Jamco_za,
Mkuu sio lazima tujenge uwanja kama huu ila jamani nasikia siku hizi hata ile mikonga ya abiria kuingia/kutoka ndani ya ndege pale JKN sii yote inafanya kazi..
Nchi yetu ina ndege sijui ngapi? (2) zinazoruka, lakini check hesabu ya wafanyakazi! Hivi kweli tunahitaji fedha na wataalam hata ktk maswala kama haya!
Mkuu Mkandara,
Wacha huo mkonga labda unahitaji technology, sisi tunashindwa hata kupeleka maji pale airport ndio tuanze kufikiria miradi mikubwa kama hiyo?
Hivi kweli hata kuweka mazingira ya maana tunahitaji investors? Unashangaa iweje hotel za kitalii kule mjini ziwe poa lakini kwenye airport kubwa kama ile tushindwa hata na usafi wa kwenye vyoo?