Wewe kijana wa sasa nakushauli uoe ila sio kufunga ndoa

mkushite

JF-Expert Member
Sep 2, 2021
623
1,467
Hii mada ya kataa ndoa inabidi ijibiwe kwa hoja na sio mihemko, vijana wetu wanaikataa ndoa wakiwa na mantiki kubwa sana, inaitaji umakini mkubwa sana kuwaelewa na kuweza kujibu hoja zao za msingi.

Kwa mimi binafsi nadhani kuna utofauti kubwa kati ya kuoa na kufunga ndoa.

1. Naanza na kuoa.

Wazee wetu wa zamani walikuwa wanaoa siyo kufunga ndoa. Ndiyo maana familia zao ziliweza kuishi kwa amani kubwa sana na kuheshimiana tofauti na sasa. Mwanamke alikuwa ana adabu kubwa na anamtii mme wake. Hakukuwa na tamaa za mali ambazo kwa asilimia kubwa zinavunja familia. Mwanamke alijua anatoka kwao anaenda kuolewa na kuanzisha familia na siyo kuchuma mali.

2. Ndoa
Ni upgrade ya kuoa ikiwa na maana hii ifuatayo.
Tafsiri ya ndoa za kipindi hiki ni kama ajira ama taasisi ya biashara yaani startup ambayo founders wawili kila mmoja ana share ya 50% ya ownership. Ambapo anytime founder yeyote anaweza kuharibu hiyo taasisi iliyoanzishwa na kuondoka na 50% yake. Na hii imetengenezwa kwa ajili ya favour ya mwanamke, power ya mwanamme ni kama haipo kwenye ndoa. Ndoa imeegemea upande mmoja na wanawake wanatumia iyo weakness vibaya sana. Hakuna mwanamme anayeweza vumilia kukaa na mwanamke malaya, mjeuri, mwenye kiburi, asiyemsikivu e.t.c eti kisa kafunga naye ndoa.

Maoni yangu ni kwamba turudi kwenye utaratibu wa zamani yaani tuoe na tuzae ila tusifunge ndoa. Familia yenye ustawi mzuri lazima iwe ni ya baba mama na watoto. Cheti cha ndoa hakikupi guarantee ya kuwa na familia yenye amani ila kimejikita zaidi kwenye upande wa ndoa ikivunjika tugawane mali.

Ndoa zimekuwa za kitapeli.
 
Mungu hapendi uzinzi. Amri ya 6 ya Mungu anasema usizini
Hizi dini ambazo zimeleta utaratibu wa kufunga ndoa hazina miaka 200 tangu zimekuja Afrika. Inamaana kipindi chote cha nyuma mababu zetu walikuwa wanazini? mbona familia zao zilikuwa zinastawi vizuri kuliko sasa. Sema tumeacha utaratibu wetu wenye amani tumefuata utaratibu wa wengine wenye migogoro na ukiangalia kwa umakini mkubwa sana, hizi dini zinatengeneza matatizo ili ziweze kuendelea kuwepo. Jiulize kama familia zikiwa na amani nani ataenda kanisani au msikitini? Asilimia kubwa ya wanaosali wana matatizo yao binafsi au kwenye familia.
 
Wazungu wenyewe mambo ya ndoa yamewashinda, imebidi waongezee na ndoa ya mkataba , ila sizani kwetu kama tunaweza kufika huko coz vijana wengi tu wanagoma kufunga pingu na hao wachache walio funga wanatimka mapema kabla ya kuwa na uchumi unaoeleweka na umri kukimbia .
 
Cheti cha ndoa
Hiki kikaratasi (mnaita cheti cha ndoa) ndiyo kinacholeta shida. Mwanamke anakitazama kikaratasi hiki kama mtaji. Huwa anafanya makeke ya kuvunja ndoa kwa kuwa ana uhakika wa mgawanyo wa mali 50% , 50%.
 
Tatizo vijana wenyewe ndio wavurugaji,twa hovyo tunapiga magoti kuvalisha pete ya uchumba,kubembeleza kwiiingiii,kuhonga kwa sana lazima vione ndoa chungu. Mwanaume ukiishi kwa misingi na misimamo imara hauwezi kataa ndoa
 
Ndoa sio mbaya ila taratibu zake ndo mbaya mfano
1. Mahari kubwa
2. Harusi za gharama
3.sheria za ndoa za kugawana 50/50
4. Ubnafsi wa wanawake, chake ni chake cha mme cha wote
5. Vyama tetezi vya wanawake kama ustawi na dawati jinsia kumkandamiza mme
6. Wazazi kumtuma binti achume mali kwa mmewe (eti mme sio ndugu yako)
7. Dhana ya kuhudumia kwamba eti kwenye ndoa kuna mhudumiwaji na mvuja jasho badala ya wapambanaji wawili yaani mpambanaji na msaidizi

Hoja hizo zikijibiwa vema basi ndoa ni nzuri na salama
 
1.Mahari inakuweka huru ndo maana ukishaoa hata mke akifa anazikwa unapotaka wewe,mahari inakupa heshima na sauti ndani ya nyumba,mahari ni shukrani kwa wazazi wa mke. Tatizo linakuja pale mnapotaka au wanapotaka sherehe kuubwa ndipo mahari inakuwa kubwa ili kuitumia kwenye sherehe ya kitchen na send off party. Ukioa familia maskini au yenye tamaa ya pesa lazima wakupige mahari kubwa

2. Harusi za gharama zinakuja pale unapooa mke mwenye kujionesha na ndugu wenye kutaka makubwa wakati uwezo hawana. Mkuu weka msimamo wa harusi uitakayo. But ili hili jambo lifanikiwe uwe na Mtarajiwa anayeelewa kipato chako na msimamo wako. Simamia unapomudu

3.Pasu kwa pasu inatumika vibaya sana ,hii sheria wanaume mkiielewa wala haitawahangaisha.

4.Kulingana ntu na ntuuuuuu(mtu na mtu)tatizo mnaoa wale wa kuringishia washkaji vijiweni na sio wale wanaojua maana ya familia na ndoa

5. Ukiifahamu haki yako kwa undani na ushahidi wote wala hakuna wa kukusumbua hapo

6. Umeingia cha kike,bonge la ndoige ,muwe mnachunguza na familia za kuoa sio umempenda binti unakurupuka kuoa bila kuchunguza chimbuko lake.

7. Hii dhana mliianzisha wenyewe ili muwe kichwa cha familia mkuu. Tangu utoton hadi nilipo nashuhudia wanaume ndio wahudumiaji wakubwa. Mkianza mahusiano muwe mna balance masuala ya uchumi sio kila outings pesa zinakuchomoka tu,kila ukiombwa pesa unatoa tu,nguo unanunua. Halafu baada ya ndoa utake kubadili style ya utoaji pesa inakua ngumu sana kukubalika

mambo numbisa
 
Vijana wanaoa kwa kigezo cha taqo na sura

ova.

5. Ukiifahamu haki yako kwa u
 
Hizi dini ambazo zimeleta utaratibu wa kufunga ndoa hazina miaka 200 tangu zimekuja Afrika. Inamaana kipindi chote cha nyuma mababu zetu walikuwa wanazini? mbona familia zao zilikuwa zinastawi vizuri kuliko sasa. Sema tumeacha utaratibu wetu wenye amani tumefuata utaratibu wa wengine wenye migogoro na ukiangalia kwa umakini mkubwa sana, hizi dini zinatengeneza matatizo ili ziweze kuendelea kuwepo. Jiulize kama familia zikiwa na amani nani ataenda kanisani au msikitini? Asilimia kubwa ya wanaosali wana matatizo yao binafsi au kwenye familia.
Alisikika mtu anaimba "IBAADA NJEEMAAA INAANZIA NYUMBANIII"
 
Back
Top Bottom