Kufungwa rasmi na milele kwa stendi zilizokuwa shekilango, Lumumba na mnazi mmoja imekuwa kicheko kwa matapeli, wezi, vibaka , wabakaji na waganga wa kienyeji waliokuwa wamekosa kazi:
MADALALI:
Ukishuka tu stendi pale , una mizigo, walet mfukoni na mabegi unavamiwa na vijana , MMOJA ANA TIKETI, MWENGINE ANAKUPIGA FINGA, MWENGINE ANAKUVUTA BEGI NA KUELEKEA UPANDE MWENGINE.
Dalali anakwambia Gari fulaniMbovu inaua sana, njoo nikupe hii haina ajali, abiria anaogopa na anamfuata dalali.
TIKETI FEKI:
Abiria anakatiwa tiketi ina jina la basi , ila ya mkononi anaambiwa akifika kwenye gari atapewa nyingine, mkononi say unaenda Arusha unalipa 40,000 kwa Dalali, alafu dalali anampa kondakta 30,000/- yeye anakupiga 10 na hujui kama ni mu wa lile basi ama la na amevaa flana ya basi husika tofauti na shekilango aboria aikuwa anafikam ofisi za basi ndani kabia.
WABAKAJI:
Genge la wahuni, wala mirungi na wanywa visungura, wao wanafanya kulaghai wanafunzi nanaotoka mikoani kuja DAr, kuwadanganya kuwapeleka chuo lakini wanaawapeleka magetoni na kuwabaka.
MUDA WA SAFARI:
Kwakuwa abiria anakatiwa tiketi na kishoka, akisema anataka basi la muda huo huo, basi mkata tiketi anamwambia basi ndio linaondoka, unakuta ni saa moja asubuhi kumbe basi linaondoka saa tano na mtu alikuwa anawahi maziko mkoani. Wale wakata tiketi si waajiriwa wa mabasi , hivyo huwezi shitaki basi. Hizi ni changamoto kubwa.
WAUZA VYAKULA:
Mtu anauza chips mayai ambayo ishapikwa inauzwa dirishani, hivi kwenye kituo cha daldala kweli chakula kinauzwa dirishani na mkuu wa mkoa anamuacha afisa afya wa jiji ofisini?
WAKATA USHURU WA KUINGIA GETINI:
Alfajiri ukingia , ukiwapa hela hawakupi tiketi, wanaibia serikali mpaka kamwanga katoke ndio wanaaacha. Hapa pawe na kamera