Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,374
- 26,981
Abiria waliosafiri na BM Coach Kutoka Arusha siku ya Jumapili 25-10-2026 , namba tajwa hapo juu, ilitoka saa nne kamili na kufika moshi Saa sita kasoro, japo ilipaswa kufika saa tano na nusu kama tiketi za Moshi zinavyo onyesha kwenye kituo chao jirani na TRA Moshi.
Abiria wa Dar es salaam walifika Tegeta Kibo Complex majira ya sa nne kamili usiku na utingo ambaye ni binti mdogo mweusi asiye na uzoefu japo ana roho nzuri, aliwatangazia abiria wanaoshukia Shekilango kuteremka hapo Kibo Complex na kusbiri usafiri mwengine.
Wasafri hao, walishushwa barabarani, bila maelekezo ya ziada na wengi walikuwa wageni wanafunzi wa mwaka wa kwanza , huku wakizurura pasi kujua, wakavuka barabara na kwenda banda la BM ku-ulizia hiyo shuttle lakini walijibiwa kwa kejeli na kuambiwa kama wanataka wamtafute aliyewakatia tiketi.
Abiria walisubiri mpaka saa tano usiku ndio SPECIAL HIRE ikaja, kumbuka wameubiri karibu saa nzima, ilipokuja na abiria kufika shekilango, bado lile basi lenye mabegi likachelewa kwa karibu nusu saa nzima , lilienda Mbezi Luis, maana yake abiria kafika Dar saa nne anachukua begi saa sita usiku, hii si sawa, kama hawana utaratibu maalum basi wawafikishe mbezi Luis na kuwa dump huko.
NB: Watu wanakimbilia BM na Esther Luxury kwakuwa kuna shuttle, lakini kwa hii tabia, anguko linakuja