Wewe ungeamua nini…???

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,244
31,338
Wewe ungeamua nini…???
Kuna jamaa kaoa lakini pamoja na hayo ana kimada nje ya ndoa yake. Mkewe alishatonywa lakini aliamua aanze na uchunguzi. Sasa kuna siku baba aliamua ku-surprise kimada wake kwa kumnunulia simu, lakini risiti iliandikwa jina lake (la baba). Alipofika nyumbani risiti akaisahau kwenye suruali, kama kawaida mama katika harakati ya kufua akiona. Baada ya kuisoma, akafahamu aina ya simu iliyonunuliwa. Cha kwanza akaamchunguza Yule kimada wa mumewe kama ana simu ya aina hiyo. Baada ya kupata uhakika huo, akaenda polisi kushitaki kuwa kaibiwa simu aliyonunuliwa na mumewe na mwizi wake anamfahamu. Kama kawa polisi wakaenda kumkamata kimada na baada ya kuulizwa akadai simu kanunuliwa na mpenzi wake. Akatumwa akamwite huyo mpenzi wake. Baada ya kutinga polisi, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
Polisi: huyu unamfahamu..??
Baba: ndiyo ni mke wangu.
Polisi: hii risiti na hii simu unavifahamu..??
Baba: ndiyo.
Polisi: vya nani…??
Baba: mke wangu.
Polisi: we dada (kimada) hii simu si yako ni ya huyu mama, hivyo unawekwa ndani kwa kosa la wizi.
Baada ya mume na mke kuondoka, mume alirudi tena kuweka mambo sawa na kimada akatoka.
Swali
kwa wanawake, kama ungekuwa kwenye nafasi ya mke, ungefanya nini…??? Na kama ungekuwa ndo huyo kimada ungechukuwa hatua gani baada ya hapo…???
Kwa wanaume, ungefanya nini kwenye nafasi ile ya mume..???
 
Aliyesababisha matatizo yote haya ni huyu m'baba na ashiki zake za mademu na nyumba ndogo!...Kumwomba talaka si suluhisho, lakini anatakiwa akalishwe chini aambiwe na wazee wenziye kwamba anajidhalilisha bure!...
 
Ama kweli nimegundua watu hawana straight answers. Wengi wetu tuko humu. Kuna hata wengine walishawahi kwenda na chupi tofauti nyumbani.
Kwa nafasi ya mume,,,,, INGEKUWA NI BUSARA ZAIDI KUKAA NA MKEWE NA KUTUBU YOTE NA AKUBALI KUANZA UPYA. I do believe that all comes round goes round. Suluisho la kweli kwa wanandoa hutokana na wanandoa wenyewe. Kwa mwaname/ke kufikiri eti wanalipiza kisasi kwa mwenzake ni upotovu mkubwa. Kama kuna ambacho unafikiri kuwa unakikosa kwa mkeo/mumeo kwa nini usitafute namna ya kukiintroduce kwa mwenzako badala ya kutafuta mtu wa nje wa kukifanya. Ukichunguza sana utakuta ni ama jambo amabalo mnaweza mkawa mmelisikia kwa marafiki hivyo mnataka mahali pa kujaribia ama ni yalikuwa mazoea yako na kwa sasa unajaribu kumficha mwenzako. Ni vizuri kuweka wazi aina ya mapenzi uyapendayo kwa mwenzako. Ninaamini kabla ya kutangaziana ndoa mlikwisha onja TUNDA na mlifanya fujo zenu. Iweje leo mmeona mnaacha fujo? Mi nafikiri mngedouble kwa sababu sasa ni halali kwenu maana mmekwisha halalisha kwa ndoa mliyokubaliana. Kutokuweka wazi aina ya mapenzi myatakayo humfanya mtaka hiyo aina ya mapenzi amtafute yule amabaye alikuwa akimfnyia hivyo vibweka. Kuweni waziiiiiiiiiiiiiii kwa wapenzi wenu.
UAMUZI WANGU NI KUOMBA RADHI KWA UJINGA NILIOUFANYA NA KUAHIDI KUTORUDIA TENA. TENA KWA DHATI KUU. Ni mawazo yangu tu
 
UAMUZI WANGU NI KUOMBA RADHI KWA UJINGA NILIOUFANYA NA KUAHIDI KUTORUDIA TENA. TENA KWA DHATI KUU. Ni mawazo yangu tu

Sidhani kama utasamehewa! Ni mwendo wa kukana kwa kwenda mbele! Si mjui huyu mwananamke ila nakumbuka wakati natoka kununua simu nilikuwa naye kwenye gari then nikagundua simu imepotea lakini siku kuambia my wife nkaogopa utanisema (Maana kwa kusema tu mke wangu umebarikiwa) ila Kosa nililofanya siku kumbuka risiti ya hiyo simu nilisahau kwenye mfuko wa suruali. (teeeehe! teeeehe! haah! haaah! mbona raha!)
 
eeeh...nimejaribu kujiweka kwenye viatu vya huyo baba vinanipwaya!!!!
 
Ama kweli za mwizi arobaini!! Ningekuwa mimi mh ngoja kwanza nikafikirie ningefanyeje ila hivyo viatu vinanipwaya mno.
 
unapodanganya,hakikisha haitajulikana milele,huyo wife atafuatilia atakuta hata dhamana ulishamuwekea bi mdogo,hapa wewe uchune tu kaa kimya
huna haja ya kucoment chochote;
1.ukikubali kosa......umempa nafasi nae akamegwe
2.ukiendelea kukataa..........ushahidi upo na unazidi kumpandisha hasira bibie.
mimi ningenyamaza tu na kuwa mpole isivyokawaida,atasemaaaaaaaaaaaaaaaa akitulianitamjibu;
'' wewe umeshaamua kunidhalilisha na kuniona malaya na mkosefu basi endelea''
unajua kwa kila wawili wapendanao yupo mjanja na mwingine ndio hivyo tena nasita kumwita mjinga. Hapa huyu jamaa ni mji...tu.
unapaswa uwe mwangalifu.unaacha risiti kwenye shati? ni uzembe wa hali ya juu kabisa.Kama huwezi kuwa mwangalifu ya nini kutongozatongoza?
 
NI kukana tu! SIna mengi maana kuongea sana kutanifanya ntoke nje ya mada!
Unakana nini sasa ndugu?
Unakana kuwa hiyo risiti ya simu siyo yako? Unakana kuwa simu siyo yako? Unakan kuwa jina lililoko kwenye risiti siyo lako? Unamkana mkeo na kumtambua kimada au unamtambua mke na kumkana kimada?
Nadhani kuliko kuonekana kituko mbele za watu wazima wenye akili, ni bora ukubali uombe radhi. Bahati nzuri wanaume wanajulikana kuwa wengi hufanya makosa kama hayo na bahati nzuri pia ni kuwa wake zenu huishia kuwasamehe bure tu.
 
unapodanganya,hakikisha haitajulikana milele,huyo wife atafuatilia atakuta hata dhamana ulishamuwekea bi mdogo,hapa wewe uchune tu kaa kimya
huna haja ya kucoment chochote;
1.ukikubali kosa......umempa nafasi nae akamegwe
2.ukiendelea kukataa..........ushahidi upo na unazidi kumpandisha hasira bibie.
mimi ningenyamaza tu na kuwa mpole isivyokawaida,atasemaaaaaaaaaaaaaaaa akitulianitamjibu;
'' wewe umeshaamua kunidhalilisha na kuniona malaya na mkosefu basi endelea''
unajua kwa kila wawili wapendanao yupo mjanja na mwingine ndio hivyo tena nasita kumwita mjinga. Hapa huyu jamaa ni mji...tu.
unapaswa uwe mwangalifu.unaacha risiti kwenye shati? ni uzembe wa hali ya juu kabisa.Kama huwezi kuwa mwangalifu ya nini kutongozatongoza?

Tall mtu wangu, inaelekea una uzoefu sana eh?
 
Kama baba nitafanya haya yafuatayo;

1. Nitamshauri huyo kimada aseme kuwa hiyo simu ameiokota, nami nitamwambia mke wangu kuwa nilimnunulia yeye lakini sijui nimeidondosha wapi.

2. Kama hiyo haitokuwa na nafasi tena, basi strongly nitamruka huyo kimada na iwe ndio mwisho wa mahusiano yetu. Au huenda atanielewa tu baadaye.
 
mie ningerudi kabla ya mume wangu na kumtoa huyo mgombea mwenza. kisha ntamwambia sio vizuri unavyofanya, lakini akikurudia we endelea tu kumtumia. tukirudi home mie na la'aziz wangu nampandishia kidogo afu namsamehe. Kwa upendo (japo hataamini) namsomea mithali 6:32 @ Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; wala fedhea yake haitafutika!! '
 
Back
Top Bottom