What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?


wafu wawzike wafu wenzao, ww km unasubiria HM aje aalifanye hiili katuu hawezi kutokea, na umempa jukummu kubwa sana ambalo haliwezii, yeye ni mbbunge wa starerhe na mambo ya anasa, nenda bilicanas utamkuta kila siku usiku anakula raha kwa mrija

mwache ale bata wakati sisi tuko kwenye karaha ni zamu yake kula anasa.
 

Hata wa mabondeni walipewa fursa ya kupelekwa Mabwepande ingawa walikuwa wavamizi . Kwa nini Mdee hataka kujua ambacho sisi tunacho kuhusu mgogoro huo?


Ni wazi CCM hawakuweka mgombea mzuri wa kupambana na Mdee kama Kippi Warioba asingeweza kupita na hilo CCM wanajutia. Huyu dada nilikuwa na imani naye sana lakini baada ya kukuta anakaa kimya kwa takribani wakazi zaidi ya 1000 kukumbwa na bomoa bomoa sina imani naye tena.
 
Kumbe mwenzetu kabaila. Ukwasi wote huo unalilia kiwanja cha uvamizi? Wacha wakuvunjie kama una hati nenda kadai haki yako mahakamani.
 
Two wrongs can never make it right. Kupewa viwanja kwa wavamizi wa jangwani sio kuhalalisha uvamizi wa viwanja. Madale hakuna maafa yoyote, wavamizi wanaondolewa full stop. Sera zenu mbovu ndio zinazokuza uhalifu kwa ajili ya kutetea wahalifu. Mfano, watu wamegomea sensa wakakamatwa, kundi fulani likaandamana waachiwe, mkafanya hivyo. Wengine wakaharibu mali kwa kuchoma nyumba za ibada wakaachiwa, mto wa mbu vilevile walichoma nyumba za ibada, maandamano waachiwe ikawa. Usilie, maana ndio mfumo mliojitengenezea, wahalifu ndio wenye haki. Umesahau EPA? Wewe kuvamia unaona ni haki, ila kuvunjiwa malalamiko chungu nzima. Makanisa yanachomwa wala hatuwasikii mkitoka povu, ngoja uchomwe msikiti hata mmoja, maandamano nchi nzima, kama vile wao tu ndio wenye haki ya kuabudu, wengine hapana. Kama mmeamua kubariki mfumo wa kihalifu, mkubali na machungu yake maana hayaelekei upande mmoja tu.
 
Wenyewe mlijua mtapona kwa kuweka ''shina la wakereketwa''.....kiko wapi?.....Leo Ndio wamkumbuka Mdee?...uvunje sheria ahalafu yeye akutetee?




HATA BATI UMEEZEKA LA MAGAMBA!!!

 
Wakubwa mama poroja anaongea ukweli kamanda halima mdee kamasikilize hawa. ila mama porojo wewe si ni magamba wanakubomolea hata wewe? Kweli magamba hawana rafiki kwenye kudhurumu haki.
 
Usiangaike na huyo mkuu, hapo nduo utajua njia ya muongo ni fupi, huyo ni pro-ccmweli ana julikana, sikuhizi sijui ka hama singida

 
Serikali yako sikivu ndiyo inafanya hivyo
 
Ni kweli sisi ni wajinga ndio maana Halima Mdee kashirikiana na wajanja kututosa kuna taarifa Madale kwamba amevuta kitu kidogo ... ukimya wake sio wa bure.
 

nyie hamjajua tu, ila ukweli ni kwamba wabunge wanawake hawana uwezo wa kuwakilisha jimbo. Nafasi sahihi kwa wanawawe ni ubunge wa viti maalum. Mdee alikuwa viti maalum ghafla mkamkabidhi jimbo kitu ambacho yeye haoni kama ni dili sana kwake. Yeye kugombea kawe ilikuwa shinikizi la chama chake na walikuwa hawategemei ushindi ndio maana walikuwa wamesha mtengea nafasi yake ya viti maalum aliyoizoea na ambayo yeye anaimudu kwani anakuwa hana majukum kijimbo ila kichama tu.
 
Mimi siwasemei wengine hii ni shida yangu na wananchi walioomba nipaze sauti kwa niaba yao kule Madele.

ACHA UJINGA WEWE,uvamie maeneo ya watu kwa ujinga wako alafu umlalamikie halima?usitegemee msaada kwa ujinga wako na halima hayuko kutetea maovu na kura usimpe kama unatabia ya kuiba vya watu ukitegemea kuna mtu wa kukutetea,usipoteze muda wako kumsubili mbuge kwa upuuzi wako na ukome maana uko mmezidi kuvamia maeneo ya watu,ulivamia ukisubili hiyo sheria ya mwaka 47 pole na umkome mbunge wetu na uvae gamba tuje tukuchome moto
 
Hapo juu umesema kuwa Ni wazi kuwa ccm hawakuweka mgombea mzuri wa kupambana na mdee.Ama kweli nimeamini kuwa ccm ni wachawi na uchawi wenyewe wameutoa kuzimu ambako si rahisi kufikika isipokuwa kwa shetani na watu wake.km ccm na serekari yake wamewabolea makazi watu wa Madale na wahanga hao wanashindwa kuliona kosa.wakaona kosa kubwa km mlima kilimanjaro kuliko lile la wabomowaji ni la Mdee na adhabu yake ni kung'olewa ubunge hapa siyo bure ni uchawi wa ccm.Askari anaonekana kabisa anamuua Mwangosi kwa kumrenga na bomu anapelekwa mahakamani halafu hapohapo kinageuzwa kibao kuwa yule alie uwa na kupekekwa mahakamani ni dr slaa na cdm. na watu wanalishikia bango kwa kusema cdm ni wauaji huku wakimwacha kumukemea muuaji halisi huu ni uchawi wa ccm.km mikutano imepigwa marufuku kipindi cha sensa cdm wanafunguwa matawi yao na ccm wanazinduwa kampeni zao kipindi hichohicho na siku hiyohiyo.CDM wanahesabiwa kuwa wamekunya mavi na kushambuliwa.na ccm wanaonekana wamekunya keki huu ni uchawi.
 
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.

Pole sana mkuu, sasa hapo hawajashika nchi sijui wakishika itakuwaje, ni kazi ya KUJIJAZA DHAHABU KOCHO KOCHO mikononi na shingoni lakini wala hawawajali wananchi wake ! na nashangaa yupo kimya sana huyu binti! ile jeuri alokuwa nayo mjengoni imeishia wapi??? Halima jitokeze mama ujibu !
 
Nafikiri Mdee yupo below expectations kwa mtizamo wa wananchi wengi,mfano ni juzi tu nilikuwa pale afrikana kwa vijana wa bodaboda na bajaji kwa shughuli maalum nao wanalalamikia mwenendo wa mbunge kutoonekana hasa kutatua kero zao za muda mrefu! Mdee take care my sister tunakutakia mema kamanda!
 

Wamebomolewa na Halmashauri inayoongozwa na Meya wa CCM!

Wakati wa bomoa bomoa policcm walikuwepo kusimamia!


Na Mkuu wa Wilaya, ambaye ni mwakilishi wa Rais eneo hilo aliafiki.

Hivi kwa nini hatuoni role ya CCM katika kitu chote hiki tunatauta mbuzi wa kafara (scapegoat) in Halima Mdee?
 
Angalia pekundu: Msimamo wa CCM ni kuwa mliobomolewa "ni wavamizi na wahuni" - Rita Mlaki (Mb CCM)

 
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.

Hivi ukibomolewa nyumba unapeleka kesi yako mahakamani au unalia mbunge aje? Halafu acha uswahili na mambo ya kienyeji wewe, hayo majungu. Mh.Mdee mara nyingi mbomvi wake bungeni ni waziri wa ardhi na mara ngapi bwana tunamwona akiwatetea wananchi na nyinyi magamba mnaishia kusema anataka sifa, sasa leo wamebomoa kibanda chako kibayabaya ndio unajifanya unajua kuwa mbunge anaweza kukutetea.

Halafu aliyevunja hilo banda lako ni nani? Si ni serikali iliyoichagua ya magamba, sasa unataka Mdee afanye nini? Mpe dola akutetee
 
Bado hajaolewa, mchumba wake wa mwisho alikuwa Joshua Nasari sijui wamefikia wapi walitangaza hadharani kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

Umbea wa ki-CCM huu. Wewe umeolewa? Yaelekea wewe ndio sonara uliyetengeneza pete ya uchumba ndio maana unafahamu sana. Mtu akifuatilia maongezi yako anajua tu ndio dizain zile zile za kusutana na kulumbana na majirani. Mbona serikali yenu ya magamba imefanya jambo la maana kuvunja hilo banda lako


Haya ndio mambo ya kiswahili ukisikia uswahili. Imekuwa nongwa sasa, mtu siku zake za hedhi zikipitiliza, MBUNGE WA CDM. Mtoto wako akifukuzwa ada ya shule kwenye kata school, MBUNGE WA CDM. Ukipoteza hela ulevini, MBUNGE. Hivi wabunge wa CCM walikuwa wakiwapikia majumbani kwenu eeh?

Wewe baba mtu mzima unazungumzia below expectation kwa mbunge anayewajibika bungeni kama Mdee hivi hata aibu huwa hatuna, eti? Hivi kero zooote siku hizi zinatatuliwa na mbunge?

Mimi naomba unitajie kero tatu ambazo BODABODA wanataka mbunge awasaidie kuzitatua, angalau na mimi leo nifumbuke.
 
Sera ya bomoa bomoa Manispaa ya Kinondoni ambayo inayoongozwa na Meya wa CCM sasa imehamia kwenye Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni kwa Mh. Iddi Azzan baada ya kutoka Jimbo la Kawe.

Jana wakazi wa Sinza Mori na Bamaga walibomolewa nyumba zao. Zoezi hilo lililoacha simanzi, majonzi na vilio kwa wakazi hao, limefanyika jana na kushuhudiwa na kamera ya mwandishi

Greda likijiandaa kuanza kazi!


Wananchi wa Sinza wakijaribu kuokoa mali zao kabla Greda halijapitia


Wanamgambo wa Halmashauri wakisimamia zoezi

Greda likivunja Geti la Nyumba

(Habari /Picha : Haruni Sanchawa, GPL)
 

Attachments

  • 1.jpg
    79.9 KB · Views: 106
  • 5.jpg
    50.5 KB · Views: 107
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…