Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Popote??? Hahahaaa hata kama ni hasira za kuibiwa ila si kusema popote Wanapouza tv tukwambie
 
umenikumbusha wkt nilipokua kigoma mgeni, usiku mida ya saa 9 wez wakafungua mlango wa chumbani kwangu, nashukuru Mungu niliwasikia mapema. sasa washafungua ndo wanaingia nikawaambia karibuni sana, tena kwa saut ya upole kama nakaribisha mgeni. kilichotokea walitimua mbio si za kawaida wakagongana wakaanguka kabla ya kukimbia tena walivyonyanyuka. muda wote huo mi nawacheki nikawauliza mbona mnakimbia? nikarud kulala nikafunga na funguo tena alaf nikauacha mlangon ila nikauzungusha kidogo ili usitoke tena kama mtu akiingiza funguo mwingine upande wa pili wa mlango.
 
Yan jamaa umeibiwa ila the way unavoandika kimasihara sana aisee
 
Fundi wajenzi wanatabia ya kugonga funguo kwenye sabuni wanaenda kuchonga kopi rait;
Hela lazima ulale nayo beneti heri ukose tendo la ndoa hela ilale kwenye bukta;
Kukosa tendo la ndoa na usha ambiwa shemeji alilala uchi ni uzembe
 
Asee bwashee hii kitu. I serious lakini kwa ulivyopresent umeifanya iwe kama kichekesho flani. Ila pole mwanangu. Kama wewe na mama mpo hai na hawajamgusa mamsap basi hizo hela zinatafutwa tu..... Ile Heineken imeniuma.... Halafu hao mabwege hata Ladha ya hiyo bia hawaijui...
 
Aika Meku, Mkuu, sina jinsi ya kuelezea maana, hawa mapimbi sasa wananifanya niangalie taarifa ya habari ya ITV bar kila saa mbili usiku...!

Kutafuta maloss report ya ID zangu walizolamba...! (manina zao).
 
wakwetu.kabisaa kwa tapo
 
Kama nyumba unayoishi ni ya kupanga na ulipoingia hukubsadilisha vitasa hasa vya nje including gate ujue mlinzi aliyeachwa akilinda nyumba pindi wanasubiri mpangaji mpya huwa anajichongea funguo mapeeeeeema kabisa. Na kama hukubadili basi iwe ni fundisho. Hata site siku hizi vile vitasa vya maana vina site keys na ukishahamia unadadili siku hiyo hiyo.
 
Ndo maana maisha yangu yote sijawahi'lala nasitokaa nilale mbupu nje,nafanya yangu nikimaliza bukta iko wapi navaa ndo nalala..situations kama hizi ndo utakapoona umuhimu wa kulala umejistiri.pole sana mkuu kwa masaibu yaliyokukuta ila tukio lako limenifanya nizidi kukazia msimamo wangu kulala nimejisitiri kwani likitokea la kutokea ni rahisi sana kuchukua hatua.
 
Pole mkuu, wanakera sana wezi. Mimi wamewahi kuvucha kioo cha gari wakaiba power windows na side mirrors. Halafu ilikuwa imebaki wiki moja kabla ya harusi yangu kipindi ambacho nilihitaji gari kufanya mizunguko.
 
sio bure Huyu atakua mhaya huyu ukisoma uzi wake utaelewa uhaya wake ila ana bahat sana hawajamlawiti
Ndiyo nini comment yako hii?
Mtu anazizima kwa maumivu ya "kupigwa", af'wewe unamletea za kuleta, akikutukana matusi ya nguoni nitam-like na kumuombea moderators wamlinde wasifute aliyokutukana.
Sipendagi ujinga mie!
 
inasemekana njia sahihi ya kujifungia ndani.. ni kufunga kwa komeo kwa ndani.... hapo mtu hata aje na funguo malaya gani hawezi kuufungua yeye akiwa nje..
Kufunga kwa komeo ndani na kupiga kufuli hilo komeo, labda waje na "fatuma" kuvunja mlango.
 
Pole sana usiku funga mlango chomoa funguo hakikisha sehemu ya kuingilia darini imezibwa (kuna nyumba kuna sehemu huachwa wazi kuingilia kwenye dari ceiling) mashetani hawa. Poole sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…