Wezi wa simu TAZARA

Pole sana mkuu,mm kuna mmoja alitaka kuniibia maeneo ya mbagala pale darajani nikiwa kwenye,alivyokuja ile kukamata simu nikamuwai kumshika mkono.Kilichofuata hapo ni kipigo na nikavunja mkono kabisa,shenzi kabisa hao vibaka.
 
Kuna jamaa walikuwa wanaiba kwa style hiyo hiyo..siku moja nikamnasa na kumkwida pale dirishani akiwa anataka kuniibia...nilimpiga vichwa huku nahesabu...watu wakanikuta Niko kichwa cha 52, 53, 54, 55,56.......!

Chai😀😀😀😀
 
Safi sana kwani si kila jambo lazima ulifikishe polisi kabla hujaonyesha jitihada binafsi kama hizo zako.
 
Safi sana, mkuu nikajua umekuja kulia kama wavulana wa dar
 
Kama Police alikuomba laki 3 ili afuatilie mwizi wa Simu yako kuna uwezekano mkubwa ulipoondoka na mwizi wako aliachiliwa......
 
Big up sana mkuu vibaka wa pale TAZARA ni wamoja na wale wa pale buguruni chama (Kimboka), wana kera sana hawa wehu. Mfanp TAZARA pale kituoni kuna yule mteja maalufu anayekuwaga kabeba kikondomu (kimfuko cheusi cha rambo) kwaajili ya kupiga nyoka mafuta kwenye magari , afu kiunoni kabana naspana yake. Ana kamwili mgoroko mgoroko hivi afu mweusiii..tiii,yaani kama wewe ni kama ni mpitaji mzuri wa pale TAZARA utakuwa ushamjua huyo jamaa.

basi wanajifanya wanapiga debe kumbe mwisho wa siku wanavizia watu wa kuwapora simu zao na kuvuka barabara huku magari yanapita kwa kasi kwenda kuvuka TAZARA mataa....kwahiyo una baki unakodoa tu macho namna anavyoyakwepa magari licha ya mwendo mkali waokuwa wapita nao madereva.

siku ukiwatia mbavuni ni kuwapa vitasa vya haja mpka wachanganyikiwe machoko hao.
 
Kuna jamaa walikuwa wanaiba kwa style hiyo hiyo..siku moja nikamnasa na kumkwida pale dirishani akiwa anataka kuniibia...nilimpiga vichwa huku nahesabu...watu wakanikuta Niko kichwa cha 52, 53, 54, 55,56.......!
Nimecheka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…