Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Nikimshitukia mtu hua sikosei na wala sirudii mara mbili... Niliyaona haya longtime....
Ati kakimbilia Ubalozi gani?... Wa - KABURU MATATA HIYAAAA!...yaani balozi zote za kiafrika hazina mpango...
 
yaani kutafakari kizimbabwe kama ndio kuangalia chini hadi kufumba macho

Ndivyo Kobe anvyotunga sheria mkuu! unajua mkuu jana nimesikiliza sana interview yake na BBC, ameulizwa sana kuwa kwa nini ubalozi wa Dutch na sio wengine? Majibu yake tu hata mimi nimeshituka kuwa something is not right na mkuu!
 
Nikimshitukia mtu hua sikosei na wala sirudii mara mbili... Niliyaona haya longtime....
Ati kakimbilia Ubalozi gani?... Wa - KABURU MATATA HIYAAAA!...yaani balozi zote za kiafrika hazina mpango...

Amekimbilia kwa wafadhili wake. Ubalozi wa SA ni mkubwa Zim kuliko nchi nyingine zote, lakini hakuuona. Kwa wanaokumbuka Bishop Abel Muzorewa, naona na huyu ndio hao hao. Kikwete katutia aibu sana kwa kuwa myopic.
 
.....are you this naive,seriously!

Bwana Koba,
Naive? No Matey, far wiser than you I know.... If I am, god-forbid, then I guess I am as silly as every ardent "New African" reader, Mbeki, Dos Santos nk... Hey, we all agree Mugabe should go (kazeeka, kama akina Omar Bongo na hata Museveni) but there really is only that stooge of a Morgan ambaye ameishakula pesa za watishi as an alternative... Afadhali Mugabe..Better the devil you know...
Jaribu kukata BBC, CNN na SKY from your diet any you may see things in another light
 
.... another BS piece of crap from one of these Mugabes idiots supporter!

Pole mzee, kama nilivyo kuambia, kata diet ya BBC, CCN, sijui marekani kuna nini nyingine? NBC... Karibu Afrika.. There are other sources of news in this part of the world..
 
kuna mwaka wakuu wa sadc kama sikosei
bw. morgan alishauriwa ahudhurie hicho kikao
ili akajenge hoja. kwa mshangao wangu huyu mkuu
alikwenda london kuonana na bw. blair na akatamka hadharani
kwamba mkutano wa sadc hautamsaidia kwani viongozi
wa kiafrika kazi yao kuteteana. naamini baada ya kauli hiyo
viongozi wengi wa sadc walimuona bomu.

binafsi baada ya hapo jamaa nilimuona kibaraka kwani niliamini
angekwenda sadc ajieleze halafu viongozi wa sadc wakijivuta ndio
awashutumu kwa kubebana. naona amerudia tena kosa lake kwa
kukimbilia ubalozi wa "wazungu".
 
Kitila Mkumbo,

Mkuu hakuna mtu anayetaka Mugabe azidi kutawala nchi hiyo maisha yake yote maadam wananchi wanamchagua, hii kweli ndiyo demokrasia!...Hapa mkuu utakuwa unaruidisha kile kinachopingwa toka awali..
Uchaguzi uliopita Mugabe alishinda kwa kura zaidi ya asilimia 80 baada ya mashambulizi mazito toka nchi za magharibi..Na Mugabe akatumia maneno yao kujipatia ushindi, hivyo tusije kusahau tulikotoka kwa sababu ya haya mauaji.
Kabla hata ya uchaguzi huo 2004/5 kama sikosei, Mugabe alikwisha wekewa vikwazo, kupakwa mavi kwa kila lugha..haikuanza jana ila yote haya yameanza toka swala la ardhi..
Kwa hiyo kitendo cha Mugabe kuua watu wake sii swala la ajabu ktk nchi za kiafrika hasa ukiwa na kiongozi mbovu kama Mugabe ambaye sasa swala la kuiongoza Zimbabwe analichukulia kama ni Wajibu wake..Kama akina Musharaf wa Pakistan..tofauti ni kuwa tu hao wengine wanapongezwa na nchi za magharibi lakini hawa wote wanatumia Ubabe kuongoza nchi.

Kwa hiyo tusitake kumvika kanzu mzee huyu kuwa anaweza kuongoza MAISHA! kama atachaguliwa.... Na nchi yeyote yenye utaratibu usiokuwa na mwisho wa awamu zakuongoza kwa kiongozi wake basi fahamu kuna Udikteta..

MDC mkuu haifaiu kabisa, huyu jamaa alikuwa kama Chiluba tu, mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi (labour movement) na kashinikizwa na Uingereza baada ya Mugabe kutangaza kuwa mwaka 2000 ardhi zinazomilikiwa na wazungu zitarudishwa kwa wananchi..kumbuka kwamba hawa MDC walikuwa wameunda muafaka na chama cha ISO na wakaja korofishana baada ya MDC kupinga swala la ardhi kuchukuliwa. MDC wakawafukuza hawa ISO toka ktk umoja wao..
Mkuu kuna vyama ambavyo vilikuwepo kabla ya MDC na swala la ardhi halijawa issue kubwa..MDC imekuwepo tu baada ya swala la ardhi kuwa agenda ya ZANU PF..

Binafsi huwezi kunambia kitu kwa sababu nawafahamu wazungu wanapokitaka kitu... Ziumbabwe kuna maslahi ya mzungu na kama unavyowasikia wao wakisema siku zote kuwa their interest comes first!.. hivyo usidhanie wanafanya hapa kazi ya kanisa..
Waafrika ndivyo tulivyo mkuu, nitarudia maneno yangu ya awali mwaka jana tu, kuwa swala la Zimbabwe ni sawa na ule mchezo wa kitoto..
Mzungu kachukua mchanga akamwambia Morgan....PUTA! - Morgan kaputa kisha mzungu kamgeukia Mugabe... loooh! jamaa kakutukania mama yako!... Ngumi, na bahati mbaya Mugabe mzima kamchakaza vizuri Morgan... kisha sisi huruma inarudi kuwa kamwonea mwenzie!..
Lakini ukweli wa picha hii wajinga ni sisi sote watazamaji, pamoja na huyo Mugabe na Morgan.. mzungu kuiweza kutuvuta na hiyo PUTA!..kisha akasema jamaa kakutukania mama yako na wewe kweli unaamini kuwa jamaa katukana wakati hukumsikia kwa mdomo wake akisema neno lolote!... kisha sisis tumejikusanya pembeni kutazama ngumi hizo badala ya kufikiria kuweka suluhu kabla ngumi hazijaiva..
Ujinga tumeuanzia mbali wakuu acheni tu tuishi kwa rehma za Mungu!
 

Lini wameacha kuteteana? Kiongozi gani wa kiafrika ametoswa na wenzake?
 
Kwa hiyo kitendo cha Mugabe kuua watu wake sii swala la ajabu ktk nchi za kiafrika hasa ukiwa na kiongozi mbovu kama Mugabe

Kweli ujinga tuliuanzia mbali!
 
Yap, ndio ukweli iwe kwa mtazamo wowote ule...
Sasa nikuulize huyo Morgan kama alijua viongozi wa Kiafrika kila siku huwa wanateteana na kuwa sababu yake muhimu asihudhulie kikao kile, ilikuwaje yeye apiganie tena UONGOZI ambao ungemweka ktk fungu hilo hilo la viongozi wa Kiafrika! au alikuwa na maana kuwa yeye angekuwa tofauti na mtetezi mwingine, Muingereza!. maanake haileti mankiti mtu kushutumu viongozi wa Africa hali wewe mwenyewe unagombea uongozi huo huo.
Mkuu huyu jamaa nomaa!... afadhali hata yule mwanamke nimesahau jina lake lakini akikua na hoja za msingi sana. Bahati mbaya ndio mfano wa Mrema...
 

Huyu Mzee hana dili. He was a hero to me when he was inside. When he agreed to play ball and sell out, yaani sijui namwonaje tu.
Hivi kwanini hakuja kwenye mazishi ya Nyerere? Kuna mtu kanikumbusha hapa.
 
Mugabe one of the worse dictators in living memory. Walikuwa wanamstahi alipofanya mauaji ya Bulawayo na mengineyo na kikosi chake cha CIO kwa mategemeo kwamba angejirudi sasa anakula nyama ya washona wenzake kwani alipokuwa anakula ya wandebele washona waliona sawa hivi sasa anakula kote kote.

Karibu kwenye Mugabe democracy. Ukisha anza kula nyama ya binadamu mwenzio huwezi kuacha. Miaka 28 bado unalalamika ati western propaganda kwa nini hukubadilika na kujijenga. Huyu Mugabe mnayemsifia ati anadiriki kusema malkia wa UK ni sawa lakini wale walio 10 downing street ndio wanamkwaza - absolutely a very SI. Atang'oka tu apende asipende.

Kinachowasumbua wengi ni Hypocrisy tu, Wazimbabwe walikuwa radhi kutawaliwa na Morgan Tsvangirai kwa kumpa kura nyingi lakini huyu babu kwa wizi wa wazi mwezi mzima na mbinu zake chafu. Who are we to choose for them ati hafai sasa nyie ndio mnafaa? Mbona Tanzania mlimchagua Che-nkapa, JK nk nani analalamika? Acheni hizo democracy haihitaji vigezo vyenu simple and clear. Ati kibaraka Je, Mugabe sio kibaraka au nyinyi sio vibaraka?
 

Haukunielewa kabla na bado haunielewi! Kwa mantiki yako wote wanaowashutumu viongozi wa kiafrika hawastahili kugombea uongozi. Unakiri Mugabe ni muuaji na hafai lakini kwa vile Morgan aliwa'snub' waafrika unaona heri huyo muuaji! Bado uko convoluted!
Iko kazi.
 
Fundi Mchundo,

Mkuu mimi mswahili na nakifahamu kiswahili vizuri, huna haja ya kupindisha tena... nambie ni wapi niliposema - Kheri huyo muuaji Mugabe!..usizuge tena maana hukosi pa kutokea...

Mkuu hivi kweli wewe unasoma between the lines au unarukia hoja tu!.. Hivi wote niliowataja kina Siad Bare, Saadam, Mobutu na wengine wote kwa picha ya Mugabe ina maana niliwaona wao ni bora..
Hakika huwezi kunielewa hata kidogo, Hili sio swala la kuruka mkojo na kukanyaga mavi... ni zito kuliko Mugabe na Morgan ambao wote wananuka kama viongozi. Na kama umesoma kwa makini nimependekeza watu wengine kabisa nje ya huyu Morgan ambaye anatumiwa na wazungu kama alivyo rais wa Iraq leo hii, rais wa Afghanstan, rais wa Misri, na ma pupet wengine ambao hata siku moja hawajaleta amani ktk nchi zao zaidi ya kuongeza hesabu ya mauaji kwa wananchi wake..Nampinga Morgan kwa sababu hiyo tu nje ya hapo sijali hata kama Mugabe akifa kesho..

As a fact hujui tu kwamba Mugabe sisi wengine tulimchoka toka mwalimu akiwa hai...Mwanzoi alitaka kuwafukuza wazungu wote!..Ni mwalimu aliyempa usia asiwafukuze wazungu wala kutaifisha mali zao, yatakuwa makosa makubwa hivyo wakashinikiza swala la ardhi kisheria. Wakiwa na kina Sithole, Nkomo na viongozi wengi tu, huyu Morgan hakuwa kati yao.. Muingereza akawageuka, MDC ikaundwa makhsusi kwa ajili ya kumwondoa Mugabe na kuwagawa Wazimbabwe..

Mkuu upewe maelezo gani zaidi kufikia hata kuiona nuru...Yote aliyoyafamnya Morgan yanapitia kwa mzungu kwanza na ndio maana kajichimbia ubalozi wa M Dutch -Kaburu. Huyu mkuu ni MNYAPALA....pupet wa Muingereza.
Mkuu kwa kheri ngoja nijinyooshe na luninga naipata LIVE birthday ya Mandela toka UK...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…