia....
Non-emotional and Politically unbiased answers only please......
Jamani mimi nauliza what has she done... not what she speaks in parliament.... if ubunge is all about speaking tuu... then we can all be there..... WHAt HAS SHE DONE FOR KAWE AND ItS PEOPLE??????????????
Unataka amtetee Rama aliyemtesa dr ulimboka?
amemtetea msanii lulu hana makosa ya mauaji.. thats the only +ve thing she had done
Sitaki mhesmiwa atumia fedha zake kugharamia maendeleo kwenye Jimbo lake... Mchango wake uwe wa uwezo wake, ushawishi wake na ubunifu wake, usimamiaji wake wa kutatua matatizo Jimboni kwake, ndio hili nina shaka nalo.... kama kweli alikua anawasimamia kidedea hawo waliopewa kazi kutekeleza kupata ufumbuzi wa matatizo Kawe, mbona tunashindwa leo kutaja hata fanikio mmoja; Ameshauri nini na kusimamia nini jimboni kwake kwa matatizo Kawe na kufanikiwa kufikisha utekelezaji hadi mwisho au kuleta ubunifu mbadala au kuwashawishi wananchi au taasisi ambazo sio za kiserekali wa jiunge kutatua kero sugu za Kawe....
tunataka viongozi wanao-Stand out kwenye jimbo...... who go the extra mile kwa ajili ya majimbo yao..... hakuna evidence kwa kuangalia mafanikio jimboni kwake kwamba amefanya chochote cha ziada....
Nimekuwekea michango yake bungeni. Ndilo jukumu lake kuifuatilia serikali. Kama vitu havijatekelezwa inathibitisha jinsi serikali isivyo makini.
Toa mfano wa hao viongozi wanao stand out kwenye jimbo na wamefanya nini. Mahanga? Mtemvu? Zungu?
Wewe ulitaka afanye nini? Toa practical suggestions.
Non-emotional and Politically unbiased answers only please......
Jamani mimi nauliza what has she done... not what she speaks in parliament.... if ubunge is all about speaking tuu... then we can all be there..... WHAt HAS SHE DONE FOR KAWE AND ItS PEOPLE??????????????
Kwa masikitiko makubwa Mh. Halima Mdee ukiwa mbunge wa jimbo la kawe ulitokea kuwa tumaini jipya kwa wakazi wa jimbo hilo. Kwani mtangulizi wako Ritha Mlaki alishindwa kutekeleza hata kiduchu kile kinachowakera wakazi wa jimbo la kawe na hasa maeneo ya makongo juu. Eneo hilo lina kero ya muda mrefu iliyosababisha makongo kama sio sehemu ya wilaya ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam. Hapa nitataja kero kuu mbili ambazo hadi niandikapo bandiko hilo nashindwa kuelewa tatizo liko wapi waheshimiwa nyie kushindwa kupata utatuzi.
1. Barabara. Ukianzia njia panda ya Chuo cha Ardhi hadi makongo mwisho na baadae kuendelea goba kutokea mbezi samaki hii barabara ni mbaya mbaya haina jinsi ya kuelezea. Imefikia mahali wakazi wa makongo juu wamechukulia kuwa sehemu ya maisha yao kila ifikapo saa 12 jioni na kuendelea kupanda dala dala kwa bei ya kuanzia sh. 500 kwa umbali usiozidi kilomita 5. Kinachoumiza hata huo usafiri wenyewe nao licha ya kuwa nauli yake iko juu bado haupatikani angaalau fadhila za madereva wa mabasi kutoka mwenge kwenda bagamoyo ndio zinasaidia vinginevyo sijui hali ingekuwaje..
2. Wakazi wa makongo juu tulishasahau hadithi ya kupata maji ya bomba. Mwaka 2009 kulifanyika uwekaji wa mtandao wa mabomba ya maji karibu eneo lote la makongo juu. Mabomba haya maarufu kama mabomba ya "mchina" tangu yalipowekwa na hiyo kampuni ya kichina mwaka huo hadi leo hayajawahi kutoa maji hata yale ya majaribio...Halima Mdee ulikuwa kuomba kura zetu kwa mbwembwe nyingi kuwa kilichomshinda Mlaki wewe utakimaliza..Lakini wakati tukiingia mwaka wa 2 tangu kufanyika uchaguzi mkuu 2010 hakuna hata dalili kuwa kuna kitakachofanyika....Mh..Halima Mdee kila nikikuangalia kupitia runinga ukiwa mle mjengoni napata hasira kuwa nilipoteza muda na kura yangu na sasa imani yangu inapotea kwako. Sina jinsi ya kuelezea hasira zangu kwako.
Mtu anaweza kusema kuwa tukikutegemea wewe peke yako utatue kero zetu ni uvivu wa kufikiri lakini hata sisi wananchi tulikuwa tayari kuchangia nguvu zetu kutatua tatizo la barabara...lakini wapi...wapi...bure tu...Nafikiria kusimama na wewe kwenye uchaguzi 2015 kupambana na wewe. Umekuwa mzuri wa kupiga kelele huko mjengoni lakini unasahau kuwa sisi tulikupa kura zetu ili utuongoze kutatua kero zetu na si vinginevyo..Naomba pindi utakaposoma thread hii jiulize moyoni mwako hivi unawatendea haki wapiga kura wa makongo????