Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,065
- 136,438
Ule muda wa Davos umefika.
Viongozi mbalimbali duniani wako huko.
Neno la muhimu hapo ni “viongozi”.
Sasa, huyu mtawala wetu ambaye ni haramu, naye ataenda au keshaenda?
Au ndo kajificha huko anakojifichaga?
Alipoingia kwenye utawala alikuwa anapenda sana kwenda Ulaya na Marekani kuuza sura kwa kisingizio cha kuifungua nchi.
Ila baada ya kutuonyesha rangi zake halisi [uuaji na ukatili wa hali ya juu], sasa hivi kawa pariah.
Anajificha. Anaongea mambo ya ajabu ajabu. Leo anasema hiki, keshokutwa anasema kingine kinachokinzana na alichosema juzi.
Hiyo hali ni dalili ya mtu kuchanganyikiwa kichwani.
Endapo kaenda huko Davos, atakayemwona atustue……