Wezi wavunja na kuiba laptop na sukari kilo 25 Ofisi za Mahakama ya Wilaya Njombe

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za wizi baada ya kuvunja Mahakama ya Wilaya ya Njombe na kuiba vitu mbalimbali vya ofisi hiyo ikiwemo Laptop tatu (3) na Sukari kiasi cha Kg 25, waliokamatwa yupo aliyeiba na mwingine aliyeenda kuuziwa Laptop hizo.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 7, 2020, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah na kuongeza kuwa tukio hilo ni la ajabu na hivyo wanangoja utaratibu ukamilike tu ili waweze kuwafikisha mahakamani kwa kuiibia Mahakama.

"Huwezi ukaamini na ninaomba uamini, kuna watu wameenda wamevunja Mahakama ya Wilaya ya Njombe, hivi ninavyoongea hapa Mahakama hiyo ilivunjwa, ikaibiwa vitu mbalimbali ikiwemo Sukari Kg 25, na Laptop 3, tumeweza kukamata hizo Laptop na watu wawili tumewakamata, yaani watu walivyo majasiri hawaogopi hata vyombo ambavyo vinawatendea haki", amesema Kamanda Issah.

 
Hii kali kuiba mahakamani ajabu na kweli
Polisi muanze na wafanyakazi wa mahakama kurahisisha upelelezi
Kuna mada ilikuja humu miaka ya nyuma kusema walinda usalama wanawajua wezi na wanawalinda
Vibaka wezi wapo wengi Mkoani Njombe ukifika kulala guest house ulale ba bag lako chini ya mtu
Ajira Biashara hakuna haya ndio matokeo yake
Wekeni mgambo ya zamani Amani irudi mtakuwa mmezalisha ajira kwa vijana wengi
 
sukari ilikua inafanya nini mahakamani hapo ?

halafu alikuambia mahakama inatenda haki ni nani ???
 
Back
Top Bottom