Mbunge wetu Halima Mdee, kumbuka maneno yako matamu kama asali uliyotoa kipindi cha uchaguzi hatimaye wana Kawe wakakupa UBUNGE. Umepita mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu umekabidhiwa dhamana ya kutuwakilisha MJENGONI Dodoma.
Twakushangaa sana unakuwa mkimya kipindi ambacho wananchi twahitaji utetezi wako. Nachukua fursa hii kukukumbusha wapiga kura wako wa Kunduchi Machimboni twapata shida, kuanzia wachimba kokoto, mama nitilie, wauza kokoto na wenye nyumba katika eneo husika twanyanyaswa na uongozi wa wilaya na mkoa. WEWE UPO KIMYA tukuelewaje??
Tulitegemea mara baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa tamko la kufunga machimbo, wewe ungetoa msimamo wa kuunga wapiga kura. Mbaya zaidi ofisini haupatikani KULIKONI Mheshimiwa, ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, tulifikiri wewe utakuwa Mbunge bora kumbe AFADHALI wakati wa RITA MLAKI alikuwa karibu na wapiga kura.
Tafadhali njoo utusikilize na kutuunga mkono ili tusihamishwe na nguvu na FFU.
Toa unafiki hapa