What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya yametufanya tusahau majukumu halisi ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.

Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi (legislative), badala yake wanajitwika majukumu ya serikali (excecutive). Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.

Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.

Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.

Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:

Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.

Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.

Wakati mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.

Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.

Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.

Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.

Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.

Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.

Richard Lucas
 
Mdee amefanya mengi. Kwa uchache

1. Ametuwakilisha wana kawe bungeni katika kutetea na kuibana serikali katika mipango yake kwa wananchi na hususani kawe. Jambo ambalo ndo jukumu lake la msingi kwama mbuge.
2. Amelia na amepambania uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi zilizotengwa kwa matumizi ya jamii na kubatilishwa kwa kupewa watz wachache wenye mihela
3. Amehamasisha na kuamsha hari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na vijana wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.
4. Ameshiriki katika shughuli mbali mbali za wananchi ikiwmo unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama kawe
5. Ameshiiriki kwa nguvu zote katika katika majukumu na harakati za chama kama mbunge wa chama.

Hakuna aliekua anaweka checklist ya kila anachokifanya, ila jibu la ujumla linaweza patikana kwa kuangalia imani na matumaini walionayo wana wa KAWE juu yake maana miaka 3 angekua hafanyi lolote walisha mchoka kama watu walivyoyachoka magamba na Vasco Dagama wenu.

Naukumbuka usemi wa mzee Malecella, wa embe liliowiva likiwa mtini."Halima ni embe lililowiva likiwa mtini, kila mpita njia analitamani na kulirushia mawe".
 
Wengine tumsaidie kwa yale ambayo yamekwama:
-Migogoro ya ardhi imekua na kupanuka sana kule Madale, Mbopo, Mivumoni;
-Matanki makubwa kabisa ya maji ya DAWASCO yako Makongo. Lakini Makongo kwenyewe maji ni shida;
-Madawati, madarasa, maabara kwa shule za sekondari, walimu bado ni tatizo;
-Usafiri kituo cha Mwenge hasa nyakati za "peak hours" ni tatizo kubwa;
-Kituo cha basi cha Mwenge kimeelemewa na WaMachinga. Tunahitaji Machinga Complex maeneo yale;
-Ajira kwa vijana wenzake ni tatizo kubwa JImboni Kawe;
-Wilaya ya Kinondoni yenye majimbo matatu ya uchaguzi inahitajika kugawanywa katika Manispaa mbili;
-Vituo vya Polisi, mahakama za mwanzo, viko hoi kimiundombinu;
Vinginevyo hongera Halima Mdee. Kura yangu unayo tena 2015. Unasikilizwa kote.
 
Jiulize wewe mwenyewe kakufanyia nini. Usikuta hata hukai kawe ndo maana unauliza kwani wanakawe wako kimya maana wanajua kawafanyia nini. Na unauliza kwetu ili iweje? kamwulize Pinda , anna makinda na wengine huko bungeni watakupa jibu
 
hayo baadae kwa sasa naomba kujua hili la Mdee na alichofanya ndani ya miaka hii ya ubunge wake... lasivyo naye basi ni wale wale.... blah blah nyingi lakini no real change kwa wananchi.... jazba nyingi lakini no real change....

Kwa hiyo wewe unajua alichofanya ni blah blah nyingi lakini ahakuna alichofanya? Hebu tuambie matatizo ya watu wa Kawe ni yapi na yeye wakati wa Kampeni aliahidi angewafanyia nini kuyatatua na mpaka sasa amefanya nini au hajafanya nini? (Katika Bunge lililokwisha ameuliza maswali 6, Maswali ya nyongeza 15 na michango 60: Source Parliament Website 2012)
 
Ametembelea shule zote za msingi na sekondari akachukua data za mahitaji yote muhimu kupeleka manispaa. Alianzisha mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi. Ametembelea kata zote za jimbo lake. Ameshiriki kampeni za bomoa bomoa ufukweni. Tanganyika Packers anafuatilia. Viwanda na mahoteli yote ya jimboni amekusanya data ili walipe kodi.
Ambayo hajafanya kikamilifu ni kampeni ya usafi hasa maji machafu ya mto mlalakua. kampeni ya vituo vya afya na polisi sijui amefikia wapi. Hata ulinzi shirikishi anapswa kuhamasisha kwani watu wanavamiwa majumbani kwao mchana na usiku hadi wengine kuuawa
 
Kwakweli wabunge wetu wanakosa kitu kimoja cha muhimu nionavyo mimi.
kuna mdau hapo juu amegusia swala la community mobilization.
wote tunafahamu serikali yetu ni slow au inashindwa for whatever reasons kutimiza wajibu wake.
however huku mitaani kwetu, there are many other things tunaweza kufanya bila msaada wa serikali and sometimes bila hata matumizi ya pesa.
sasa basi tungekuwa na wabunge wajanja hii ni avenue wangejitadi to explore na kujibebea maujiko na pia kufanikisha baadhi ya ahadi.
kwa mfano, swala la usafi linaweza kufanyika kwa mtindo huu. na haya mambo yapo interconnected, kwa mfano eneo lenu likiwa safi na kusifika mji mzima, kuna uwezekano mzuri sana mkapandisha thamani ya eneo and as a result watu wanaomiliki properties kufaidika.
its about time jamani watanzania tubadilike na tusababishe maendeleo yetu sisi wenyewe. tukiweza kufanikisha baadhi ya mambo sis wenyewe hata serikali itaona aibu na pia tutakuwa tumejitofautisha sis na wao, badala ya kuishia kulalamika.
 
Mbunge wetu Halima Mdee ni mtoro jimboni kwani mara baada ya kumalizika kikao cha bunge la bajeti, hajaonekana jimboni hata ofisi yake pale Kinondoni wilayani, muda wote imefungwa.

Tunashangaa akiwa bungeni ni hodari kuuza sura katika TV huku akiomba miongozo isiyo na tija kwa wapiga kura wake.

Yafuatayo ni matukio ambayo mbunge makini angekuwa karibu na wapiga kura wake, lakini kwa Halima Mdee imekuwa tofauti, akizidi kuwa MTORO kwa wananchi wa jimbo la Kawe:

1. Kushindwa kuwatetea wakazi wa Madale waliogeuziwa kibao na wenye pesa na kuitwa wavamizi wa ardhi ambako nguvu ya ziada imetumika na kuwachomea makazi na mashamba yao.
2. Waislam kugomea Sensa hasa maeneo ya Ununio, Bunju, Boko na Tegeta Kibaoni ; yeye ameshindwa kuwahamasisha wahesabiwe ili waingizwe katika mipango ya maendeleo ya serikali.

Mwisho wana CDM mutoe ushauri kwa Halima Mdee kuwa ubunge ni kazi ya kuwatumikia wananchi wakati wa RAHA na SHIDA inabidi uwe karibu na wananchi.
 
Yupo kwenye msafara wa M4C si wapigania ukombozi au mlivyomchagua hamkujua hilo?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wana Kawe twamshangaa mbunge wetu kwa vile suala la madaktari alivalilia mbuga kuvunjwa kwa haki za binadamu wakati suala la jeshi la polisi kuwapiga mabomu wapiga kura wake kule Madale yuko kimya??
 
Poleni sana next time bora mumpe Mbatia.

Huku Ubungo sisi wenyewe Mnyika bado hatujaona impact yake kwenye jimbo.
 
Mbona matatizo kama haya yapo majimbo yote ya Dar kwa nini unamsakama Halima Mdee, karibu huku kwetu Temeke utuambie waathirika wa mabomu ya Mbagala wamelipwa na nani mpaka sasa, nenda Ukongo waulizie waathirika wa mabomu ya Gongolamboto wako wapi sasa. Acha majungu na fitina na kama ni sensa sio tu Kawe waislam wamegoma ni almost nchi nzima wewe hukuangalia taarifa ya habari ITV mpaka kule kwetu Katavi mkoa mpya wamegoma kuhesabiwa. Acha majungu na kuwapotosha wana Kawe kama una shida binafsi peleka malalamiko ofisi yake ya Bunge ipo wazi na sio kumpaka matope
 
Mbona matatizo kama haya yapo majimbo yote ya Dar kwa nini unamsakama Halima Mdee, karibu huku kwetu Temeke utuambie waathirika wa mabomu ya Mbagala wamelipwa na nani mpaka sasa, nenda Ukongo waulizie waathirika wa mabomu ya Gongolamboto wako wapi sasa. Acha majungu na fitina na kama ni sensa sio tu Kawe waislam wamegoma ni almost nchi nzima wewe hukuangalia taarifa ya habari ITV mpaka kule kwetu Katavi mkoa mpya wamegoma kuhesabiwa. Acha majungu na kuwapotosha wana Kawe kama una shida binafsi peleka malalamiko ofisi yake ya Bunge ipo wazi na sio kumpaka matope
Samahani kwa kutoa malalamiko dhidi ya mbunge wangu. Mie mambo ya Temeke, Ilala, Ubungo nk hayanihusu nimezungumzia mbunge wetu. Wapiga kura wamepigwa na polisi pia wakachomewa nyumba na mashamba yeye ameshindwa kuwasaidia wala kuwapa pole. Kuwa mkweli Halima Mdee hatupi haki yetu wana Kawe
 
Mbona matatizo kama haya yapo majimbo yote ya Dar kwa nini unamsakama Halima Mdee, karibu huku kwetu Temeke utuambie waathirika wa mabomu ya Mbagala wamelipwa na nani mpaka sasa, nenda Ukongo waulizie waathirika wa mabomu ya Gongolamboto wako wapi sasa. Acha majungu na fitina na kama ni sensa sio tu Kawe waislam wamegoma ni almost nchi nzima wewe hukuangalia taarifa ya habari ITV mpaka kule kwetu Katavi mkoa mpya wamegoma kuhesabiwa. Acha majungu na kuwapotosha wana Kawe kama una shida binafsi peleka malalamiko ofisi yake ya Bunge ipo wazi na sio kumpaka matope

Mleta mada ametegemea makubwa kutoka kwa Halima Mdee kwakuwa ni mbunge kijana, mpya na wa upinzani.

Angekuwa mbunge tu ilimradi mbunge kama wale waliopita hamna aliyelalamika, hii na matarajio makubwa tuliyonayo wananchi!
 
Mbunge wa CCM wa tarime amepora uwanja wa mpira wa miguu mbezi beach eneo la jogoo. Halima mdee uko wapi?
 
Back
Top Bottom