Fundi Mchundo,
Mkuu ama kweli una cheap politics... Sasa unataka kusema uchaguzi wa rais Zimbabwe ni kati ya Mugabe na Morgan?... hii imenza lini ama unazungumzia kurudiwa kwa upigaji kura..Je, hizi mbinu za wazungu wamezianza majuzi baada ya uchaguzi?..ama nimesema wamezianza toka mwaka 2000 baada ya Mugabe kuchukua ardhi..na ndio sababu ya hapa tulipofika..wapo viongozi wengine kibao kwa nini usiwataje wale isipokuwa Mugabe tuuu umemshupalia kama vile ndio neno lilowekewa ubani. Hoja hujibiwa na hoja, wee sema mazuri ya Morgan kisha dhidi ya maneno yangu tutaendelea...
Hivi kweli unasoma nayoandika mkuu.
Ebu nikuulize tena kwa wale wanaosema Chadema haifai kuongoza ama Mbowe hafai wana maana kuwa wanampendekeza Kikwete kuwa ni bora na wanampigia debe..Haya nambie sisi tunaompinga Kikwete hivi sasa tunampigia debe nani maanake kuna watu wawili ktk ufahamu wako.... wapi na wapi mkuu!
Wee vipi soma maandishi ya watu na jaribu kuyaelewa kwanza.
Mkuu kama Kikwete na Lowassa ndio watabakia ktk uchaguzi wa rais Tanzania nitawapinga wote!.. nitayasema mabaya ya Lowassa kama atakuwa ktk nafasi ya Morgan na nitaendelea kumpinga Kikwete (Mugabe) kwa yale alokwisha yafanya!.. Hii ndio lugha yangu.. bado tu!
Exactly Bob hapo ndipo unashindwa kumuelewa Fundi na wengine wenye mawazo yanayofanana fanana na ya kwake kama sisi. Hapa hakuna anayemtetea Morgan au ambaye anasema kwamba wazungu hawako culpable kwa matatizo ya Zimbabwe. No.
Hapa tunaongelea ni jinsi gani Mugabe anavyowatreat wale wasiokubaliana na sera zake! wanaochomwa matako na kuuawa..siyo wazungu hata kidogo, na anayewachoma siyo Bush ni Mugabe na utawala wake.
Hili swala kitu ambacho Fundi amejaribu kukielezea hapa na wengine ni kwamba tunaangalia hali ilivyo kwa sasa. Ukiingiza uporaji wa mashamba sijui na mambo gani ya kihistoria we LOSE FOCUS of our arguments na Mugabe anataka topoteze mwelekeo wa arguments. Ndo maana wote wanaomtetea Mugabe..hawaongelei violence dhidi ya wananchi, bali wamejikita kwenye madhambi ya wazungu na mashamba! Kitu ambacho hakimsaidii mwananchi aliyechomwa moto na hana pesa ya kwenda hospitali!
Exactly thats what Mugabe wants. To cover his evil and terror against his opponents kwa kutumia historia!.. Kwa hiyo Mugabe anawachoma moto na kuwaua raia wake kwa kulipiza kisasi kwa wazungu? Hapana hili swala tuliangalie kama lilivyo. Huwezi kuua watu na kusponsor terror dhidi ya wapinzani wako kwa pretext ya HISTORIA jinsi ulivyonyanyaswa na wazungu. Sijui ni kitu gani BOB usichokielewa hapa.
Lastly, unaweza kumhukumu Morgan ambaye hata ikulu hajaingia? kwa nini tusiheshimu mawazo ya wazimbabwe..kumuingiza Morgan au Mugabe madarakani?..asipotimiza matarajio ya wazimbabwe ataondolewa after five years in a fair and periodic election! Thats our concern. Tumeyaona Malawi Muluzi aliingia kama hero after Kamuzu Banda but we have seen how HIS people have pushed him out. Zambia Chiluba aliingia baada ya Kaunda kama hero..but we have seen how people have kicked him out. So hata Zim, Morgan akipewa mandate na wananchi..akavurunda, basi watamtoa kwa amani....kwa hiyo wale waliompigia kura walitumwa na wazungu kwamba wampigie kura Morgan? si ni wazimbabwe kama walivyo wengine? Sasa kwa nini leo tumhukumu Morgan kama kibaraka wa wazungu? Simply because ame-elicit support ya wazungu na waafrika wengine kama akina Fundi na Masanja?
People, politics za Africa ni ngumu sana. Usipokuwa makini..utaona kwamba kila kitu ni conspiracy ya wazungu. Kitu ambacho siyo kweli! Leo tunaambiwa pesa za EPA, MEREMETA nk..ZILIMSAIDIA Muungwana kushinda..now hiyo pesa Mbowe, Mrema, Lipumba..wataitoa wapi? Think about it! Na hatuna hata sheria makini ya kuweka playing level field kati ya wagombea..sasa leo tunaambiwa kwamba wapinzani..ni vibaraka wa wazungu, bila kuhoja maneno ya wale wanaotwambia hivyo!
Kwa Tanzania, its perfect example..kama JK is screwing up..then lets Tanzanians decide in 2010 to let him pack. Simple. Lakini huu mtego wa kuwa-crucify wapinzani eti wanakuwa sponsored na outsiders, wakati incumbents walioko madarakani wanatumia resources za SERIKALI ni kutowatendea haki. Zanzibar..mpaka leo CUF inaonewa kwa BRAND YA UARABU maana kwa hoja CCM hawawezi kuwashinda. Kitu ambacho Fundi, mimi na wengine tumekataa kuingia kwenye huo mtego wa viongozi wetu wanafiki ambao wameishiwa hoja na baadala yake wameamua name calling ndo iwe silaha badala ya hoja.
Masanja,